GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,024
- 119,543
Najua kuna watu watakuja hapa kunishanga na kunishambulia ila kwakuwa huwa najiamini kwa kile ambacho nakisema na nakimaanisha wala sitojali. Narudia tena Mpambe yoyote yule wa Rais (ADC) tena akiwa na Sare zake za Kijeshi huwa haruhusiwi Kucheka au Kutabasamu katika Mazingira yoyote yale awapo na Boss wake ambaye Kimedani ni CIC (Amiri Jeshi Mkuu).
Hivyo huyu ADC wa Rais Samia tafadhali watu wa Protokali wa Kijeshi wamkumbushe kuwa hatakiwi kufanya hivyo kama ambavyo anaonekana amefanya katika Ukurasa wa X (zamani Twitter) wa Rais Samia huku pembeni yake (kulia kwake) akiwa na muota ndoto za alinacha kuwa siku moja atakuja kuwa Rais wa Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba.
Na nashauri ambao mtanishangaa kwa huu Uzi watafuteni kwanza watu wa Protokali za Kijeshi na TISS wawaelimishe Ok?