Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,369
- 12,970
Kwanza kabisa Rais mwenyewe kwa matendo na maneno ameonyesha kuwa hataki habari za uchawa. Lakini machawa hawaishi kumsifu kwa hata vitu vya kuchekesha kabisa. Leo hii jambo la kumsifia Rais limekuwa kama dhihaka. Dhihaka kama hiyo iliandikwa karibu miaka 80 iliyopita.
- Rais Samia awakana machawa, asema yeye hana makundi
Mwaka 1945 mwandishi George Orwell aliandika kitabu shamba la wanyama. Humu ndani ya hadithi kulikuwa na kiongozi mmoja dikteta hasa. Sasa alikuwa na machawa wake waliomsifia kwa kila kitu. Baadhi ya sifa alizopewa ni kama zifuatazo.
Ikawa ni kawaida kumsifia Napolioni kwa kila mafanikio na hali nzuri iliyowapata wanyama. Ungeweza kumsikia kuku mmoja akiwaambia wenzake, “Chini ya uongozi wa kiongozi wetu ndugu Napolioni, nimeweza kutaga mayai matano ndani ya siku sita.” Au ng’ombe wawili wakiwa wanakunywa maji kwenye lambo wanaweza kusema kwa furaha, “Shukrani ziende kwa uongozi wa ndugu Napolioni, maji haya yana ladha nzuri ajabu.”