Waafrika wengi zaidi waanza kujifunza Kichina

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,023
1,047
W020230216834551714680.png


728.jpg


Lugha ni moja ya vyanzo vikuu vya mawasiliano kati ya watu wa tamaduni tofauti, na ufahamu wa lugha unasaidia katika mawasiliano kati ya pande husika.

China ni nchi ambayo imejikita katika uwekezaji katika nchi za nje, na hivyo ufahamu wa lugha hiyo ni moja ya vyanzo vya ajira katika nchi nyingi ambako China imewekeza.

Lugha ya Kichina inaendelea kupata umaarufu katika nchi mbalimbali duniani, na wengi wanaojifunza lugha hiyo, wanasema inatokana na fursa nyingi za ajira, hususan katika kampuni za China ambazo zimewekeza katika nchi nyingi duniani.

Barani Afrika, kuna Taasisi 61 za Confucius na Madarasa 48 yanayotoa mafunzo ya lugha hiyo. Licha ya hayo, kwa kushirikiana na China, nchi 16 za Afrika zimeingiza somo la lugha ya Kichina katika mitaala rasmi ya masomo.

Hvi karibuni, darasa la Confucious la Shule ya sekondari ya State House nchini Kenya lilizinduliwa rasmi. Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mkuu wa shule hiyo Everlyn Nabukwesi aliwahamasisha wasichana hawa kujifunza kichina kwa bidii, na kufahamu vya kutosha China.

Nchini Ethiopia, wafanyakazi katika Kurugenzi ya Huduma za Kigeni iliyo chini ya Idara ya Huduma za Uhamiaji na Uraia nchini humo wameamua kujifunza lugha ya Kichina ili kuweza kuwasiliana kirahisi na wageni kutoka nchini China.

Teshager Moga, mfanyakazi katika Kutugenzi hiyo, anasema kikwazo cha mawasiliano ni jambo kubwa wanachokumbana nacho kila siku katika kuwasiliana na raia wa kigeni. Anasema raia wa China wanachukua idadi kubwa ya raia wa kigeni wanaokwenda katika ofisi yao kila siku kushughulikia mahitaji ya visa na mambo mengine, na licha ya juhudi za kuziba pengo la mawasiliano hususan katika kuwasiliana na raia wa China, bado kuna changamoto ambazo zinajitokeza.

Hivyo, Moga na wafanyakazi wenzake 19 kutoka Kurugenzi tano zilizo chini ya Idara ya Huduma za Uhamiaji na Uraia wameanza mafunzo ya miezi mitatu ya lugha ya Kichina. Mafunzo hayo ya muda mrefu yatakayotolewa katika Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, yanatarajiwa kuwawezesha maofia hao kuwa uelewa wa kimsingi wa lugha ya Kichina.

Moga anasema, mafunzo hayo ya miezi mitatu sio tu yatamwezesha yeye na wafanyakazi wenzake kuwa na ujuzi wa lugha ya Kichina, lakini pia yatawasaidia kuifahamu zaidi China na watu wake. Amesema anatarajia baada ya mafunzo hayo wataweza kuwasiliana vizuri na kuwahudumia raia wa China, na hivyo kuboresha kidhahiri utoaji wa huduma za kila siku.

Berelihem Hate, mmoja wa wanafunzi 20 watakaopata mafunzo hayo, anasema ana matarajio mazuri sana kwa kuwa wataweza kuzungumza na kuelewa vizuri lugha ya Kichina, na hatimaye kuwasaidia katika kuhudumia raia wa China. Anasema kutokana na kikwazo cha lugha kilichopo, Idara hiyo iliwahi kuajiri mkalimani wa lugha ya Kichina ili kusaidia mawasiliano na raia wa Kichina, lakini hata hivyo bado mahitaji ni makubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Uhamiaji na Uraia ya nchini Ethiopia, Bruhtesfa Mulugeta amesifu mafunzo hayo, na kuwataka wanafunzi kuhudumu kama daraja kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Ofisa Mkuu Mwandamizi wa Ubalozi wa China nchini Ethiopia, Shen Qinmin amesema, ushirikiano katika elimu ya lugha kati ya nchi hizo mbili umeweka msingi wa uhusiano wa nchi hizo katika sekta zote na kutumika kama nguzo ya ushirikiano wa kivitengo katika ngazi zote. Amesema kuwawezesha watoa huduma, kama wafanyakazi katika Idara ya Huduma za Uhamiaji na Uraia ya nchini Ethiopia kuwa na uwezo zaidi wa kuwasiliana, kutajenga mazingira chanya katika kuboresha uzoefu wa raia wa China nchini Ethiopia.
 
Watz wajifunze kingereza kwanza , maana mwisho wa safari watajikuta hawana Huwezo wa kuongea lugha yoyote kwa ufasaha. ..hii ilimtokea Rais wa Tz awamu ya Tano .
 
Na ndani ya miaka kumi ijayo nchi nyingi za Kiafrica zitakipa kisogo kizungu na kutumia kichina kama lugha ya kufundishia.
EAC & Central Africa ndio target na wameshaingia makubaliano hayo kimyakimya
 
Na ndani ya miaka kumi ijayo nchi nyingi za Kiafrica zitakipa kisogo kizungu na kutumia kichina kama lugha ya kufundishia.
EAC & Central Africa ndio target na wameshaingia makubaliano hayo kimyakimya
mwandende in nyakyusa voice hicho kingreza kinatutoa jasho itakuwa kichina babax weeee
 
Back
Top Bottom