Wakuu naishi vipi na 2d animation skills

Mechanic 97

JF-Expert Member
Feb 6, 2021
536
869
Wakuu nimekua nikitamani kufanya cartoon na 2d animation tangu niko shule. Hivyo imepita miaka mingi bila kutimiza ndoto kutokana na kutokuwa na resource mbalimbali.

Sasa mwaka fulani hivi nilipata wazo kuhusu cartoon nanipo mbioni kulitimiza lakini kimbembe nimekiona kwenye 2d animation Kwa maana sielewi nitauza vipi. Japo Nina kishikwambi Cha inch 10.1 na nilinunua app ya flipclip ambayo ni lifetime hivyo hivi vitu vimeniamsha kufanya jambo hili ila sielewi jinsi Nitauza
 
Wakuu nimekua nikitamani kufanya cartoon na 2d animation tangu niko shule. Hivyo imepita miaka mingi bila kutimiza ndoto kutokana na kutokua na resource mbalimbali. Sasa mwaka flani hivi nilipata wazo kuhusu cartoon nanipo mbioni kulitimiza lakini kimbembe nimekiona kwenye 2d animation Kwa maana sielewi nitauza vipi. Japo Nina kishikwambi Cha inch 10.1 na nilinunua app ya flipclip ambayo ni lifetime hivyo hivi vitu vimeniamsha kufanya jambo hili ila sielewi jinsi Nita uza
Mkuu fanya kazi kama freelancer kwenye site kama fiverr
 
Vikwazo vingi huko hafu huwezi kufanikiwa Kwa kiasi kikubwa unapata pesa za kawaida sana. Yaani Mimi nataka niwe msaani kama wasinii wengine.
Tafuta kozi mitandaoni. Kama huna hela pirate kozi, pita youtube, jiunge na communities reddit, fb, twitter etc....

Ungana na wenzako wenye ujuzi kama wako mnaweza anzisha production company au animation studio

Sema hii ni kama upo serious yaani unataka kufanya animation tu.

Hata freelancing sio mbaya kujaribu, vikwazo vitakujenga
 
Nimeshindwa kuiishi hii ndoto hadi sasa, sijui chochote kuhusu uandaaji wa animations lakini ni kitu napenda nifanye na contents mbalimbali nnazo.
2d animation kama unajua kuchora unaweza Anza hata Sasa ila katika ulimwengu wa 3d sikushauri inahitaji uwekezaji aisee nilisha jifunzaga blender ule mziki sio wa nchi hii hafu kwenye kutengeneza animation ndio utata mkuu sijui kuna ku add bone, sijui physics, mara kurender yaani ni hatari ila ukiweza 3d hata YouTube unapiga pesa tu. Maana kuna jamaa ni muhindi alikua anachannel ndio aliye ni inspire
 
Daaah bado sana kaka..
Kingine ili ujue haya mambo usijidanganye et utafanya Kwa simu ni uwongo .

Tafuta pc na tafuta mtu anayejua.
Haya mambo uwezi soma mtandaoni et kwa tutorial hapana..
 
2d animation kama unajua kuchora unaweza Anza hata Sasa ila katika ulimwengu wa 3d sikushauri inahitaji uwekezaji aisee nilisha jifunzaga blender ule mziki sio wa nchi hii hafu kwenye kutengeneza animation ndio utata mkuu sijui kuna ku add bone, sijui physics, mara kurender yaani ni hatari ila ukiweza 3d hata YouTube unapiga pesa tu. Maana kuna jamaa ni muhindi alikua anachannel ndio aliye ni inspire
So kama anajua kuchora 2d kashamaliza sio
 
Tafuta kozi mitandaoni. Kama huna hela pirate kozi, pita youtube, jiunge na communities reddit, fb, twitter etc....

Ungana na wenzako wenye ujuzi kama wako mnaweza anzisha production company au animation studio

Sema hii ni kama upo serious yaani unataka kufanya animation tu.

Hata freelancing sio mbaya kujaribu, vikwazo vitakujenga
Tatizo kuitransform freelancing kuwa big business ndio utata hafu mle una yonyeka sana. Kwa Sababu nimejaribu kuangalia client wengi wa animation wengi Wana YouTube channel ndio wanahost zile
 
Unanyonyeka?

Fursa ya kukuza ujuzi wako unaipata huku unalipwa halafu unasema unanyonyeka?

Haupo serious

Utabaki tu kuplan plan plan, utekelezaji zero.
 
