Waziri Makamba, Ule mpango wa kuisuka UPYA Wizara ya Mambo ya nje uliishia wapi?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
16,375
24,736
Ulipoingia wizara ya nishati Kwa mara ya kwanza, ulikuwa na MIKAKATI mingi, customer care ikajitegemea, service za mitambo na njia za umeme, pesa zikalipwa na tatizo liko pale pale, software ya mabilioni ikawekwa, ununuzi wa nguzo za umeme za zege zinazovunjika zenyewe,, mitungi ya gas, bei za kuunganisha umeme zikapanda ,ukaagiza Crane la 26 tonnes, halijawahi kufika Hadi leo nk nk

Ameingia Doto Biteko, YEYE anahangaika na kuhakikisha umeme unapatikana, hatuoni mbwembwe.

Ulipohamia wizara ya mambo ya nje, ulimweleza Rais Samia kuwa unataka kuisuka UPYA wizara ya mambo ya nje iwe ya kisasa zaidi.

Tulitegemea tuone mauzo ya bidhaa nje ya Nchi yakiongezeka Ili mfuko wa dollar utune, fursa za kuwekeza nje ya Nchi ziongezeke ,Tulitegemea shilingi yetu iimarike, Badala yake inadorora Kila uchwao, nk nk.

Case ya mpaka na Nchi ya Malawi iliishia wapi?

Pia tungependa kujua, mwili wa kijana wetu mtanzania aliyeuwawa Israel, ulipatikana?

Tuambie, mpango wako wa kuisuka UPYA wizara ya mambo ya nje , uliishia wapi?
 
Tulitegemea Nchi yetu mauzo ya bidhaa nje ya Nchi yapae Ili shilingi yetu iimarike na hazina ya dollar itune,

Iweje shilingi yetu idorore?

Vipi kuhusu mpaka wetu na Malawi?
 
kiukweli huyo jamaa mi binafsi hajawahi kunishawishi.

si kama namchukia ila hana project sustainability. ila naona ana kismart flani cha kupendwa na watawala.
Ni upendeleo,

Hakuna Cha usmati Wala nini.
 
Tulitegemea Nchi yetu mauzo ya bidhaa nje ya Nchi yapae Ili shilingi yetu iimarike na hazina ya dollar itune,

Iweje shilingi yetu idorore?

Vipi kuhusu mpaka wetu na Malawi?
Ulipoingia wizara ya nishati Kwa mara ya kwanza, ulikuwa na MIKAKATI mingi, customer care ikajitegemea, service za mitambo na njia za umeme, pesa zikalipwa na tatizo liko pale pale, software ya mabilioni ikawekwa, ununuzi wa nguzo za umeme za zege zinazovunjika zenyewe,, mitungi ya gas, bei za kuunganisha umeme zikapanda nk nk

Ameingia Doto Biteko, YEYE anahangaika na kuhakikisha umeme unapatikana, hatuoni mbwembwe.

Ulipohamia wizara ya mambo ya nje, ulimweleza Rais Samia kuwa unataka kuisuka UPYA wizara ya mambo ya nje iwe ya kisasa zaidi.

Tulitegemea tuone mauzo ya bidhaa nje ya Nchi yakiongezeka Ili mfuko wa dollar utune, fursa za kuwekeza nje ya Nchi ziongezeke ,Tulitegemea shilingi yetu iimarike, Badala yake inadorora Kila uchwao, nk nk.

Case ya mpaka na Nchi ya Malawi iliishia wapi?

Pia tungependa kujua, mwili wa kijana wetu mtanzania aliyeuwawa Israel, ulipatikana?

Tuambie, mpango wako wa kuisuka UPYA wizara ya mambo ya nje , uliishia wapi?
wizara ya mambo ya njee inafanya vizuri mno, kwa haraka na kwa ufanisi zaidi kwasasa, ukilinganisha na wakati mwingine wowote huko nyuma 🐒

mahusianao ya Tz na nchi mbalimbali duniani mathalani katika nyanja za kirafiki, kibiashara, kielimu, michezo, afya, usafirishaji, technologia, utalii na uwekezaji yameimarika zaidi ukilinganisha na vipindi vilivyo pita 🐒

hata hivyo,
wizara chini ya very able minister J. Makamba inaendelea kuboresha mambo kadha wa kadhaa ya kisera, kisheria na kimkakati ili kuendana na dynamics za international relations, politics and diplomacy ya jinsi mashirikiano duniani yanavyo endeshwa 🐒

ni Muhimu kuwa na subra Lakini wastahimilivu, kwani mambo mazuri hayataki haraka 🐒

viva J.Makamba viva..
Eid Mubarak JF family 🌹
 
Miili ya Watanzania walioripotiwa kufa Israel ilipatikana?

Na tetesi za wanajeshi wetu 3 kufariki congo ni za Kweli?
 
Back
Top Bottom