Upuuzi mtupu 🚮 kuna matatizo kibao katika hii jamii, hayatatuliwi. Kuna watu wana kesi za kubambikiwa wanaozea magerezani. Picha mnaithamini kuliko uhai wa wanachi wanaokosa dawa, vifaa tiba.

Watoto wanatembea kilomita nyingi, kufuata shule. Mmeshindwa kuyatatua haya na mengine, mnaweza kutatua adhabu ya picha ndani ya wiki. Takataka kabisa ...
 
Atatoka soon...na hao firauni wenzako hawatafanya hivi daima...jinsi mambo yanavyokwenda hawataenjoy huu upuuzi kwa muda mrefu....picha ya Samia inafungiwa maandazi kila siku...picha yake si msahafu.
Majizi ya kodi za masikini yangekuwa yanahukumiwa haraka hivi si tungekuwa mbali.
Fursa tele mtaani hio hela ya kulipa faini mtaji tosha ukiwa na akili ya kuchomoka
 
Wakati huo mafisadi wakiwa mitaani au kesi zao kuunguruma kwa miaka...
 
Kijana Shadrack Chaula (24) mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amehukumiwa faini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka miwili jela akishindwa kuilipa faini hiyo kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Julai 4, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Shamla Shehagiro.

Awali, mawakili wa Serikali, Veronica Mtafya na Rosemary Mginyi waliieleza Mahakama kuwa Julai 2, 2024 katika eneo la Ntokela mshtakiwa alisambaza video zenye taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok, kinyume cha kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandaoni.

Chaula ambaye pia ni msanii wa uchoraji, video yake ilisambaa mtandaoni Julai 2 akiwa anachoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, suala ambalo lilikemewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na kuagiza akamatwe.

Mwananchi

Pia soma===>>> Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake
Kesi imeendeshwa faster? Andaeni utaratibu wa michango kule X
 
Huyu si ndo alitoa mpaka location yake kwamba haogopi😂😂😂

Haya tuone sasa
Hivi unadhani udhalimu unaweza kushinda haki? Haki ina tabia ya kuchelewa lakini mwishowe hufika. Unaweza kuwa uraiani na unadhani uko huru kumbe huu udiktekta kesho unagonga hodi nyumbani kwako
 
Uonevu!

Usipambane na mtu aliyekuzidi pesa, cheo au watu nyuma yake kama wewe hauna hivyo vitu au back up!

Funika kombe mwanaharamu apite..!🤸
Duniani watu wangekuwa na akili kama zako ungekuta tunaishi kama wanyama. Anyways ni watanzania wengi wana mawazo kama yako na ndiyo maana nchi inazidi kudidimia.
 
CHADEMA wakiongozwa na Erythrocyte wamchangie asitupwe gerezani!
Hakuna aliye salama kwenye utawala wa kidhalimu. Muulize Kinana au hata Kikwete. Ni suala la muda tu. Ni kama nyumbu aliyeko mbugani anacheka simba anapokamata mwenzake.
 
Tumekabidhi madaraka jitu shamba sana.limechafua Nchi Kwa kuweka mabango ya picha yake ambayo yamegeuka kuwa uchafu.
 
Hiyo unaogopa wewe woga ni ujinga, kumbuka alitaja mpaka alipo alijua kinachofuata Imani yake imeshinda miaka miwili kitu gani Kwa jambo ulilosimamia likafanikiwa. Tayari ujumbe umefika duniani kote
Sababu alizo zipigania za ushoga si kubwa kiasi hicho nchini kwetu mpaka ajitoe muhanga afungwe mimi kwa maoni yangu polisi wangemchukua na kwenda kumpima akili hata kama wangemkuta ana akili timamu wao wangesema tu karukwa na Akili basi. Kuna mambo mengine watu wanayakuza wakati wala siyo issue yoyote. Kubwa.
 
Hiyo unaogopa wewe woga ni ujinga, kumbuka alitaja mpaka alipo alijua kinachofuata Imani yake imeshinda miaka miwili kitu gani Kwa jambo ulilosimamia likafanikiwa. Tayari ujumbe umefika duniani kote

Endeleeni kuwajaza ujinga. Play stupid games win stupid prizes.
 
Upuuzi mtupu 🚮 kuna matatizo kibao katika hii jamii, hayatatuliwi. Kuna watu ana kesi za kubambikiwa wanaozea magerezani. Picha mnaithamini kuliko uhai wa wanachi wanaokosa dawa, vifaa tiba.

Watoto wanatembea kilomita nyingi, kufuata shule. Mmeshindwa kuyatatua haya na mengine, mnaweza kutatua adhabu ya picha ndani ya wiki. Takataka kabisa ...
DPP, POLICE, MAHAKAMA havihusiani na ujenzi wa miundombinu wala kuleta dawa majukumu yao ndo hayo waliyo tekeleza na wanalipwa kwaajili hiyo.
 
DPP, POLICE, MAHAKAMA havihusiani na ujenzi wa miundombinu wala kuleta dawa majukumu yao ndo hayo waliyo tekeleza na wanalipwa kwaajili hiyo.
Wewe naye sijui umetokea wapi. Aliyeliibua hili ni mkuu wa mkoa, na akasema akamatwe. Huyo kamaliza shida zote za mkoa wake? Ikabaki ya picha tu. Hapa hatuzungumzii kazi ya nani na nani. Wewe kama comment ya mtu huielewi ipite tu.
 
Back
Top Bottom