Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,884
Chama cha Mapinduzi kiliahidi Wananchi ahadi kedekede mwaka 2015 kupitia Ilani yao. Hata hivyo utekelezaji wa Ilani Katika miaka 5 ni 31% tu hivyo kupata alama D. Baadhi ya maeneo ambayo CCM haikutekeleza Ilani ni Pamoja na
1. Ibara ya 20(h)(ii) CCM waliahidi Kukamilisha hatua za kuanzisha Akaunti ya Fedha ya Pamoja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. HAIJATEKELEZWA
2. Kwenye Sekta ya Kilimo Ibara 22(c) CCM waliahidi Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 461,326 mwaka 2014 mpaka 1,000,000 mwaka 2020. Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya Mwaka 2020 Eneo la Umwagiliaji ni Hekta 461,326. Bajeti ya Sekta ya kilimo ilikuwa Sh. 1.08T mwaka 2015, imeshushwa mpaka Sh 201 Bilioni Mwaka 2020.
3. Kwenye Sekta ya MIFUGO: CCM waliahidi Ahadi 17 (uk.10-20) hakuna hata moja iliyotekelezwa.
4. Kwenye Sekta ya Uvuvi kuna
Ahadi 16 (uk. 21-22) hakuna iliyotekelezwa. Kwa Mfano waliahidi kununua Meli 5 za uvuvi Bahari Kuu na kujenga Bandari ya Uvuvi ukanda wa Pwani.HAIJATEKELEZWA.
5. Kwenye Sekta ya Viwanda CCM iliahidi Kuongeza mchango kwenye Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kutoka 9.9% mwaka 2015 mpaka 15% mwaka 2020 (uk.31). Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa Sekta ya Viwanda ilichangia 8.5% tu kwa Pato la Taifa. ( Hali ya Uchumi wa Taifa 2020, Wizara ya Fedha Uk. 3). Mradi wa Mchuchuma na Liganga Uk. 31 kama sehemu Ujenzi wa Viwanda mama. HAUJATEKELEZWA.
Hali ya Mauzo Nje kulinganisha Mwaka 2015 na Mwaka 2020
- Bidhaa za Viwanda Mwaka 2015 mauzo USD 1.4 Bilioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 800 Milioni
- Bidhaa za Maua na mboga mboga Mwaka 2015 Mauzo USD 960 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 174 Milioni
- Bidhaa za Samaki Mwaka 2015 Mauzo USD 402 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpak USD 155 Milioni
6. Kwenye Sekta Usafirishaji CCM waliahidi “Kwa ushirikiano wa Sekta Binafsi kuanza ujenzi wa reli zifuatazo;
Dar – Tabora – Kigoma
Uvinza – Msongati
Isaka – Kigali
Mtwara – Songea – Mbamba Bay (Mchuchuma na Liganga )”
Hata hivyo Serikali inatekelezwa hili kwa mikopp ghali.
7. Kwenye Sekta ya MAFUTA NA GESI ASILIA Ibara ya 44(d) CCM waliahidi Kuendeleza mradi wa Gesi (LNG) uk 71. Mradi huo HAUJATEKELEZWA.
8. Kwenye Sekta ya MAJI: CCM iliahidi Watu 85% kuwa na Maji safi na salama mwaka 2020, Lakini mpaka sasa ni 67% tu ya Watu Vijijini wanapata Maji uk.99. Waliahidi kujenga Bwawa la Kidunda, HALIJAJENGWA.
9. Kwa upande wa UWEZESHAJI wa Wananchi Ibara ya 57(d) uk.105 ya Ilani waliahidi kutenga Kiasi si cha Sh. 50M kwa kila Kijiji kama mfuko wa mzunguko (Revolving Fund). HAWAJATEKELEZA
10. Vile vile CCM waliahidi Ibara ya 57E(v) Kuanzisha mfuko mkubwa wa kitaifa wa wajasiliamali wadogo na wa kati kwa ushirikiano na mfuko wa hifadhi ya jamii. HAIKUTEKELEZWA. Badala yake Wampewa vitambulisho. Hata wanaotelekea nyanya chini wanatozwa pesa za vitambulisho.
11. Kwa upande wa AJIRA waliahidi kutengeneza Ajira Milioni Moja Katika miaka 5. ( uk. 4, 8, 9, & 10 )
Watanzania wana wajibu wa kuikataa CCM ifikapo Oktoba 28, 2020 na kuchagua ACT Wazalendo na Vyama vingine vya Upinzani ili kurejesha furaha kwenye nyoyo za Watanzania
Agosti 2020