Kamanda Asiyechoka
JF-Expert Member
- Sep 13, 2020
- 3,315
- 5,052
Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Julai 4, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Shamla Shehagiro.
Awali, mawakili wa Serikali, Veronica Mtafya na Rosemary Mginyi waliieleza Mahakama kuwa Julai 2, 2024 katika eneo la Ntokela mshtakiwa alisambaza video zenye taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok, kinyume cha kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandaoni.
Chaula ambaye pia ni msanii wa uchoraji, video yake ilisambaa mtandaoni Julai 2 akiwa anachoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, suala ambalo lilikemewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na kuagiza akamatwe.
====================
Mtakumbuka kuwa tarehe 02 Julai, 2024 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilitoa taarifa ya kukamatwa kwa Shadrack Yusuph Chaula [24], msanii wa sanaa ya uchoraji, Mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndanto Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya kutokana na tuhuma za kuchoma picha Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kujirekodi huku akitamka maneno yenye kuashiria uvunjifu wa sheria za nchi.
Leo Julai 04, 2024 mtuhumiwa amefikishwa mahakamani katika Mahakama ya Wilaya ya Rungwe kwa kosa la kuaandaa na kusambaza taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya kimtandao ya mwaka 2015 ambapo alikiri kosa na alipatikana na hatia na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili Jela au kulipa faini kiasi cha shilingi milioni tano.
Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Pia soma===>>> Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake