Robot la Matope
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 7,174
- 14,008
Habari wapendwa wana Jf wenzangu.
Awali ya yote nipende kusema, Watanzania sio waaminifu (na mimi nikiwemo). Hili tatizo sijui limesababishwa na nini lakini imani yangu inanituma kuamini ya kuwa aina ya uongozi tulio nao. Mtoto hawezi kulia kwenye familia ya wezi na asiwe mwizi. Ndio maana asilimia kubwa ya watoto wanafanya kazi za baba zao (Ref : TRA, JWTZ, PT, CRDB etc).
Nikirudi kwenye mada, Dar es Salaam ni kitovu cha biashara sio kwa watu tu wa mikoani bali hata nchi jirani zinazotuzunguka. Kutoka na maendeleo ya sayansi na teknologia kwa sasa, hakuna umuhimu wa mteja kwenda sokoni. Mfano kutoka huku kwetu Kashenye mpaka ufike Kariakoo nauli sio chini ya 200,000!! Lakini ukiagiza mtandaoni unaweza kusave zaidi ya 90%!
Sasa hapo kwenye 90% ndo watu tunapobamizwa baaa!! Mtu anawekeza bidhaa yake kwenye mtandao, mteja anaipenda anatuma pesa na ya kutolea muuzaji na jambazi anapotea na kila kitu.
Bora huyo, kuna wale wauzaji wa simu za wizi (hapa naomba niseme ukweli, HAWA WATU WANASHIRIKIANA NA BAADHI YA POLISI). Mtanzania kwa moyo mkujufu unanunua simu kwa muuzaji, ikifika kwako siku mbili nyingi, polisi hawa hapa wametoka Dar-es-Salaam kwa usafiri binafsi, wanakutafuta wewe mwizi wa simu. Simu uliyonunua mtandaoni ni ya wizi, wizi wenyewe umefanyika Dar ndani ndani huko na aliyeibiwa simu kauwawa na mkewe kabakwa!!! Walikua na mtoto na hawajui yuko wapi!! Yarabi tobaaa!
Mimi huyu mtu wa Kyamulaile niliesomea Kyampisi middle school na kumalizia elimu yangu kwenye shamba la mzee la kahawa sijiwahi kufika hata Nyakanazi Dar-es-Salaam nimefikaje? Nimeuaje? Nimebakaje? Na huyo mtoto nimempeleka wapi? Wakati ukiendelea kujiuliza hayo maswali, kuna kofi moja matata unalipokea (wao wanaita banzi au Restart). Akili inapokaribia kukukaa sawa unapigwa pingu na kwenye gari yao unapandishwa na mwendo unaanza.
Ukiwa njiani ndo vitisho vinazidi na wanaanza kufanya bargaining.. una shilingi ngapi? Mafuta yao unayalioaje? Huyu mtoto aliyepotea wanaweza kumpata kama utakaa sawa, mama aliyebakwa watampoza, marehemu wakamjengee kaburi nk.... Mkamatwa na ngozi ndo mwizi wa ng'ombe... Dah, Mpaka hapo ushafirisika.
STORY OF CHANGE
Serikali kupitia mamlaka zake, wasajiri watu (verifier) ambao watakua na permanent address. Watu hawa ndo wawe wanatoa certificate za kuuza bidhaa mtandaoni ili ikitokea mtu katapeliwa waanza na huyu verifier!
Twende sawa, huyu verifier ndo atakua muunganishi kati ya muuzaji na mnunuaji. Pesa atapokea yeye na mzigo atatuma yeye kwa makubaliano let say ya kulipwa hata 3% ya pesa za manunuzi.