Zitto Anataka kusema nini?

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Wana JF,

Katika ukrasa wake wa facebook zito kaandika haya,
Kwa kuwa tumeamua kupambana dhidi ya rushwa, hongo, ufisadi, uzembe na uvivu;

Kwa kuwa tumeamua kuhakikisha kuwa mali asili ya Nchi yetu Tanzania ni mali ya wananchi wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini nchini kwetu na kuleta maendeleo sawia na endelevu ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa;

Kwa kuwa tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na lililo juu ya misingi ya haki kwa watu wake wote;

Kwa kuwa tumeamua kushiriki katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili kuwaenzi waasisi wa ukombozi wa Mwafrika na kujenga kontinenti lenye sauti yenye nguvu na ushawishi katika jamii ya mataifa ulimwenguni;

Kwa kuwa tumeamua kupigania demokrasia, uhuru wa mawazo, umoja, utu, uadilifu, uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa na Amani;

Kwa kuwa kwa nia moja tumeamua kujenga chama cha mrengo wa kushoto chenye kufuata misingi ya Demokrasia ya Kijamii (Social Democracy),

Demokrasia ya Rasilimali na misingi asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) kama Azimio la Arusha ; na

Kwa wajibu tulio nao wa kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia na utamaduni wa mfumo wa vyama vingi Tanzania;

Hivyo basi..........."


Sijui anataka kumaliziaje!

Hapo kwenye unyerere sijamuelewa anamaanisha Nyerere Msanii au marehemu Julius Nyerere? Unyerere wa vitendo ni pamoja na kuachia ngazi zote alizo nazo ikiwa ni pamoja na uenyekiti wa PAC, ambapo atapoteza na kile cheo alichopata juzi juzi kwenye kamati ya PAC za Africa, aachie Ubunge arudi Kigoma kukuza wakala wa CCM.
 
Kwa kuwa tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na lililo juu ya misingi ya haki kwa watu wake wote;.
Yes, Chama kinachoasisiwa kwa muundo wa kuwarubuni viongozi wa vyama vya upinzani ni cha kuogopa kama UKOMA.
 
Zitto, hawezi Achiba posho za PAC ki rahisi namna hiyo.....anawagilibu wakina Kitila yeye anasubiri kuvuta za Bunge la katiba kwanza na za mashirika ya umma .....NHC watamuumbua soon....
 
Kwa kuwa kwa nia moja tumeamua kujenga chama cha mrengo wa kushoto chenye kufuata misingi ya Demokrasia ya Kijamii (Social Democracy), Demokrasia ya Rasilimali na misingi asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) kama Azimio la Arusha ;
Upo sahihi anapaswa kuachia nafasi zake kwa kuwa zimetokana na CHADEMA kwa kuwa tayari hapo amekiri kuanzisha ACT.
 
Semeni na kuandika ninyi, wengine wakisema viazi! Siasa za nchi hii ndo mtagundua kuwa watz wanauwezo wa kuchuja, kuamua na kufuata njia waipendayo. ZZK moto mkali sana, najua hamtaamini mpaka iwachome!
 
Huyu dogo asiwaumize vichwa kwani kishachanganyikiwa na ndo maana anajidai hatagombea Ubunge kwani ameshanusa upepo na kujua hatima mbaya kwake
 
zitto atawachezea sana watanzania wengi hasa wale wavivu wa kufikiri, zitto atawatumia sana vijana wengi hasa wale wasaka tonge na wale wasomi walio weka akili zao mifukoni na kuamuwa kutumika kama dekio
 
CHADEMA ni lazima mjiandae kisaikolojia, huyu kijana ni tishio kwa msatakabali wa chama chenu ambacho mwanzoni mlijivua nguvu ya vijana, nguvu ambayo hapana shaka sasa inayumba yumba ikisubiri kuona ZITTO KABWE anaweka wapi mizizi.
 
zitto atawachezea sana watanzania wengi hasa wale wavivu wa kufikiri, zitto atawatumia sana vijana wengi hasa wale wasaka tonge na wale wasomi walio weka akili zao mifukoni na kuamuwa kutumika kama dekio

mmmmmmmmmm, usianze kuwa na mashaka na vijana wengi, huo ndiyo ukweli kwamba vijana wanamtaka kijana kama ZITTO na si vinginevyo, wewe kama unajijua ni mzee shauri yako manake uzee siyo lazima umri, unaweza kuzeeka hata kwa fikira. Lazima kijana yoyote mpenda maendeleo amuunge mkono ZITTO KABWE.
 
Zito akiondoka atakitikisa chama lakini hataweza kufikia lengo la kuua harakati hizi kamwe! Ataingia kwenye historia ya Mrema na atakwisha kisiasa taratibu.
 
CDM endeleeni kushikilia ukweli kuwa chama hiki kimeanzishwa ili kuwavuruga,mkimwaga hiyo sumu vizuri itazaa matunda.
 
mmmmmmmmmm, usianze kuwa na mashaka na vijana wengi, huo ndiyo ukweli kwamba vijana wanamtaka kijana kama ZITTO na si vinginevyo, wewe kama unajijua ni mzee shauri yako manake uzee siyo lazima umri, unaweza kuzeeka hata kwa fikira. Lazima kijana yoyote mpenda maendeleo amuunge mkono ZITTO KABWE.
Katika hali ya Kimungu (yaani perfection) tunasema mtu akifanya mambo mia moja kati yake 95 mabaya alafu 5 mazuri basi tuangalie mazuri na tusahau mabaya ili kumpa moyo lakini katika hali halisi ya kidunia inakuwa kinyume, hata akifanya mazuri 95 bado tutaangalia mabaya 5!
Kwa maana hiyo huyu bwana anakuja kihivi lakini hayuko wazi na malengo yake hayaeleweki kwa watu wanaofikiri kwa umakini. Kumbuka hata hiyo ccm hatuipendi lakini kuna baadhi ya mazuri imefanya!
Zitto ataeleweka kwa kuweka wazi tuhuma zinazomkabili na hata zile ndogo kama za NSSF na Wasanii.
Sio ajabu hata anavyopost maandiko yake inakuwa 'kitafsida' zaidi.
 
CHADEMA ni lazima mjiandae kisaikolojia, huyu kijana ni tishio kwa msatakabali wa chama chenu ambacho mwanzoni mlijivua nguvu ya vijana, nguvu ambayo hapana shaka sasa inayumba yumba ikisubiri kuona ZITTO KABWE anaweka wapi mizizi.

Naomba unipe majibu ya haya maswali:
(1). Kama ni kweli Zitto alikuwa na nguvu ndani ya Chadema ni kwa nini viti vya madiwani vilipungua?

(2). Na kwa kuwa Zitto ananguvu ndani ya Chadema kwa nini hakuongeza mbunge hata mmoja wakawa wawili na kiendeleza mapambano ya ukombozi?
 
Back
Top Bottom