So kama anajua kuchora 2d kashamaliza sio
2d animation kazi kumbwa ipo kwenye kuchora hayo mengine sijui animation mechanics, mambo ya frame ni kawaida sana. Ila wa 3d animation sijui modelling, texturing, sculpting, rigging, rendering sijui ndo uje kwennye animation mechanics, frame, storyboards ndio maana 3d animation huwa haifanywi na mtu mmoja
 
2d animation kama unajua kuchora unaweza Anza hata Sasa ila katika ulimwengu wa 3d sikushauri inahitaji uwekezaji aisee nilisha jifunzaga blender ule mziki sio wa nchi hii hafu kwenye kutengeneza animation ndio utata mkuu sijui kuna ku add bone, sijui physics, mara kurender yaani ni hatari ila ukiweza 3d hata YouTube unapiga pesa tu. Maana kuna jamaa ni muhindi alikua anachannel ndio aliye ni inspire
Mimi kuchora najua ndio kipaji changu. Hayo mengineyo ndio naanza kuyajua hapa ulivyoyaeleza maana watu wangu wa karibu niliowahi kuwashirikisha hili wazo walikuwa wananiona kama zimeanza kuniruka.
 
2d animation kazi kumbwa ipo kwenye kuchora hayo mengine sijui animation mechanics, mambo ya frame ni kawaida sana. Ila wa 3d animation sijui modelling, texturing, sculpting, rigging, rendering sijui ndo uje kwennye animation mechanics, frame, storyboards ndio maana 3d animation huwa haifanywi na mtu mmoja
Ooooh kumbe... Haya nimeelewa bana
 
Mimi kuchora najua ndio kipaji changu. Hayo mengineyo ndio naanza kuyajua hapa ulivyoyaeleza maana watu wangu wa karibu niliowahi kuwashirikisha hili wazo walikuwa wananiona kama zimeanza kuniruka.
Jamii zetu bado sana aisee ila bado unaweza mkuu wenyewe wanasema hii fani unastafu Hadi pindi ambapo mikono yako itakuwa haiwezi kushika pencil chakufanya tafuta tablet la android hili ni cheap sana. Na application kama vile flipclip na ibis paint
 
Wakuu nimekua nikitamani kufanya cartoon na 2d animation tangu niko shule. Hivyo imepita miaka mingi bila kutimiza ndoto kutokana na kutokuwa na resource mbalimbali.

Sasa mwaka fulani hivi nilipata wazo kuhusu cartoon nanipo mbioni kulitimiza lakini kimbembe nimekiona kwenye 2d animation Kwa maana sielewi nitauza vipi. Japo Nina kishikwambi Cha inch 10.1 na nilinunua app ya flipclip ambayo ni lifetime hivyo hivi vitu vimeniamsha kufanya jambo hili ila sielewi jinsi Nitauza

Hongera mkuu kwa jitihada za kutaka kufanikisha malengo yako.

Naamini tatizo na changamoto kubwa ni kwenye ubunifu na kwa namna gani utaweza kufanya projects zako?

Fanya kitu cha tofauti mkuu watu tutakutafuta.

Hapo umesema kishikwambi?

Unamaanisha
Graphics tablet=kishikwambi.

Bilashaka utakuwa unaifahamu smith micro anime studio
Kitambo sana nimefanya 2d na hii kitu.
 
Jamii zetu bado sana aisee ila bado unaweza mkuu wenyewe wanasema hii fani unastafu Hadi pindi ambapo mikono yako itakuwa haiwezi kushika pencil chakufanya tafuta tablet la android hili ni cheap sana. Na application kama vile flipclip na ibis paint
Nitatafuta mkuu muda nipo free nifanye nachokipenda.
 
Nimeshindwa kuiishi hii ndoto hadi sasa, sijui chochote kuhusu uandaaji wa animations lakini ni kitu napenda nifanye na contents mbalimbali nnazo.

Mkuu unaweza.

I dare you to start with a stick man character

Mkuu kama ulishawahi hata kutengeneza powerpoint presentation yenye mishale ina rotate ujue tayar ulishafanya animation.
 
Hongera mkuu kwa jitihada za kutaka kufanikisha malengo yako.

Naamini tatizo na changamoto kubwa ni kwenye ubunifu na kwa namna gani utaweza kufanya projects zako?

Fanya kitu cha tofauti mkuu watu tutakutafuta.

Hapo umesema kishikwambi?

Unamaanisha
Graphics tablet=kishikwambi.

Bilashaka utakuwa unaifahamu smith micro anime studio
Kitambo sana nimefanya 2d na hii kitu.
Hapana sio graphics tablet ni tablet la kawaida tu kama simu tu ila lenyewe nalipendea Kwa Sababu ya large surface. graphics tablet ni Bei ghali mno micro anime mm sijaipata ila kitambo hicho nilianzaga na stoppola hii niliona itanighalimu kwakuwa ilikua unachorea nje then unascan picha kwenye app nikaona jau nikaja kujua kuhusu flipclip mayo haikua nzuri Kihivyo ila update za hivi karibuni zimenifanya nione fursa inawezekana.
 
Mkuu unaweza.

I dare you to start with a stick man character

Mkuu kama ulishawahi hata kutengeneza powerpoint presentation yenye mishale ina rotate ujue tayar ulishafanya animation.
Power point nimewahi tengeneza sana, kivipi ni animation?
 
Back
Top Bottom