Wenzetu mnaosafiri nje ya Tanzania mmewahi kukutana na tangazo letu kama hili huko?

w0rM

Member
May 3, 2011
68
166
Habari WanaJF,

Leo nimepita pale maeneo ya St. Peters karibu na Mbuyuni Jijini Dar es Salaam nimekutana na bango hili kubwa sana likiwa na maandishi mamubwa “Visit South Africa” inaweza kuwa sio jambo baya ila najiuliza na sisi kwenye nchi za Wenzetu tunafanya kujitangaza hivi?

IMG_9749.jpeg


Nawaza katika nchi za wenzetu sisi tunaweza kuweka bango kubwa namna hii na kusema “Visit Tanzania” katika eneo linalopitiwa na watu kwa wingi kila mara.

Yawezekana likawa ni tangazo la ndege za South Africa ila hadi ujue hivyo ni mtihani kwani cha kwanza unaona ni maneno makubwa kabisa “Visit South Afica” ni kama tunawahamasisha Wageni na Watanzania waende South Africa.

Naweza kuwa nakosea. Ila je hii ni sawa? Na Tanzania inafanya hivi huko Ugenini?
 
Hilo ni tangazo la biashara jiji lako limeshaingiza pesa kazi iliyobaki ni namna ya kuzitumbua tu.

Huonagi epl matangazo ya visit rwanda visit azerbaijan
 
Nawaza katika nchi za wenzetu sisi tunaweza kuweka bango kubwa namna hii na kusema “Visit Tanzania” katika eneo linalopitiwa na watu kwa wingi kila mara.
Hapa ilikuwa ni Khartoum, Sudan.

Matokeo yake ni kwamba kuna kundi kubwa la madaktari wanafunzi wamekuja Tanzania kusoma programu za shahada za udaktari pale Muhimbili

1711554948004.png



1711555052700.png
 
Back
Top Bottom