Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 943
- 4,458
Nimeona madhara yaliyoletwa na maji kwenye eneo la Rufiji. Nafahamu wapo watu wanapiga propaganda kuhusu bwawa la umeme kuwa ni chanzo cha mafuriko haya.
Ndugu zangu tumetoka kwenye mgawo wa Umeme juzi tu; tunapoona umeme umerejea bila mgawo tutambue wapo viumbe wazalendo walifikiria kuikomboa nchi na janga la umeme hata kupelekea wakapoteza uhai.
Tunapaswa kuwashukuru kwa uthubutu na kuendelea kuwapongeza kila tunapowasha taa ya umeme nyumbani au kazini.
Hatupaswi kuwakatisha tamaa wanaoona mbele tunapaswa kuwaandika kwa wino wa dhaabu. Ni kweli Rufiji imepata madhara kama ambavyo Morogoro wamepata madhara.
Ili kumsaidia Mhe. Rais nashauri watu wa Rufiji waliopata tatizo la mafuriko wapelekwe Msomera wakaishi huko na eneo lenye mafuriko libaki sehemu ya hifadhi.
Kupanga nikuchagua; tuwalipe fidia kwa madhara wanayopata kisha tujadiliane nao kuhusu kuhamia sehemu salama. Cha msingi utaratibu uwe shirikishi na fidia iendane na mahitaji ya sasa. Contrary ipo siku tutapata msiba mkubwa hapa nchni kwa mafuriko.