Waziri Bashe anajua sana kucheza na akili za wananchi wa hili Taifa

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,732
6,545
Bashe namkubali kwenye jambo moja tu, anajua mno kucheza na akili za wajinga na anajua fika nchi ina wajinga wengi ambao kureason hawawezi kitu na hapo ndio anapo pitia. Zile project zake zenyewe ni full janja janja tupu.

Bashe anakuambia nchi ina chakula kingi sana hasa hio michele imejaa full kila kona. Wajinga tunakubaliana naye ila hatuhoji Watanzania wangapi wanashindwa kumudu hata milo miwili? Tunakubaliana naye kwa sababu sisi tunamuda hio milo mitatu? Vipi wenzetu ambao wako kwenye nchi huru na hawamudu hata milo miwili na wazir anatangaza chakula ni kingi ilihali watu wanashinda njaa?

Sasa wajinga hawaulizi ni kivipi sasa Serikali isilishe mashule? Nani asiejua ni wazazi wanachangishwa kulisha watoto mashuleni jukumu ambalo ni la Serikali? Serikali ilisha wahi lisha hata watoto wa chekechea hata shule moja tu ya mfano?

Watalawa wako busy kuagiza magari ya anasa ya Billion 500 kila mwaka ila hawawezu lisha watoto.

Sehemu nyingi za nchi zimejaa watoto wenye utapia mloa, kama Chakula kipo kwa nini tusiwalishe?

Wajinga pia wanashindwa kuhoji msaaada wa chakula ni aibu haijalishi mnapewa cash au Chakula. Msaada wa Chakula ni aibu na ni indicator za umasikini tu. Ni sawa na ushindwe kulisha familia yako aje njemba kusaidia kutoa chakula uanze kumkataza kwamba asilete msaada wa chakula nyumbani kwako bali alete pesa wewe ununue mwenyewe.

Mwisho, kama ni misaada ya aibu tukitakate yote, Kujengewe vyoo ni aibu kubwa pia, misaada ya neti mbona hatuikatai? Misaada ya net si inatolewa na hao hao USAID?

Tuache ujinga wa ndege Chichidodo.
 
Msomali ni mwizi, sema Bashe, Aweso, Ummy, Nape, Kijaju, Mchengerwa yale makelele na kumulikwa na camera kila wakati yanamfanya maza aone ni wachapa kazi haswa
 
Ni kweli km wanakataa chakula kwa nn hela wanachukua ???.Yaan ubaambiwa mm nakupa mchele ulishe watoto wako unaanza mbwembwe ila ingekua ni hela wangekua wameandaaa mapokezi ya maana.Ujinga tupu.
 
Upumbavu ni mzigo,cha kushangaza wanao piga kelele wakiambiwa wachangia chakula Cha watoto ili wapate kula mashuleni Wanaanza kulalamika.

Binafsi naunga mkono msaada wa chakula kwa watoto.Ni mpumbavu tu ndo atabeza huo msaada.
 
Ni kweli km wanakataa chakula kwa nn hela wanachukua ???.Yaan ubaambiwa mm nakupa mchele ulishe watoto wako unaanza mbwembwe ila ingekua ni hela wangekua wameandaaa mapokezi ya maana.Ujinga tupu.
Na ungekuta wangepewa hizo pesa,wangeangiza Mchele toka China.Taifa hili lina ujinga mwingi sana.
 
Msomali ni mwizi, sema Bashe, Aweso, Ummy, Nape, Kijaju, Mchengerwa yale makelele na kumulikwa na camera kila wakati yanamfanya maza aone ni wachapa kazi haswa
Ndio michezo anayoipenda Samia hujaona juzi wakat anaapisha viongozi wapya. anawaambia Kuna baadhi yao anawaona mitandaoni wakiwatumikia wananchi kwahiyo kuweni kama wao bila kujua kwamba hao anawaona mtandaoni wanaenda site na makamera man wao kwenye kuandaa hayo maigizo.
 
Amefanikiwa kucheza na akili za wajinga, amefaulu. Anafahamu akili za watanzania zipo based on negativity, akapeleka mpira huko huko!, dadek!
 
WE ndio una akili? Umeifanyia nini nchi hii
Kwani huyo kilaza mwenzio Bashe kalifanyia nini taifa?

Si huyohuyo alichukua maDJ, wacheza dansi, bodaboda na cameramen eti kuwafundisha kilimo kwa miezi kadhaa kwenye BBT. Wakati Wizara yake ina vyuo chungu nzima vya kilimo vinavyotoa wahitimu waliosoma miaka na waliokuwa na nia kabisa ya kilimo na wamefaulu.

Wameishia wapi?
 
Ndio michezo anayoipenda Samia hujaona juzi wakat anaapisha viongozi wapya. anawaambia Kuna baadhi yao anawaona mitandaoni wakiwatumikia wananchi kwahiyo kuweni kama wao bila kujua kwamba hao anawaona mtandaoni wanaenda site na makamera man wao kwenye kuandaa hayo maigizo.
Maza ndiyo anapenda hivyo
 
Bora ujinga wa watanzania kuliko mtu anaefumbata Mapato ya Udhalimu akidhani amepata kumbe anagundua kafumbata hewa. Na muda mrefu umepotea alafu hawezi ku rudi nyuma akarekebisha.
 
Back
Top Bottom