Wanakuja dhalili wanaondoka wakiwa Wafalme

mrdocumentor

Member
Nov 27, 2021
43
55
Katika maisha ya Mtanzania ambae anapenda mpira na anaufuatilia walau kwa asilimia 40 lazima atakuwa na upande kati ya Simba au Yanga, hizi ni timu zetu kubwa lakini hizi ni kama utamaduni kwetu pia, hicho ndicho hufanya watanzania wengi kuwa ni washabiki wa timu hizo.

Jambo usilolifahamu kuhusu timu hizi mbili, zote zina tabia inayofanana, Simba na Yanga kwa umoja wake zote zinafanya kazi ya kuwafichua waliofichikana na kuwapandisha walioshuka kisha kuwalisha wanaostahili kula vizuri tu.

RELAX!!!
Kwa miaka ya hivi karibuni timu hizi zimekuwa zikichukua wachezaji wengi wa kigeni ambao wanaamini kuwa wataleta chachu ya mafanikio ya Club zao lakini pia kuwezesha wachezaji wa ndani wajifunze kutoka kwa wenzao ambao wanatoka nje.

Kwa uwezo wa timu zetu kwa sasa kwenye soko la usajili wana uwezo mkubwa wa kupata wachezaji wenye kiwango cha kati ambao kulingana na ligi yetu wanaweza kupambana na kupata fursa ya kuzisaidia timu zao zipate ushindi ndani na nje pia.

Wachezaji hao wa kiwango cha kati kuna wakati wanakua kwa kasi mno na kuonekana kuwa wana kiwango cha juu kuliko kawaida, hapo ndipo timu zenye uwezo mkubwa wa pesa na zenye ushawishi zaidi kutuzidi huwa zinakuja mezani ili kuhitaji saini ya mchezaji husika.

Mchezaji akishaondoka, timu zetu hizo zinarudi sokoni tena kumtafuta mwenye kiwango cha kati tena ili aje kuwasaidia, wakati mwingine akue mikononi mwetu ajitengenezee soko mwenyewe alafu aondoke zake akatafute changamoto nyingine na hiyo changamoto nyingine ikiwa ya moto kweli tunamsujudia anarudi tena hapa "Shamba la bibi", kifupi tunashindwa kukaa na wachezaji wazuri.

Sio vibaya kuuza wachezaji kwa sababu ni biashara kama zilivyo biashara nyingine, Lakini tunatakiwa kuimarisha vyanzo vyetu vya mapato ili tusiache mchezaji tukiwa tuna muhitaji sana au kama tunawauza basi tuwauze kwa pesa ndefu ambayo itasaidia timu.

Tusipoimarisha vyanzo vya mapato vya timu, timu zetu zitaendelea kuwa academy za kukuza vipaji visivyo vya kizalendo.
 
Back
Top Bottom