Yapi ni maji bora kwa ajili ya kunywa?

baada yakuwa wa mjini ukakataa maji ya asili yako! yapo na yale yaliyochemshiwa kuni yananukia moshi...😅
humu duniani kasheshe ni nyingi..
Mazoea hujenga tabia 🤣
Unashangaa maji? Chakula flani ukikaa miaka hujapika siku ya kupika lazima upoteane.
 
Usalama wake ni upi huo?
Maji ambayo hayana nutrients bado tuyaite salama
Hizo nutrients tutazipata kwenye vyanzo vingine
Lakini Nutrients haziwezi kuzuia maji kuwa safi na salama
Kama kuna uwezekano wa kuongeza hizo nutrients bila kuathiri usalama wake basi yatafaa sana
"Tawile Tawile......"
 
Inategemeana na unaishi wapi!! Ukae Tandale halafu unywe maji ya Chem Chem!! Kila siku utakuwa mgeni wa typhoid.

Mimi nilishakimbia mjini mkuu,naishi nje ya mji kabisa!55kms from Mbeya town,ubavuni kabisa mwa mlima Rungwe,huku maji siyo changamoto kwa kweli.
 
Wazee kitu kinaitwa shabu,sijui kitaalamu..je kina tibu maji,zamani nilikua naona mama akiweka kwenye maji kwa dk kadhaa na maji kujichuja vizuri..na je kina madhara yoyote ukiitumia.
 
Wazee kitu kinaitwa shabu,sijui kitaalamu..je kina tibu maji,zamani nilikua naona mama akiweka kwenye maji kwa dk kadhaa na maji kujichuja vizuri..na je kina madhara yoyote ukiitumia.
Shabu ni kitu gani?
 
S
Maji yakishachemshwa ni hatari kwa afya pia.
Usipochemsha unakutana na bacterias
Ukichemsha unakutana na chemicals. (madini yaliyo kwenye chuma zilizotengeneza sufuria.)
sasa hata chakula kilichopikwa kwa sufuria ni hatari sana,.. Maana sufuria kila siku inakwanguliwa na steelwire,.. bado chakula hichohicho kinapakuliwa na kuwekwa kwenye bakuli na sahani za plastics.

Kila kitu kina ubaya wake, tunaangalia tu namna ya kupunguza ubaya wake.
 
Hapo sawa.
 
Nyumbani kwetu maji ni ya bomba kisha wanayachemsha. Nikawa mbali almost 2yrs+, siku nimeenda yakanishinda kabisa kunywa.. nikatafuta ya chupa niliyozoea

Kaskazini maji mazuri ni Kilimanjaro, Dew drop, Jibu & Shafii water.
Hata SEQUA nayo ni mazuri sana

Chanzo cha maji yote Kaskazini ni mito mikubwa na chemichemi kitu kinachoyafanya yawe na ladha asili pamoja na kuwa huwekwa chemical kuyahifadhi.
 
afu utashangaa anaeulza iv anaandka uku kashkilia chupa ya coca au kikopo cha master au kitoko.

ila anaogopa chemicals za kwenye Kilimanjaro drinking water

😆😆
 
Hata SEQUA nayo ni mazuri sana

Chanzo cha maji yote Kaskazini ni mito mikubwa na chemichemi kitu kinachoyafanya yawe na ladha asili pamoja na kuwa huwekwa chemical kuyahifadhi.
Sequa siyafahamu.

Hayo shafii ukute yana ubaridi ule wa hali ya hewa,, ni matamu, unakunywa maji unaenjoy.

Nakubaliana na hoja yako. Kuna waterfall 1 nilikunywaga maji yake… yalikuwa poaa sana
 
1. Maji ya mvua
Kuna watalaam wanasema sio salama kwakuwa yana chemicalza huko angani
Kuna wengine wanasema ndo salama kwakuwa ni asilia, yamejichuja na yapo salama

2. Maji ya dukani
Haya ambayo yapo kwenye machupa
Mfano hill water, jambo, afya n.k
Kuna watalaam wanasema sio salama kwa kuwa yameongezea chemicals za kuyasafisha yawe meupe yani ule weupe sio asilia na yana madhara

3 maji ya bomba
Wengine wanasema ni maji mazuri tuyaamini kwakuwa yana madini yanatoka kwenye mwamba japo yana rangi mbaya ambayo binafsi siyaamini.
Na process yote hadi yafike kwa mteja yanakuwa yamewekewa madawa

Wataalam naomba mnisaidie niwe nakunywa maji gani yenye virutubisho vya mwili
Chemsha Maji ya Kunywa vizuri, yachuje na kuyapooza, hayo ni maji sio tu Bora, bali pia safi na salama Zaidi kwa afya yako binafsi na familia yako kwa ujumla 🐒

na gharama za kununua maji, kutibu maji na mardhi baada ya kunywa maji chafu utakua umezikwepa
 
Back
Top Bottom