Yaliyojiri kwenye ukaguzi wa Polisi katika Ofisi za JamiiForums na Nyumbani kwa Mkurugenzi, Maxence

image.jpg

JE MLIO MKAMATA MELO MNAJUA UMUHIMU WA JF KWA SERIKARI AU KIMBELEMBELE TU?
 
Hata wakienda ofisini hakuna watakachofanya, Data za JF zote zipo kwenye datacentre zilizopo nje ya nchi.
Sanasana labda kama wakiomba jamaa wawape password kulogin kwenye server wao wenyewe kitu ambacho JF wana haki ya kugoma, hili swala mwisho wa siku wata-lose tu watake wasitake labda wajitoe akili watumie mabavu.
Inasikitisha sana- hasa waki kutana vilaza-
 
NDUGU YANGU MAGUFULI Achana Na JF - was hard to build this- geelimbe@hotmail.com hao wanao ji fanya washauri wa usalama wa Internet wana kazi nyingine za kufanya - JF Ni kazi ya ofisini-! Faza lekagi-
 


Leo mida ya mchana, polisi kutoka kituo cha Kati, Dar es salaam wakiambatana na Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Ndugu Maxence Melo, walifika katika ofisi za Jamii Media kwa ajili ya ukaguzi.

Zoezi hilo limekwenda sambamba na kuwahoji wafanyakazi (Social Media Engagers na Content Quality Controllers) juu ya utendaji wa shughuli zao za kila siku.
Baada ya ukaguzi na mahojiano, polisi wameondoka na nyaraka za usajili wa Jamii Media ikiwemo cheti cha mlipa kodi, cheti cha BRELA, leseni ya biashara, n.k.

Pia polisi imewachukua wafanyakazi wawili kwa mahojiano zaidi.

Polisi wameelekea nyumbani kwa Maxence Melo ambako nako wamefanya ukaguzi ndani ya nyumba. Katika zoezi zima la ukaguzi, sehemu zote mbili, Jeshi la Polisi halikuhitaji wala kuchukua kifaa cha mawasiliano ya kimtandao kama router, flash, hard disc, au kompyuta.

Msafara umeelekea Polisi kituo cha kati kukamilisha mahojiano kati ya Mkurugenzi na wafanyakazi wawili waliochukuliwa.

Tunaomba umma utambue kwamba Jamii Media haina servers wala min-server ofisini kwake, nchini Tanzania wala Afrika. Pili, tunaomba watumiaji wa JamiiForums.com wasitiwe wasiwasi juu ya usalama wa taarifa zao. Teknolojia tunayoitumia (encryption) kumsajili mtumiaji wa JamiiForums.com haituwezeshi kumfahamu mtumiaji yeyote labda yeye akubali kwa hiari yake kujiweka wazi mtandaoni.

Imetolewa na Uongozi,
Jamii Media.

Eehh sasa ndio kusema wanafanya upekuzi

Hata wakienda ofisini hakuna watakachofanya, Data za JF zote zipo kwenye datacentre zilizopo nje ya nchi.
Sanasana labda kama wakiomba jamaa wawape password kulogin kwenye server wao wenyewe kitu ambacho JF wana haki ya kugoma, hili swala mwisho wa siku wata-lose tu watake wasitake labda wajitoe akili watumie mabavu.
Walifikiri watakuta server imefichwa nyumbani ili waipeleke kituo cha polisi kati.

Masikini polisi wale hawaelewi masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano, kuwa jf ipo hosted off-site na nje ya Afrika.
 
Tutachangia tu mkuu. Sidhani kama polisi wanajua chochote kuhusu mambo ya high tech. Nikitu kinashangaza kumlazimisha mtu atoe majina ya wateja wake wakati wanalindwa na privacy law. Polisi wetu OMG. ndo shida ya kuchukuwa failures na kuwaingiza kwenye majeshi hahahahaha ngoja nicheke kidogo ili niongeze siku.
Walifikiri watakuta mafaili (ya makaratasi) yenye majina ya wateja yamefichwa nyumbani kwa Mello, kumbe kitu kipo hosted cloud kidigitali.
 
Online media kama jf vifaa vyake vingi ni software na applications mbalimbali. Sasa hivyo vitu vinapekulika? Kwani ni mafaili na makabrasha?
Inawezekana, ila kitendo cha kupekuwa na kuvuka vizingiti vya usalama kwenye mifumo ya kompyuta Na kunakini taarifa kinaitwa udukuzi (hacking).

Hacking ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya mitandao.

Je polisi wapo tayari kufanya hili?
 
huyu si mpuuzi wa lumumba unadhani ana akili basi wanaongeaga upuuzi humu hataree hawana hoja za maana kwao neno lowassa kiroba na upuuzi kama huo alioandika melo haumii lolote tutakao umia ni sisi sasa ameshikiwa mtutu analazimishwa kutoa majina yetu na ip adress ili mtu ajulikane.............
Ondoa shaka mkuu, username nyingi si majina halisi ya wateja. Pili IP Address zinazotolewa na mobile ISP ni za mafungu, yana IP address moja ina watumiaji 100.
 
hivi mnafikiri kina Melo na Mwanakijiji walivyo sema hapa ni mahali pa great thinkers walikosea ? Wanachowaza leo wenzao waliwaza miaka 10 iliyopita ..hivi wanaelewa hata Cloud computing inavyofanya kazi kwa mfano ? Hata tusigusie servers maana sijawahi kuona watu kama polisi
Cloud computing ni giza nene kwa jeshi la polisi.
 
Kwa heshima na taadhima Rais Dr John Magufuli tunaomba uingilie kati suala la Max kutiwa nguvuni na polisi. Max aachiwe huru kuendeleza na kukuza uhuru wa raia kupata na kutoa habari.

Tunaheshimu polisi na ufanyaji wao wa kazi uliotukuka ila kwa hapa naona watapitiliza. Kama kuna vitu ambavyo polisi wanaona virekebishwe humu JF, mawazo yao yanakaribishwa pasipo kubughudhi, kuzuia au kuathiri kwa namna yeyote jukwaa hili. Ni mara nyingi nimemsoma Invisible na wenzake wakiomba members watoe mawazo ya kuboresha JF. Mawazo ambayo mara yametumika kuunda na kuboresha JF hadi kufikia hapa.

Tunaomba Max aachiwe huru.
 
Mtu kama max kajiajiri na kaajiri vijana.. Badala ya kum support jf iende hadi west africa wao wanamuweka ndani.
Mwisho wao hawa jamaa sio mzuri..
Nina uhakika 2020 watakuwa kama yule jamaa wa Gambia
selikari inayochukia sekta binafsi haitaki secta binafsi iendeshe uchumi.eti wanalinda madaraka yasiwaponyoke.
 
Sikuwahi kufikiria Ujinga huu... Tatizo viongozi wana fikiri wao ndio Kila kitu...haya gusagusa Sasa HAPA Sasa ndo mmeshika tako la CHUKI....
 
U
Walifikiri watakuta mafaili (ya makaratasi) yenye majina ya wateja yamefichwa nyumbani kwa Mello, kumbe kitu kipo hosted cloud kidigitali.
Uwezo finyu- kukamatwa MELO Ni Kama kuanika akili adhalani-
Kama kuvaa Kanzu bila CHUpi alafu unapita tiktak-
 
Back
Top Bottom