Wale wanaouza mabegi, vitenge kwa mnada na kurusha pale Ilala na Karume ni matapeli

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,632
Wale wanaouza mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha pale Ilala na karume ni matapeli

Unanunua kitenge unapewa begi bure na rubega 3 bure kwa elfu 5 tu Ngoja niwape taarifa mchukue tahadhari

Kwanza sipo hapa kuharibu biashara za watu. Ni hivi katika ya karume na ilala njiani pale kwenye kibao cha shule ya michikichini kunakuaga na wakaka wanauzaga nguo,mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha juu

Mtu ananunua Tisheti moja anapewa zawadi ya begi kubwa bure, Vitenge vya wax kigoma anapewa pair tatu bure, na rubega aka mkorori mbili bure hapo kanunue tishert ya 3000.....huu ni utapeli

Ngoja niwaambie wanachofanyaga Wanatafutaga kinadada ambao ni watu wao na kina kaka wanawachanganya katika ya watu kwahiyo wakiwa wanauza wanatupa ofa kama hizo wanawatupia wale wanawake wao kwamba eti ionekane kanunua kitenge kwa buku kapewa begi bure, mashuka bure na mashuka ya kimasai bure.

Wakishawarushia watu wao utaona wale wadada mmoja mmoja kwa wakati wake akijifanya anaondoka akifika huko ndani ndani anaenda kumkabidhi mtu wao maalum ambaye naye huzirudisha stoo then watazitoa kwa njia nyingine na kuzirudisha hapo mnadani.

Wanaopigwa na wapita njia ambao watavutiwa jinsi watu wanavyozawadiwa vitu basi wewe mpita njia utajiunga, watakuambia ununue tishet kwa elfu kumi then wanakwambia utulie watakupa zawadi ya bure, utaendelea kusubiria huku ukiona wenzako (wale watu wao) wakiendelea kuzawadiwa vitu kibao, wakiona una wasiwasi watakuambia nunua sasa upate mabegi mawili bure, utanunua utaambiwa mwishoni utapewa zawadi mwisho wa siku watafunga mnada na kusema usubiri wanakuja then watapotea wote mmoja mmoja.

Hao wadada na wakaka ambao ni watu fatilia kwa makini hata wakinunua wakitupiwa hizo zawadi ukiangalia kwa makini anayekusanya pesa za wanaolipa akiwasogelea wanajifanya wanatoa pesa lakini hawalipi anamsogelea masikioni na kumpa maelekezo kwamba ninini cha kufanya

Cha ajabu utakuta hao wadada wanaojichanganya na wanunuzi ni wao tu ndo hurushiwa hayo mabegi na mavitenge na zawadi halafu baadae wanarudisha kimya kimya hadi wanapoendaga kuviweka ili virudishwe mnadani napajua

Halafu hao hao wadada wanaojifanyaga wanunuz nawakutaga hapo kila siku kingine kama jioni au giza linaingia ili muuza mnada mtu wao aweze kuwatambua wadada wote hufunga vilemba, mitandio au vitambaa au kanga kichwani ili waweze kuwatambua.

Huo ni utapeli unaoendeleaga hapa ilala kwetu nimewapa taarifa mapema msanuke maana kila siku watu hulizwa hapa hubaki wakilia, yaani kila siku ni lazima nikute watu wakilia hapo na wengine wanaondokaga nyumbani na hela au kabeba hela kwa ajili ya mambo ya msingi akifika hapo anamalizia kwa hao matapeli anabaki bila hata nauli

Juzi kuna mama kalizwa kama elfu 90 hivi na alikopa Kwenye kikundi yule mama ilibidi aombe nauli, mwingine ni mtoto wa shule mpita njia aliona tishet kali akajichanganya elfu 50 aliyopewa na mzazi ikaliwa na wahuni akabaki akilia na kusaga meno.

Kuweni makini na hao matapeli wa mnada hapo njia ya kuelekea kati ya ilala na karume na huo mnada mara nyingi hufanyikia pale kilipo kibao cha shule ya michikichini Wapita njia kuweni makini
 
Ni wewe ndio umechelewa kushtuka. Hata Arusha wapo hawa.

Hivi mbona viashiria vya utapeli vipo wazi tu sijui hata Watu wanaoingia mkenge wanakwama wapi.

Kiashiria kikuu cha kwanza kamwe usiamini kama kuna Mtu yupo tayari kupoteza wewe upate...kwani wewe nani? isitoshe hata ukiwaangalia hao Wahusika tu kwa muonekano hawafanani kabisa na hicho wanachokihubiri.
 
Ni wewe ndio umechelewa kushtuka. Hata Arusha wapo hawa.

Hivi mbona viashiria vya utapeli vipo wazi tu sijui hata Watu wanaoingia mkenge wanakwama wapi.

Kiashiria kikuu cha kwanza kamwe usiamini kama kuna Mtu yupo tayari kupoteza wewe upate...kwani wewe nani? isitoshe hata ukiwaangalia hao Wahusika tu kwa muonekano hawafanani kabisa na hicho wanachokiubiri.
Fact
 
Wale wanaouza mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha pale Ilala na karume ni matapeli
Unanunua kitenge unapewa begi bure na rubega 3 bure kwa elfu 5 tuNgoja niwape taarifa mchukue tahadhari

Kwanza sipo hapa kuharibu biashara za watu
Ni hivi katika ya karume na ilala njiani pale kwenye kibao cha shule ya michikichini kunakuaga na wakaka wanauzaga nguo,mabegi,vitenge kwa mnada na kurusha juu

Mtu ananunua Tisheti moja anapewa zawadi ya begi kubwa bure, Vitenge vya wax kigoma anapewa pair tatu bure, na rubega aka mkorori mbili bure hapo kanunue tishert ya 3000.....huu ni utapeli

Ngoja niwaambie wanachofanyaga..... ....Wanatafutaga kinadada ambao ni watu wao na kina kaka wanawachanganya katika ya watu kwahiyo wakiwa wanauza wanatupa ofa kama hizo wanawatupia wale wanawake wao kwamba eti ionekane kanunua kitenge kwa buku kapewa begi bure, mashuka bure na mashuka ya kimasai bure

Wakishawarushia watu wao utaona wale wadada mmoja mmoja kwa wakati wake akijifanya anaondoka akifika huko ndani ndani anaenda kumkabidhi mtu wao maalum ambaye naye huzirudisha stoo then watazitoa kwa njia nyingine na kuzirudisha hapo mnadani

Wanaopigwa na wapita njia ambao watavutiwa jinsi watu wanavyozawadiwa vitu basi wewe mpita njia utajiunga, watakuambia ununue tishet kwa elfu kumi then wanakwambia utulie watakupa zawadi ya bure, utaendelea kusubiria huku ukiona wenzako (wale watu wao) wakiendelea kuzawadiwa vitu kibao, wakiona una wasiwasi watakuambia nunua sasa upate mabegi mawili bure, utanunua utaambiwa mwishoni utapewa zawadi mwisho wa siku watafunga mnada na kusema usubiri wanakuja then watapotea wote mmoja mmoja

Hao wadada na wakaka ambao ni watu fatilia kwa makini hata wakinunua wakitupiwa hizo zawadi ukiangalia kwa makini anayekusanya pesa za wanaolipa akiwasogelea wanajifanya wanatoa pesa lakini hawalipi anamsogelea masikioni na kumpa maelekezo kwamba ninini cha kufanya

Cha ajabu utakuta hao wadada wanaojichanganya na wanunuzi ni wao tu ndo hurushiwa hayo mabegi na mavitenge na zawadi halafu baadae wanarudisha kimya kimya hadi wanapoendaga kuviweka ili virudishwe mnadani napajua

Halafu hao hao wadada wanaojifanyaga wanunuz nawakutaga hapo kila siku kingine kama jioni au giza linaingia ili muuza mnada mtu wao aweze kuwatambua wadada wote hufunga vilemba, mitandio au vitambaa au kanga kichwani ili waweze kuwatambua....

Huo ni utapeli unaoendeleaga hapa ilala kwetu nimewapa taarifa mapema msanuke maana kila siku watu hulizwa hapa hubaki wakilia, yaani kila siku ni lazima nikute watu wakilia hapo na wengine wanaondokaga nyumbani na hela au kabeba hela kwa ajili ya mambo ya msingi akifika hapo anamalizia kwa hao matapeli anabaki bila hata nauli

Juzi kuna mama kalizwa kama elfu 90 hivi na alikopa Kwenye kikundi yule mama ilibidi aombe nauli, mwingine ni mtoto wa shule mpita njia aliona tishet kali akajichanganya elfu 50 aliyopewa na mzazi ikaliwa na wahuni akabaki akilia na kusaga meno

Kuweni makini na hao matapeli wa mnada hapo njia ya kuelekea kati ya ilala na karume na huo mnada mara nyingi hufanyikia pale kilipo kibao cha shule ya michikichini.....Wapita njia kuweni makini
Utapeli wa namna hii Ulikuwepo tangu miaka ya 90 kwa sie wahenga,
Kipindi hicho walikuwa hawatumii nguo,ni viberiti,au karata zinachezewa chini,zinachanganywa,unaulizwa umeiona,ukiweka hela umeliwa,aneweka hela,akala ni mtu wao,
Na siku zote huwa naamini,hakuna "free lunch"duniani,ukiona unapewa Bure au kwa bei kiduchu,gharama yake utalipa kubwa
 
Kweli hahaha
 
Back
Top Bottom