Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
19,435
30,372
Salaam, Shalom!

Nimefuatilia Kwa ukaribu jinsi waziri Jerry Slaa anavyofanya katika utatuzi wa migogoro ya ardhi, japo Bado ni mapema sana kusema kuwa anafanya vizuri, lakini Kwa sasa itoshe kusema ana kitu kinachoonekana, na atafika mbali, tuendelee kumwombea.

Nimesikiliza Kwa Umakini jinsi alovyotatua case ya Tajiri aitwaye Mzee Mmassy aliyenunua nyumba Kwa marehemu aliyeko kaburini, yaani document zinaonyesha marehemu akiwa kaburini alisaini mauziano na kumuuzia nyumba tajiri Mmassy, na jinsi alivyotatua case Ile kwa uwazi Kwa kutumia nyaraka halali katika ofisi ya ardhi, na jinsi alivyoweza kuwarudishia nyumba watoto na mke wa marehemu nyumba Yao, kiukweli Mungu aendelee kumjalia uhai na AFYA na baraka kiongozi huyu.

Nilifanikiwa pia kufuatilia jinsi alivyosaidia kutatua mgogoro ulioletwa na Msama, Kwa kutomtendea HAKI yake mama yule aliyedai kiwanja chake, pia nimeona ufuatiliaji, uthubutu na uchapakazi wa Waziri huyu kijana Jerry Slaa.

Ni maombi yangu, akae chini na viongozi wenzie katika wizara yake na kuja na mpango MIKAKATI wa kutatua migogoro ya ardhi Nchi nzima bila kuwepo haja ya kusafiri huku na huko, uwepo mfumo mzuri na WA haraka zaidi kuwafikia wananchi na kutatua migogoro hiyo ya ardhi.

So far, KAZI imeonekana inafanyika,

Mungu Mbariki Waziri huyu Jerry Slaa,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Ameeen.

Source: Milard Ayo tv.

Karibuni🙏
 
Huyo hamna kitu, ana-deal na kiki ambazo akikutana na mbabe anakwama, yaani uje mtaani umtoe mtu kwenye nyumba, hiyo ni kazi yako kama waziri? Anatafuta yale yaliyomkuta Mwamwindi wa Iringa.

Wizara ina mambo makubwa ya kisera ya kufanya, hayafanyii kazi.

Kuna tatizo kubwa la utawala wq ardhi (land administration) hasa kwa kuwa asilimia kubwa ya nchi yetu haijapimwa. Sheria ya ardhi namba 4/1999 inajishughulisha na ardhi yenye hati, lakini wangapi mjini wqna hati? Wale wasio na hati wanakuwa regulated vipi? Wizara imetoa muongozo kwa uhamishaji wa miliki ambazo hazina hati?

Wizara ina mpango gani kuunga mifumo ya kibenki na usajili wa ndoa ili mali za dhamana wakopeshaji wajue hali ya mkopaji?

Kulikuwa na mradi wa hati za kidigitali, umekwama wapi?

Benki ya dunia walitoa bilioni 350 kufadhili mradi wa wizara ya ardhi ambao unajumuisha ujenzi wa majengo ya taasisi za ardhi kila mkoa, mbona bajeti inaisha, majengo hayapo? Na hata vifaa walivyosema watanunua kwa ajili ya kila mkoa ili kupima ardhi havipo? Hizo hela zimeenda wapi?

Mamlaka zinapoingiza vijiji mjini, wizara imetoa muongozo kuhusu ardhi iliyokuwa ya vijiji? Kuna namna au mfumo wa vijiji kukabidhi ardhi kwa Halmashauri? Au ndio inaachwa kwa viongozi wa mitaa mipya wajiuzie wanavyotaka?

Hatumuoni katika migogoro ya hifadhi za taifa na wananchi, anazurura mijini tu. Kapima vijiji vingapi mwaka huu? Amegawa hati za kimila ngapi?

He is just a petty politician ambaye alitakiwa ajenge josho ili kuosha wanyama kwq maelfu, yeye kaamua kuchambua manyoya ya mnyama mmoja mmoja ili awe anatoa kupe
 
Huyo hamna kitu, ana-deal na kiki ambazo akikutana na mbabe anakwama, yaani uje mtaani umtoe mtu kwenye nyumba, hiyo ni kazi yako kama waziri? Anatafuta yale yaliyomkuta Mwamwindi wa Iringa.

Wizara ina mambo makubwa ya kisera ya kufanya, hayafanyii kazi.

Kuna tatizo kubwa la utawala wq ardhi (land administration) hasa kwa kuwa asilimia kubwa ya nchi yetu haijapimwa. Sheria ya ardhi namba 4/1999 inajishughulisha na ardhi yenye hati, lakini wangapi mjini wqna hati? Wale wasio na hati wanakuwa regulated vipi? Wizara imetoa muongozo kwa uhamishaji wa miliki ambazo hazina hati?

