Wapi nitaupata wimbo huu wa zamani (zilipendwa)?

Hard drive

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
265
62
Habari wakuu!

Natanguliza shukrani wa wadau na wapenzi wa nyimbo za zamani (zilipendwa),naombeni msaada wa kujua jina la wimbo na wa/mwimbaji kwa kuwa msanii aliyeimba simjui wala jina halisi la wimbo silijui ,ila nakumbuka baadhi ya maneno yaliyomo kama;

“kule bagamoyo kule, kule bagamoyo kuleeeee, kuna mandege meupe”

Kwa yeyote anayeujua huu wimbo msaada tafadhali ili niweze kuupakua na kuendelea kuburudika na wimbo huu.

Ahsanteni!
 
Kweli umri wa "zilipendwa" unatofautiana kati ya mtu na mtu. Huu wimbo aliimba Muumin Mwinjuma miaka ya mwanzoni ya 2000 akiwa na Mchinga Sound (kama sikosei)

Kule Bagamoyo kulee
Kule Bagamoyo kulee
Sehemu za Zinga na Pandee
Kuna madege meupee

😀😀😀😀
 
Yuko sawa tu, ndio umri wake. Tunao vijana wamezaliwa 2000 ndo wanaingia vyuoni mwaka wa kwanza sasa, wapo humu na ni wajuaji haswaaa, sasa kama nyimbo ilitoka wakati yeye anazaliwa aiitaje?

Zilipendwa haziwezi kubaki kuwa zile za wazee walizosikiliza 1960's - 1990 tu, maana kuanzia miaka ya 1990 ndipo wakina Salehe Jabir walipoanza hizi zetu sie vijana wa kileo
 
Huu wimbo ni wa Muumini Mwinyijuma. Umepigwa sana Clouds radio enzi za kipindi kinaitwa Bambataa hata hivyo nilitarajia nikute wimbo ambao Marijani au Niko Zengekala wamehusika. Huu siyo wa zamani sana.
 
Yuko sawa tu, ndio umri wake. Tunao vijana wamezaliwa 2000 ndo wanaingia vyuoni mwaka wa kwanza sasa, wapo humu na ni wajuaji haswaaa, sasa kama nyimbo ilitoka wakati yeye anazaliwa aiitaje?

Zilipendwa haziwezi kubaki kuwa zile za wazee walizosikiliza 1960's - 1990 tu, maana kuanzia miaka ya 1990 ndipo wakina Salehe Jabir walipoanza hizi zetu sie vijana wa kileo
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom