Walemavu wa macho 10 waliofanya mambo makubwa

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,539
Waswahili husema ulemavu mbaya ni wa akili wakiwa na maana kwamba ukiwa chizi/taahira hutoweza kufanya jambo lolote la maana maisjani japo viungo vyako vitakuwa vinafanya kazi
Sasa tuwaangalie walemavu wa macho walioweza kufanya mambo makubwa na kudhihirisha kwamba kuwa mlemavu sio mwisho wa maisha

............................................. . . ...... .


10 Doc Watson
1ea70eb118099588937d6e1bb6472d51.jpg

6b435a7188913e568ecc92f2ef0224cd.jpg


1f43492aff99cadf0357d460d8512d4d.jpg

Alizaliwa mwaka 1923 na kufariki dunia 2012 akiwa na umri wa miaka 89
Huyu alikuwa ni msanii wa muziki licha ya kuwa kipofu(sijui hili neno ni tusi)
Alikuwa ni mwimbaji na mpiga gitaa mahiri
Wazazi wake wamechangia mafanikio yake maana hawakumtenga wala kumficha
Kaimba ngoma kibao kama vile Sitting On Top Of The World

 
Last edited:
9/Diane Schuur

29f084d5519b68813cfdff19c1485466.jpg

21b9790ea7b6c8401d524598cb208c51.jpg

9d4fa9fa7e0a67528c449bba492ee1b2.jpg

Alizaliwa Disemba 10 mnamo mwaka 1953
Huyu ni kipofu mwingine mjanjamjanja ambaye anakimbiza tu kwenye muziki wa Jazz yaani huyu kwa wasioona ndiye Madonna wao
Siyo tu anafanya muziki kutafuta sifa bali anaingiza mpunga wa maana kupitia sanaa
Huyu amenyanyapaliwa sehemu kibao ila akakomaa nao na kuwadhihirishia kwamba kukosa macho/kuona sio kukosa akili na kipaji
Kapiga ngoma kibao kama vile
Louisiana Sunday Afternoon,Deedle's Blues,Easy To Love,TheMan Ilove
Ana album 23 na zinskimbiza tu sokoni na kuongiza mpunga The Man I Love
 
8/David Paterson
7e45a2092e4c17a2dd149febefcc9b53.jpg
2420594bc117726b51df5fc0a777f271.jpg
534e3ac1cad099c597c8dc7b4a3d4d6a.jpg

Alizaliwa Mei 20 mwaka 1954
Mlemavu huyu wa macho aluamua kujikita kwenye siasa na kufanikiwa kuwa Gavana huko Marekani
Alikuwa Gavana wa 55 wa New York yaani aliliongoza moja kati ya jiji la maana kabisa huko Marekani....ni bora huyu mlemavu mwenye busara kuliko kuongozwa na Bashite !!
Aliliongoza jiji la New York kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010
Ni msomi kutoka Colombia University na hakuridhika hivyo akaenda kumalizia na shule ya sheria (uwakili) huko Hofstra Law School :
Huyu ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika kama Barack Obama na mpambanaji haswa na alisifika kwa hotuba zenye kuvutia
 
7/Helen Keller
a0a42f251cfeaa2fa56b7d4d0388ef66.jpg
3f024c3dcf129a3548a1d9009a87f3c6.jpg

Ni mzaliwa wa Alabama huko nchini Marekani
Alizaliwa mwaka 1880 na kufariki dunia mwaka 1968 akiwa na umri wa miaka 88
Huyu sio tu alikuwa haoni bali pia hasikii kitaalamu anaitwa Kiziwi asiyeona ukienda pale Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko utawakuta watoto wa aina hiyo hawa kuwafundisha ili wakuelewe ni jambo gumu linalohitaji moyo na kujitolea
Sasa huyu pamoja na hali yake alikomaa na shule na kufanikiwa kuwa Kiziwi asiyeoona wa kwanza kupata Shahada ya Sanaa yaani alikomaa na nukta nundu tena bila kumsikia mtu hadi chuo kikuu !!!
Huyu alikuwa ni Mhadhiri na Mtunzi
12d211f08e6ca70b1bb1a6a80575d6b8.jpg
8d5165b903205c9ab20670fc8355f3e0.jpg
054d9be0f15e834cf3957b455d676501.jpg
c3f72047efe8791c19a1717a68de345b.jpg

Kaandika vitabu kibao vilivyotikisa na kuishangaza dunia
Huyu ndiye kiziwi asiyeona maarufu zaidi duniani
 
6/Jose Feliciano
7b4aab9675e34f84aa459269dccdd255.jpg
7bcfcf9b8dabeb19b978464369574b7d.jpg
666ba94c0f40e5dad4154346b54ed0db.jpg

Alizaliwa Septemba 10 mwaka 1945
Huyu ni msanii kutoka Puerto Rico
Ni mwimbaji na mtunzi/mwandika nyimbo mwenyenye mafanikio makubwa nchini humo na duniani kwa ujumla
Wimbo wake wa Feliz Navidad unakimbiza duniani kwa ujumla kila unapofika msimu wa sikukuu ya Christmass
Jamaa anaimba kwa kutumia lugha za Kilatini na Kiingereza hivyo kufanikiwa kuliteka soko la muziki kila pembe ya dunia
Nyimbo zake nyingine ni kama vile :
Su Hija Me Gusta
Light My Fire
 
5/Jeff Healey
4d282b69e103f7598444683370fa981b.jpg
91b6a8a1c235ace3766e4232cbaec110.jpg
4d1ef24cd96d57553a725b26ed1d987c.jpg

Alizaliwa mwaka 1966 na kufariki dunia mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 41
Huyu alikuwa ni raia wa Canada mwenye vipaji kibao licha ya ulemavu wake wa kutoona
Alikuwa ni Mwimbaji,mpiga gitaa na mcheza filamu mahiri huko Canada na Hollywood nchini Marekani
8b10f12b597ea9390804a9ef5f9adaad.jpg
Huyu alipambana na hali yake licha ya kubezwa hadi kufanikiwa kuwa mtu mashuhuri kwenye filamu na muziki kiasi cha kupiga pesa ya maana kwa kuutumia ulemavu wake bila kupiga watu assist kama za bwana mmoja wa Jf na akafanikiwa kumiliki bendi
Kibao cha Angel Eyes, ndio kilichotamba zaidi kiasi cha kukamata # 5 Billboard Hot 100 na kuuteka ulimwengu
Kaimba pia :
Think I Love You Too Muc
Stop Breaking Down
Hoochie Coochie Man
Like A Hurricane..
 
Daaah mi mzima kabisa hata kutunga ngonjera tu siwezi.
Watu na talent zao daaah.
Ulemavu mbaya ni wa akili tu mkuu
Kuna watu walemavu ila wana vipaji
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Ulemavu mbaya ni wa akili tu mkuu
Kuna watu walemavu ila wana vipaji
Hahahaha
Hapo sawa kabisa.
Akili ikilemaa haikosagi kuitwa chizi,mara hana akili huyo,mwendawazimu,saa mbovu.nk
Daaah noma sana.
 
4/Casey Harris
cb3c64d7b8d9b7c69dca1c8ddc7ded44.jpg
2915cf8955aad06f4a4ae5fd76d2cf13.jpg
0a86ed0b19d2405cbb6be5d9552b5612.jpg
Huyu mlemavu wa macho bishoo alizaliwa Januari mwaka 1987
Huyu naye alipambana na hali yake kuanzia utotoni hadi ujanani na kufanikiwa kutimiza ndoto zake za kimaisha
Ni memba wa kundi la X--Ambassadors Hawa jamaa wanatamba sana na nyimbo zao kibao tu
 
3/Ray Charles
542f261d5ed9d312bc35a48727533225.jpg
3bf8f03a22f027415e73ac236d1fb697.jpg
419352c01926d9d4bb9b14a10596b188.jpg

Alizaliwa mwaka 1930 na kufariki dunia mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 73
Huyu alikuwa ni mwanamuziki mahiri wa nyimbo za injili,Jazz na Pop alikuwa pia na uwezo mkubwa wa kuandika nyimbo
Jamaa licha ya kuwa kipofu ila alikuwa ni bishoo wa kutupwa ujanani kuanzia nywele ,mapigo ya pamba hadi miwani nyeusi alichagua tu za kibishoo
Pia alikuwa ni mpenda totoz sliyepitiliza
Kaimba nyimbo kibao kama vile;
Seven Spanish Angels
Georgia On My Mind
I Can't Stop Loving You
Hit The Road ,Jack

Seven Spanish Angels
 
2/Andrea Bocelli
0246ce8ce03bf04dddd8159635539ef0.jpg
77082a3827a84149d740a947177f43d3.jpg
9cedfa196c31b9aa8d005c8992e00bd9.jpg

Alizaliwa Septemba 22 mwaka 1958
Huyu ni mwanamuziki mashuhuri wa Kiitaliano
Sio tu mashuhuri jamaa ni mjanjamjanja anacheza hadi filamu licha ya kwamba haoni
ee614118eeb8a7c1808d95ea563309e7.jpg
kawahi kutajwa kwenye orodha ya 50 Most Beautiful People na jarida moja mashuhuri duniani
Muziki wake pia ameimba na mastaa kibao akiwemo Celine Dion
Pia kaimba:
A Mio Padre
Because We Believe
 
1/Stevie Wonder
e8728c7f999a44057b3372a1e90b8f11.jpg
6c623d9229eba6f4c9152ef6cf771ac5.jpg
83339fca46d02bb88e1107b50377a96c.jpg

Alizaliwa Mei 13 1950
Huyu wala sihitaji maneno mengi kumwelezea maana bado yupo masikioni na machoni kwa watu na muziki wake unajulikana vilivyo

Je Wajua ?
Stevie Wonder hana uwezo wa kusikia harufu pia ana uwezo mdogo wa kutambua ladha ya kitu mdomoni

.
.
.
.

Mwisho
The Bitoz
..............
 
Naona ukiwa kipofu kazi rahis ni hyo ya kuimba mziki tu hamna kipofu mcheza mpira au basketball hata mmoja
Ukiwa mlemavu wa aina yoyote ile kuna mambo huwezi kufanya mfano kuwa Mwanajeshi
Ndio maana kwa Kiingereza huitwa Disable people
 
Back
Top Bottom