Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Watumishi wa Afya walioajiriwa september 2013 na 2014 kwa sasa wana miaka takribani 6 mpaka 7 kazini na hawajawahi kupandishwa madaraja ya mishahara yao ambao ni Takwa la kisheria

Mnaahidi watapandishwa LINI? SABABU ZA MSINGI

KUWACHELEWESHEA HAKI YAO NI NINI?
 
Poleni na kazi watendaji na watalaam wetu. Mi naomba ile namba ya Amana referral Hospital mlioweka kama contact number mnazoweka ziwe zinafanya kazi, mfano namba +255 22 286 1902 ukipiga unapata majibu " Sorry the call is not through, because the callee has not paid the bills" tunajua mnatumia namba za mkononi kwa ajili ya kazi za ofisi lakini hii ni kero kubwa sana

Karibu Idara zote za serikali wana tatizo hilo, Ila kwa muhimu wa TAASISI yenu tunaomba mtuwekee namba inayofanya kazi , maana kama ni bili hailipwi leo wala kesho. najua itachukua muda mrefu kutatua hilo ila naomba tu utujulishe kama huu ujumbe umeusoma na unashughulikia, itatosha, sisi tutasubiri hata kama mtarekebisha 2021/ - 2030 hatujali tumevumilia mengi sana.
 
Mimi niwapongeze sana wizara ya afya kwa mageuzi makubwa ya sekta ya afya nchini

1.Kumekua na madaktari bingwa wa kutosha pamoja na vitendea kazi vifaa tiba katika hospitali zetu za mikoa na rufaa

2.Kumekua na uboreshwaji mkubwa wa huduma kwa wagonjwa ( Customer care) siku hizi matusi, kupuuzwa na dharau kwa wagonjwa vimepungua sana kama sio kwisha kabisa

3.Kumekua na ongezeko la watendaji, maboresho ya hospitali, kujengwa kwa hospitali mpya na vituo vya afya kwenye kata zetu na vijiji, hata wale waliokua hawajui hospitali siku hizi wanazijua na wanapata huduma

4.Kumekua na uboreshwaji wa bima ya afya ya taifa. Siku hizi watu wa NHIF hatudharauliki kama awali. Nimeshuhudia mke wa ndugu yangu ambae mumewe ni mwalimu na yeye mama wa nyumbani akifanyiwa upasuaji wa moyo kwa kutumia NHIF bila kikwazo na kupona. Hongera sana MNH

5.Niseme pia kumekua na huduma bora zaidi hospitali za serikali na hospitali na mashirika ya kijamii/dini kuliko hospitali binafsi. Kwakuwa nyie ndio wasimamizi mtusaidie wananchi kujua tatizo ni nini. Kuna hospitali ambazo ukifika mjamzito kujifungua wanakushawishi kufanya upasuaji sijui hili limekaaje kiafya

Ushauri
1.Matibabu ni gharama sana na watanzania wengi hawana uwezo wa matibabu. Tunaomba nyie na NHIF muandae mpango mzuri na rahisi wa kila mtanzania kuchangia bima ya afya. Kama ilivyo Ile 50,400 kwa watoto basi angalieni watu wazima na familia wanaweza lipia kiasi gani kwa kila mwaka.
NHIF wakiweza kuweka njia rahisi na nafuu na kutengeneza mfumo ambao wananchi wengi watakua wanachangia itakua rahisi pia wananchi wachache wanaougua kutibiwa, kuliko sasa wanavyochangisha wananchi wachache na pesa nayo inakua chache kuwatibia wananchi wachache wanaougua

2.Kingine basi niwaombe mshirikiane na wizara ya elimu kuweka somo litakaloweza kubeba maadili na desturi za mtanzania na maisha yake. Vijana wetu siku hizi hawana jando na unyago, wazazi wote wawili wamekua watu wa majukumu mengi huku watoto wakiachwa wanajifunza toka kwenye t.v. na wasaidizi wa nyumbani. Ukitengenezwa mtaala mzuri wa kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne nina uhakika vijana wetu wanaweza kuwa taifa bora sana baadae. Tutaepuka hata watoto kuendelea kuharibiwa kwa kurubuniwa kwani wengi wanakua hawajui na wanafanyiwa mambo mabaya wakiwa wachanga sana hadi inapojulikana inakua basi tena

3.Wizara ya afya na elimu angalieni hizi boarding za watoto wadogo jamani na mkiweza mzifungie kabisa au pale penye ulazima kibali kitoke kwenu. Hainingii akilini mtoto wa miaka 2, 3, 4, 5, hadi 10 kuwa shule ya bweni. Malezi na matunzo ya awali toka kwa wazazi ni muhimu sana kwa mtoto. Wamama na wababa kwanini tunazaa halafu hatutaki kulea? Kweli baba na mama wanampeleka mtoto mdogo bweni, mtoto ambae hata kujifunika shuka usiku au kupiga mswaki hawezi!! Halafu wanakaa nyumbani, wanakula kwa amani kabisa na kulala?? Kuna visa vingi nimekutana navyo vya kuumiza sana toka kwa hawa watoto

Cc Wizara ya Afya Tanzania

Nimekusoma ndugu mtaalam na mchambuzi mbobevu wa mambo ya kiafya, Wizara wanatakiwa kuhakikisha kunakuwepo na uhakika wa vipimo mhimu katika hospital zao maana ni aibu kubwa unakuta kila kipimo mhimu kutopatikana kwa mda wote kwa sababu ya mashine kuwa mbovu ama kutokuwepo kabisa vipimo hitajika kwa hospital ya ngazi husika ama wafuatilie kwa ukaribu zaidi uendeshaji wa hospital zao ili kupunguza vikwazo kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma kwao.

