Watu wanaodhaniwa kuwa Polisi wamkamata Sheikh Abdulrazack Mohamed na kumpeleka kusikojulikana

Zakamwamoba

Senior Member
Jul 28, 2016
177
609
Taarifa kutoka huko Tunduru mkoani Ruvuma zinadai kwamba Sheikhe afahamikae kwa jina la Abdulrazack Mohamed alikamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa polisi (kutokana na mavazi yao) mnamo tarehe 7 mwezi March 2024 na kupelekwa kusikojulikana.

Ndugu walivofanya ufuatiliaji kwenye vituo vyote vya polisi vya Mkoa wa Ruvuma hawakumpata jamaa yao huku polisi wakisema hawajamkatama hali ya kuwa mtu huyo alikamatwa majira ya mchana Tunduru mjini na watu hao waliovalia sare zinazoendana na Jeshi la Polisi.

Ndugu walipojaribu kutoa taarifa polisi ya ndugu yao kupotea inasemekana polisi waliikataa taarifa hiyo na kuwataka waondoke wakamtafute ndugu yao.

Mpaka leo hii tarehe 06 April 2024 bwana Abdulrazack hajulikani alipo na haijulikani amekamatwa kwa sababu gani.

RPC wa Ruvuma toa neno kuhusu hili, kama waliomkamata ni polisi basi apelekwe mahakamani, kama sio polisi ifahamike na juhudi za kumtafuta zifanyike.

==

Pia soma
:
Polisi yafafanua madai ya kuwa Sheikh Abdulrazack Mohamed ambaye hajulikani alipo kwamba alikamatwa na Polisi
 
Au ni taarifa za waliofinywa huko urusi walitaja mtandao mzima? Holdon wakati anakamatwa tayari wale magaidi walioshambulia urusi walikuwa wamesha fanya ugaidi wao?
 
Taarifa kutoka huko Tunduru mkoani Ruvuma zinadai kwamba Sheikhe afahamikae kwa jina la Abdulrazack Mohamed alikamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa polisi (kutokana na mavazi yao) mnamo tarehe 7 mwezi March 2024 na kupelekwa kusikojulikana.

Ndugu walivofanya ufuatiliaji kwenye vituo vyote vya polisi vya Mkoa wa Ruvuma hawakumpata jamaa yao huku polisi wakisema hawajamkatama hali ya kuwa mtu huyo alikamatwa majira ya mchana Tunduru mjini na watu hao waliovalia sare zinazoendana na Jeshi la Polisi.

Ndugu walipojaribu kutoa taarifa polisi ya ndugu yao kupotea inasemekana polisi waliikataa taarifa hiyo na kuwataka waondoke wakamtafute ndugu yao.

Mpaka leo hii tarehe 06 April 2024 bwana Abdulrazack hajulikani alipo na haijulikani amekamatwa kwa sababu gani.

RPC wa Ruvuma toa neno kuhusu hili, kama waliomkamata ni polisi basi apelekwe mahakamani, kama sio polisi ifahamike na juhudi za kumtafuta zifanyike.

==

Pia soma: Polisi yafafanua madai ya kuwa Sheikh Abdulrazack Mohamed ambaye hajulikani alipo kwamba alikamatwa na Polisi
Hatutetei wezi
 
Back
Top Bottom