Wale mananga wa KWATA tukutane hapa

Nakumbuka siku moja A Coy walikuwa wamepangiwa fatiki jiko kuu pale Kunduchi, kama mnavyojua ukiwa kuruti hushibi vizuri kutokana na kibati unachopigwa,mimi na wenzangu 6 toka B Coy tukazamia kwenye fatiki ambayo haikuwa ya kombania yetu tukapiga mzigo tukala tukashiba vizuri sasa wakati tunajadili jinsi ya kuondoka,akatokea mkufunzi wa A Coy mnaa kishenzi Cpl Masire maarufu kama Kanda bongoman kutokana na kofia lake la pama alilokuwa anapenda kulivaa, baada ya kutuona aaaah! nilisikia tu akiwaita wenzake babaa kuna wavamizi huku,wakatutenga haya A Coy simama kulia kwangu tukabaki wavamizi toka Bravo tunahang hang tifu lililofuata hapo siwezi kulisahau kwanza tulididiga mle mle jikoni kama dk 40 huku fito zikitembea mgongoni,wakatuoa nje na kutuingiza kwenye mitaro iliyokuwa jiko kuu na kutuamuru tulale na kuanza kucrawl kutafuta samaki, yale maji yalikuwa na mabaki mabaki ya vyakula yalikuwa yananuka kishenzi,baada ya doso hilo wakatutoa mtaroni na kuamuru tuunde treni, yaani hapo ni kuchuchumaa na kushika kiuno cha mwenzako,Kanda bongoman akasema mtaruka kichura kwa kufuata mlio wa filimbi na hakuna kuachia kiuno cha mwenzako,uelekeo ni kwenye kombania yetu. Akaanza kupuliza filimbi tukaanza kuruka kichura, L/Cpl Didas akamwambia Kanda bongoman Baba mbona yanaruka huku hayaimbi? Ok sasa mtaruka huku mkitamka sisi ni wavamizi toka Bravo Coy. Yaani siku hiyo sitaisahau katika maisha yangu, kombat zilikuwa zinanuka uvundo wa maji mchafu,tulikabidhiwa kwenye Kombania yetu kwa Sgt Njowela a.k.a Idd Amin baba doso likaanza upya nilitamani nitoroke mafunzo lakini nilikomaa mpaka nikamaliza Depo. Kwa hiyo Jeshi sio kazi rahisi rahisi kama wengi wanavyodhani.
 
D

Laaaleki.
Duuuuuuuu, huyo kandabongomani noma sana.
Ila mliiva mpaka mliweza kuvamia kambi ya adui.
 
Wakati tuko Depo RTS Kunduchi, kipindi cha kwata kuna mkufunzi alikuwa anaitwa Ssgt Menyu alikuwa anaamuru platuni nzima ivue combat shirt, mnabaki na suruali ndio kwata linaanza, tulishamaliza kwata no.1 ya funga fungua. Tulikuwa kwenye kwata ya utembeaji, usimamaji na ugeukaji.Sasa huyu Ssgt Menyu alikuwa akitoa amri ya kutembea, sasa yale mausingizi ya wiki 6 na lile jua kali unakuta mtu anatembea huku amesinzia ngoma ina kuja pale anapoamuru platuni kuhalt,unapokosea yeye alikuwa hampigi yule aliyekosea, alikuwa anamshushia mabanzi ya mgongo mtu aliyekuwa nyuma ya yule aliyekosea huku akikuambia kwani wewe hukumuona.
hahahhaa hivi Menyu yuko wapi siku hizi??
 
Back
Top Bottom