utakuja
JF-Expert Member
- Sep 20, 2010
- 991
- 801
Habari zenu wakuu! Kama muhanga wa bei hizi kubwa za vifurushi vya intaneti (ambaye siishi karibu na eneo lenye Fibre) nilivyosikia kwamba Vodacom leo wanazindua huduma za 5G kwa majumbani-- nilijawa na furaha, lakini baada ya kuingia kwenye ukurasa wao mahususi wa kufanya 'pre-order' kidogo nikaishiwa na nguvu. (Kama inavyoonekana pichani) Bei hizi si rafiki kwa Mtanzania na sielewi walikuwa wanafikiria nini.