ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,019
- 7,223
Ingawa makundi mbalimbali nchini yatamkumbuka sana, vyama vya upinzani vitakuwa kundi la kwanza kumkumbuka na kummiss Rais Kikwete.
Kikwete ni Rais pekee aliyeuvumilia, kuupa uhuru na kuupalilia upinzani njia ya kujiboresha. Iwapo wapinzani wangekuwa makini, wangenufaika sana na uhuru huu waliopewa.
Historia itamkumbuka Kikwete kama Rais aliye tayari kusikiliza mawazo tofauti hata yale yanayolenga kumshambulia. Wapinzani wameshindwa kutumia fursa hii kujipatia angalau 45% ya Bunge. Fursa adimu kama hii haitakuwepo tena kwenye awamu ya tano.
Tabasamu la Kikwete ambalo wapinzani aghalabu wamekuwa wakilikejeli ni miongoni mwa vitu watakavyovimiss sana wanapohutaji muafaka wa masuala ya kisiasa ya kitaifa. Hili litakuwa somo kuwa kitu hukithamini mpaka kitakapokosekana.
Uongozi wa awamu ya nne ulikuwa haupendi shuruti. Ulikuwa unatoa muda wa kufikiria. Ulikuwa unatoa nafasi ya kujirekebisha. Wapinzani walikuwa mbele kupinga aina hii ya uongozi. Kwa bahati, umekuja uongozi wa aina tofauti.
Mlichokiomba mmekipata...