Jamii kubwa inategemea sana hizi hospital kwa sababu ya kipato duni lakini hugeuka kuwa kero kwao kuliko suluhisho kwa shida zao hivo kutafuta njia mbadala ambazo huwa si rafiki kwa afya zao.

Nakazia tena inatia aibu sana kukosekana kwa basic laboratory investigations kwa hospital ngazi ya rufaa mkoa, wizara inafanya kazi kubwa na nzuri usiku na mchana kujaribu kupanua na kuongeza juhudi ya kutoa huduma bora kwa wananchi lakini iwapunguzie mzigo kwa kuongeza vipimo na wataalam wa kada husika ili kuleta ustawi bora wa afya
 
Nimekusoma ndugu mtaalam na mchambuzi mbobevu wa mambo ya kiafya, Wizara wanatakiwa kuhakikisha kunakuwepo na uhakika wa vipimo mhimu katika hospital zao maana ni aibu kubwa unakuta kila kipimo mhimu kutopatikana kwa mda wote kwa sababu ya mashine kuwa mbovu ama kutokuwepo kabisa vipimo hitajika kwa hospital ya ngazi husika ama wafuatilie kwa ukaribu zaidi uendeshaji wa hospital zao ili kupunguza vikwazo kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma kwao,. Jamii kubwa inategemea sana hizi hospital kwa sababu ya kipato duni lakini hugeuka kuwa kero kwao kuliko suluhisho kwa shida zao hivo kutafuta njia mbadala ambazo huwa si rafiki kwa afya zao...Nakazia tena inatia aibu sana kukosekana kwa basic laboratory investigations kwa hospital ngazi ya rufaa mkoa, wizara inafanya kazi kubwa na nzuri usiku na mchana kujaribu kupanua na kuongeza juhudi ya kutoa huduma bora kwa wananchi lakini iwapunguzie mzigo kwa kuongeza vipimo na wataalam wa kada husika ili kuleta ustawi bora wa afya

Jonno sijui uko mkoa gani lakini huku kwetu naona wanaendelea kuboresha siku baada ya siku.

Ili kuongeza ufanisi na kupunguza au kubalance idadi ya wagonjwa kadri ya uwezo wa hospital, hospital zetu kubwa za rufaa kanda zimeendelea kuwezeshwa kuwa vipimo ambavyo ni vya gharama kubwa na vichache, na wakati huohuo hospital za wilaya na mikoa zikiboreshwa katika kuwa na wataalam, majengo na vitendea kazi vingine.

Kwa mfano kanda ya kaskazini ukiwa unatibiwa mount meru hospital unaweza kutumwa kufanya vipimo kcmc na kurudisha majibu na ukapata matibabu kama ilivyo kwa hospitali za mkoa kama kibaha ambapo mgonjwa anaweza kupelekwa mloganzila au amana kwa uchunguzi zaidi au muhimbili.

Mimi sio mbobezi kwenye sekta ya afya ila tulikotoka palikua pagumu jamani enzi zile unafikishwa hospitali hujitambui unalazwa chini hazikua na tumaini, tulipo pana ahueni na tunapoenda pana mwanga zaidi
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz

Official Blog www.afyablog.moh.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfyaView attachment 1588107
Hivi Tanzania kuna Corona ?
 
Hivi mbona siku hizi NHIF wanaendelea kupunguza dawa, nimeandikiwa dawa ya duphaston mara kadhaa, lakini ukienda dirashani wanakwambia imeisha nenda kanunue.

Kuna siku nilienda hospitali moja ya private wakaniandikia kwenye fomu ya bima nikanunue pharmacy wao hawana, nilitembea pharmacy zote kubwa zinazojulikana nikiwaonyesha ile karatasi ya bima wakaniambia hawana hiyo dawa.

Basi nikamtuma mtu akaninunulie kwa cash kwenye phamarcy mojawapo nilizotembelea, Basi yule mtu alipewa hizo dawa na ziligharimu 75000/ kwa dose. Sasa hii inamaanisha nini jamani, nini maana ya kuwa na bima sasa. Wizara tunaomba mtusaidie kwa hilo.
 
Ajirini na waphamacia jmn maana wengi wanaishia kuuza dawa za kutoa mimba mtaani
 
Suala la Wazee bado ni changamoto. Lile dirisha la Wazee ndani hakuna Daktari. Sera ya Wazee ya mwaka 2003 hadi leo hamjaitungia Sheria, hivyo kusema Wazee watatibiwa bure si kweli.

Ni lini mtawakumbuka hawa Wazee ambao masuala yao yapo ndani ya Wizara hii?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz

Official Blog www.afyablog.moh.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfyaView attachment 1588107
Asante kwa kaz yenu nzuri. Swali langu ni kuwa, mgonjwa anapoambiwa alete damu(watu wa kuchangia damu) damu anayoongezewa mgonjwa inakuwa ni ile iliyoletwa na watu wa mgonjwa?

Nina mgonjwa katika hospital ya litembo iliyoko wilayan mbinga mkoa wa ruvuma, mgonjwa wangu amefanyiwa upasuaj, baada ya upasuaj wakasema mgonjwa inatakiwa kuongezewa damu. Ili damu iongezwe ni lazima tulete watu wa kutoa damu. Hili suala lipoje?
 
Back
Top Bottom