Wajerumani na majina ya Kitanganyika

ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,746
5,437
Napenda kujua ni kwa namna gani wajerumani walitumia kuyapa majina haya maeneo ya Tanganyika enzi za ukoloni majina ya kijerumani?
German placenames
Most place names in German East Africa continued to bear German spellings of the local names, such as Udjidji for Ujiji and Kilima-Ndscharo or Kilimandscharo for Mount Kilimanjaro. (Kigoma was known for a time as Rutschugi.) The few exceptions to the rule included
as well as German translations of some local phrases, such as Kleinaruscha for Arusha-Chini and Neu-Moschi for the settlement that is now known as Moshi. Lake Eyasi was known as the "Hohenlohe Sea", and the mission town of Sankt-Michael (St. Michael) near Kahama was formerly more important
 
Sijaelewa lengo hasa la mada yako. Yaani unataka kuja nini hasa?

Mkuu majina uwezi kuyabadili kwa lugha yoyote ile, mfano mimi naitwa Ruhi uwezi kuniita Juma kwa kisa unaongea/tumia lugha ambacho ni tofauti na lugha yangu.

Hivyo ningependa kujua ni namna gani wajerumani walitumia kuyapa maeneo ambayo kulikua yanafaamika tayari kwa majina kutokana na wakazi wake, ni kwanini hawakuendelea kutumia majina waliyoyakuta wakayaita tena kwa lugha yao?
 
Kama nimekuelewa vizuri basi mchango wangu ni huu: Kwanza, kama ulivyosema, kuna baadhi ya maeneo kama Arusha,Kilimanjaro na Moshi, ambako Wajerumani waliendelea kutumia majina waliyoyakuta. Hata hivyo waliyaandika majina hayo kulingana na jinsi ambavyo wao waliweza kuyatamka (tunaita sound-spelling). Mfano mzuri hapa ni Kilimandscharo (Kilimanjaro), Aruscha (Arusha) na Moschi (Moshi). Linganisha: sauti [sh] (kiswahili) ----> [sch] (Kijerumani); sauti [nj] (Kiswahili) ----> [ndch] (Kijerumani), na sauti [j] (Kiswahili) ----> [dz] (Kijerumani).

Pili, katika maeneo mengine, Wajerumani (hata wakoloni wengine) hawakutumia majina waliyoyakuta kwa wenyeji Bali wakaleta majina mapya. Majina haya yalitokana na majina ya watawala wao na watu wao wengine maarufu. Mifano mzuri hapa inaweza kuwa Wilhelmstal/Wilhelmsdorf (Lushoto/Handeni?), Bismarckburg (Kasanga/Rukwa?) na Langenburg (Tukuyu). Ikumbukwe kuwa Wilhelm ilikuwa mtawala wa Ujerumani na Bismarck alikuwa ni Kansela maarufu wa Ujerumani (ndo yule wa Berlin conference).

Pia yapo maeneo yaliyopachikwa majina ya miji, vitongoji na mitaa ya Ujerumani. Nadhani hapa mifano kama Neu-Trier (Mbulu), Neu-Hornow (Honnow?), Neu Bonn (Mikese?), Weidhafen (Manda?) n.k. inahusika.

Nadhani nitakuwa nimekupa dondoo kidogo.
 
Mm Niko Uvinza ila Kila nikiuliza wenyeji maana ya jina Hilo hawana majibu yakutosheleza..
 
Sijui kwanini wamlitutawala lakini hawakuacha urithi wa rugha kabisa 🤔🤔
 
Nipo kyela...
Hii nchi ingekuwa ulaya ndogo kama tungetawaliwa na huyu bwana.

Tusingekuwa wavivu na tungekuwa na asili ya kujituma.

Alikuwa anania kubwa sana ya kutuendeleza kama jimbo la taifa lake.

Alikuwa ana Plan ya kupitisha Reli kwenye kata ya Mwaya ambayo kwa sasa dah imechoka sana nashindwa kueleza.

Nimefurahi sana kuona maeneo kama Lumbila na ikombe tayari yalipewa majina na mgermany miaka hiyo... kwa sasa ni porini na eneo kama ikombe kyela ni eneo lisilofikika... miaka 70 ya uhuru wanaikombe wanashuhudia kwa mara ya kwanza umeme ukiwashwa kwao 2023 na barabara ikijengwa kwao 2024... that is disaster
 
Ukitumia neno shule katika Kiswahili, ujue hilo ni neno la Kijerumani tumetohoa kutoka "schule". Ndiyo maana Zanzibar walipokuwa na infkuence ya Uingereza zaidi hawatumii sana neno shule, wanatumia skuli.

Ukitumia neno hela, kulikuwa na sarafu ya Kijerumani iliitwa "Heller".

Hiyo mifano michache tu.
 
Hata neno DUKA ni kijerumani neno Dukan, Pesa (peso) kireno, meza (mezr) kireno
 
Sijui kwanini wamlitutawala lakini hawakuacha urithi wa rugha kabisa 🤔🤔

Rugha ni nini?

If you mean lugha, unataka lugha yao ya nini? Kiswahili kinakushinda hiyo ya watu utawezea wapi?
 
Nipo kyela...
Hii nchi ingekuwa ulaya ndogo kama tungetawaliwa na huyu bwana.

Tusingekuwa wavivu na tungekuwa na asili ya kujituma.

Alikuwa anania kubwa sana ya kutuendeleza kama jimbo la taifa lake.

Alikuwa ana Plan ya kupitisha Reli kwenye kata ya Mwaya ambayo kwa sasa dah imechoka sana nashindwa kueleza.

Nimefurahi sana kuona maeneo kama Lumbila na ikombe tayari yalipewa majina na mgermany miaka hiyo... kwa sasa ni porini na eneo kama ikombe kyela ni eneo lisilofikika... miaka 70 ya uhuru wanaikombe wanashuhudia kwa mara ya kwanza umeme ukiwashwa kwao 2023 na barabara ikijengwa kwao 2024... that is disaster
Usemavyo ni kweli. Ukisoma kwenye kitabu cha von Lettow Vorbeck "My Reminiscences of East Africa" anaonyesha dhamira, malengo na maono ya Wajerumani kwenye koloni lao la Afrika Mashariki. Pia, anakuonyesha kiwango cha maendeleo kilichokuwepo kipindi hicho. Kwenye kitabu "Battle for the Bundu" kilichoandikwa na John Miller anatueleza Wajerumani walikuja Afrika Mashariki kuishi na siyo kuchuma. Walikuwa na mipango thabiti ya kuendeleza eneo hili. Maeneo mengi yalyokuwa maarufu kipindi hicho leo ni dhooful hali. Hata Kilimatinde ulikuwa mji maarufu enzi za Wajerumani lakini leo hii chali.
 
Back
Top Bottom