Wizara ina mpango gani kuunga mifumo ya kibenki na usajili wa ndoa ili mali za dhamana wakopeshaji wajue hali ya mkopaji?

Kulikuwa na mradi wa hati za kidigitali, umekwama wapi?

Benki ya dunia walitoa bilioni 350 kufadhili mradi wa wizara ya ardhi ambao unajumuisha ujenzi wa majengo ya taasisi za ardhi kila mkoa, mbona bajeti inaisha, majengo hayapo? Na hata vifaa walivyosema watanunua kwa ajili ya kila mkoa ili kupima ardhi havipo? Hizo hela zimeenda wapi?

Hatumuoni katika migogoro ya hifadhi za taifa na wananchi, anazurura mijini tu. Kapima vijiji vingapi mwaka huu? Amegawa hati za kimila ngapi?

He is just a petty politician ambaye alitakiwa ajenge josho ili kuosha wanyama kwq maelfu, yeye kaamua kuchambua manyoya ya mnyama mmoja mmoja ili awe anatoa kupe
Ana KAZI kubwa Bado mbele yake,

Lakini Hadi sasa,

Kuna kitu kinaonekana anafanya, mfumo wa kupata HAKI katika ardhi ni corrupt sana,

Uthubutu,msimamo, na u hapakazi wake upongezwe,

Kiongozi huyu, apewe support na ushauri,

Atalisaidia Taifa letu kupiga hatua.

Abarikiwe.
 
Kiongozi anajenga mifumo, hakuna mfumo aliojenga mpaka sasa, angekuwa na mfumo, asingekuwa na haja ya kutembea mpaka vyumbani mwa watu.

and land justice, kama ilivyo haki yoyote ile, huwezi kuifanya kwa mfumo wa mob justice, unakusanya vijitu mtaani, unasikiliza unaamua, hakuna due process halali ya kisheria ambayo itafanya haki ionekane inatendeka. Kuna mahala atakutana na jambo, yeye binafsi atadhalilika, na serikali itadhalilika.
 
If that's the case,

Kwanini chiembe hataki kusikia kuhusu Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi?
 
Huyo hamna kitu, ana-deal na kiki ambazo akikutana na mbabe anakwama, yaani uje mtaani umtoe mtu kwenye nyumba, hiyo
Yaani ni hopeless kabisa.katika viongozi wa hovyo tulio nao huyu jamaa ni namba moja.

Hajiamini kabisa.anatumia jeshi la polisi kutisha watu.

Sijui kwa nini raisi anaendelea na huyu jamaa.

Kamuabisha shehe kariakoo. Hata sheria za wakfu hazifahamu.

Tanganyika law society, tume ya haki za binadamu, mwanasheria mkuu pamoja na mahakama wanatakiwa watoe tamko kukemea huu ujinga
 
Matatizo mengi ya nchi hii ni ya kimfumo (kikatiba, kisheria, kiutawala na kisera), ili nchi iweze kusonga mbele dawa ni kurudi kwnye drawing board (Katiba isukwe upya).

hizi ngonjera za kuinua watu mnatutangazia kuwa ni manabii na mitume wa zama hizi wakati ubovu upo kwenye mfumo ikome.
Mnakumbatia matatizo halafu mnatutengenezea watu wa kuigiza kuyatatua
 
Mayayizo mengi ya nchi hii ni ya kimfumo (kikatiba, kisheria, kiutawala na kisera.
Ni Kweli kabisa,

Hizo Sheria, Katiba, sera, zinahitaji viongozi wenye uthubutu,uchapakazi, misimamo isoyumba Ili mifumo ufanye KAZI,

Tupambanie KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote,

Pia tuwatie moyo na kuwaombea viongozi wa caribre ya Jerry Slaa.

Ubarikiwe.
 
Sina shida ya yeye kama anachapa kazi, ila hakuna haja ya kusaka "cheap popularity" mara afanye kazi mbele ya kamera, kazi zake njema zitajitangaza haina haja kutangaza tangaza
Wananchi tuna HAKI ya kujua KAZI wanazofanya viongozi tuliowaajiri.

Vyombo vya habari kusambaza habari ni muhimu kabisa,

Wananchi tuna HAKI ya Kupata habari.
 
Watanzania ambao ni miongoni mwa waafrika wengi wajinga waliozaliwa katika bara la wajinga hawajui wanataka nini.

Nchi hii inasheria, taratibu za ununuzi na umiliki wa ardhi ila taratibu hizo hazifuatwi na watumishi wa wizara husika na baadhi ya wanachi pia hawafuati hizo taratibu tena makusudi.

Sasa mnataka waziri akae ofisini atengeneze mifumo ipi tofauti na hii iliyopo? Tatizo sio mifumo ni watumishi wasio na weredi sasa hawa unadeal nao vipi bila kuwafikia hukohuko waliko na kuwanonesha kwa vitendo wajibu wao ni upi, maana wakifukuzwa kazi bado mtakuja hapa kulalamika wameonewa.
 
Back
Top Bottom