Kimsingi kuna mambo yanafikirisha sana. Hivi kwa mfano nimeenda zangu stationery, nikatengeza picha ya huyo mama, baadaye nikaona ni michosho!

Nikaamua kuichoma moto au kuichana, ndiyo nifungwe miaka miwili au kulipa faini ya milioni 5!

Learned fellows watatusaidia kujua imetumika sheria gani. Ili tuondoe aibu yetu mbele ya safari
 
Zamani walau madikteta uchwara waliweza kuzima uhuru wa maoni sababu ya nchi za dunia ya 3 zilikuwa gizani kiteknolojia.

Nakukumbusha tu taarifa ya kwanza kuwa Magufuli amefariki ilitolewa tarehe 9 March 2021 kwenye ukurasa wa Evarist Chahali ila jumuiya ya Tanzania ikatangaziwa 17 March 2021, ikimbukwe baada ya Magufuli kufungia mitandao kwa siku 5 tangu October 28 hadi November 3 mitandao mingine yote ilirudi isipokuwa twitter ambayo haikupatikana bila VPN kwa watumiaji wa Tanzania kwa takriban miezi 6 je ja taarifa ya kifo chake ikatokea mtandao alioufungia .

Jibu ni kuwa huwezi zuia nguvu ya umma , sauti za watu wote na mitandao kwa zama hizi ukifungia huku watu wanatokea
 
Kijana Shadrack Chaula (24) mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amehukumiwa faini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka miwili jela akishindwa kuilipa faini hiyo kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Julai 4, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Shamla Shehagiro.

Awali, mawakili wa Serikali, Veronica Mtafya na Rosemary Mginyi waliieleza Mahakama kuwa Julai 2, 2024 katika eneo la Ntokela mshtakiwa alisambaza video zenye taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok, kinyume cha kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandaoni.

Chaula ambaye pia ni msanii wa uchoraji, video yake ilisambaa mtandaoni Julai 2 akiwa anachoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, suala ambalo lilikemewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na kuagiza akamatwe.

====================

Mtakumbuka kuwa tarehe 02 Julai, 2024 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilitoa taarifa ya kukamatwa kwa Shadrack Yusuph Chaula [24], msanii wa sanaa ya uchoraji, Mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndanto Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya kutokana na tuhuma za kuchoma picha Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kujirekodi huku akitamka maneno yenye kuashiria uvunjifu wa sheria za nchi.

Leo Julai 04, 2024 mtuhumiwa amefikishwa mahakamani katika Mahakama ya Wilaya ya Rungwe kwa kosa la kuaandaa na kusambaza taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya kimtandao ya mwaka 2015 ambapo alikiri kosa na alipatikana na hatia na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili Jela au kulipa faini kiasi cha shilingi milioni tano.

Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.


Pia soma===>>>
Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake
Kumbe kesi zinaweza kwenda kasi hiv? Mahabusu wanakaa muda mrefu Kwa nn? Au kuna aina za kesi? Na uhusiano wa kesi inamhusu nani?
 
Jambo la huyu kijana kuchoma picha ya Rais,ni ishara kwa watawala kwamba HAMKANI SI SHWARI TENA.Na PANAPOFUKA MOSHI KUNA MOTO
 
Back
Top Bottom