BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,482
- 8,336
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema idadi ya Vifo vya Wajawazito vimepungua kutoka Vifo 556 vilivyotokea mwaka 2016 hadi kufikia Vifo 104 kwa kila Vizazi Hai 100,000
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2024/25 Bungeni, pia, Waziri Ummy amesema Vifo vya Watoto wenye chini ya Miaka 5 vimepungua kutoka 67 hadi 34 kwa kila Vizazi 1,000
Aidha, Vifo vitokanavyo na UKIMWI vimepungua kutoka Vifo 29,000 vilivyotokea mwaka 2022 hadi Vifo 22,000 vilivyotokea hadi kufikia Machi 2024. Vifo vilivyotokana na Kifua Kikuu (TB) vimepungua kutoka 25,800 mwaka 2022 hadi 18,100 Machi 2024.