#COVID19 Wimbi jingine la Corona linapopita angani

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
28,181
36,164
Imekuwa kawaida kwa mawimbi ya hii ngwengwe kukatiza duniani mwishoni mwa mwaka kuelekea mwanzoni mwa miaka mipya.

Rejea historia, mengi yanajiongelea menyewe.

Tayari nchi kadhaa zikiwamo India, Japan na Marekani zimechukua tahadhali na wasafiri ndugu zetu damu damu kutokea pande za China.

Kwetu kumekuwa na ongezeko la matangazo tata radioni kuhusu kujikinga na Ebola. Kwamba:

"Nchi moja jirani yetu ina Ebola tuchukue tahadhali kwa kunawa maji tiririka na sabuni, tujiepushe na mikusanyiko, tuepuke sehemu wanazo shikashika watu wengi, nk."

Hizi ni tahadhali za Ebola?

Ama kweli akili ni nywele.
 
Papa Benedicto ambaye ana miaka 95, hali yake ya afya siyo nzuri. Tumuombee
 
You utter 🤡...🤣🤣. Soma bandiko lako tena

Bandiko langu ni hili ndugu:

--------
Kwetu kumekuwa na ongezeko la matangazo tata radioni kuhusu kujikinga na Ebola. Kwamba:

"Nchi moja jirani yetu ina Ebola tuchukue tahadhali kwa kunawa maji tiririka na sabuni, tujiepushe na mikusanyiko, tuepuke sehemu wanazo shikashika watu wengi, nk."

Hizi ni tahadhali za Ebola?

Ama kweli akili ni nywele.

---------

Hiiiiiiii bagosha!

Mtaelimika lini ndugu mjumbe?
 
Corona tulishakula pesa za msaada, tukaenda kujengea madarasa huku tozo tusijue siku hizi zinakwenda wapi kufanya nini, kilichobaki kwetu ni kuomba Mungu balaa lisitukute, tukiulizwa maswali ya ule msaada ya kwanza tuliupeleka wapi sijui tutawajibu nini wenye dunia.
 
Inasikitisha sana maana tumebakia sasa kuhanja hanja hatujui tuseme nnii au tuache nini. Wenyewe wanasema wako kazini kumbe macho kodo kwenye maslahi yao binafsi.
 
Back
Top Bottom