Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,734
- 2,265
Kuna watu, wengine wanasiasa wakubwa tu, wamekuwa wakiimba wimbo wakutufarakanisha Mbeya, sisi kwa sisi na vilevile kuwa wana Mbeya hawampendi Rais Magufuli.
Wameumbuka vibaya.
Ujio wa Rais Magufuli Mbeya ulikuwa kwa mafanikio makubwa.
Kuna hata waliodiriki kusema wanasiasa wa mkoani Mbeya watasusa kufika mikutano yake.
Tumeona natumefarijika viongozi wa Mbeya mzee Mwandosya , Sugu, Mary Mwanjelwa , Tulia Ackson wote wameshirikiana vema kufanya ujio wa Rais kuwa wa kupendeza.
Kwa hiyo kuna watu sasa wanatafuna kucha zao.