Vodacom acheni kuchezesha bahati nasibu kwa wateja wenu

wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,454
4,376
Kampuni ya Vodacom imekuwa ikichezesha bahati nasibu kwa wateja wao mf. 'Jay milioni' na hii 'Kamata mpunga' ya sasa.

Wateja wa Vodacom wamekuwa wakitoza pesa kila wateja wao wanaposhiriki bahati nasibu hizo.

HOJA

1. Vodacom ni kampuni inayojihusisha na mawasiliano na huduma za kifedha hii bahati nasibu ni kuwanyonya watanzania walipaswa kutoa zawadi kama reward kwa wateja wao. Mf. kampuni za soda, benki zimekuwa zikitoa zawadi kwa wateja wao pasipo kuchangishwa au tozo ya ushiriki wa kupata zawadi.

2. Vodacom kuchezesha bahati nasibu haiko sawa maana wao ndio wanakusanya pesa na wao ndio wanachezesha hiyo bahati nasibu hapa ni rahisi kudanganywa katika mapato yao na utoaji wa zawadi.

Mytake:
TCRA wazuie Vodacom kuchezesha bahati nasibu
kama utoaji wa zawadi uwe huru kwa wateja wote pasipo tozo au makato ya pesa za ushiriki.
 
SIO YA KUKOSA: 7xxxxxx0969 hii ni KAMATA MPUNGA ya Vodacom! TUMA NENO GO KWENDA 15544 & UNAWEZA KUSHINDA TZS 5,000,000.
TZS 300/SMS




nikifika hapo kwenye TZS 300/SMS HUWA HATA SISHIRIKI KWA NAMNA YOYOTE ILE.
 
Kampuni ya vodacom imekuwa ikichezesha bahati nasibu kwa wateja wao mf. Jay milioni na hii kamata mpunga ya sasa.

Wateja wa vodacom wamekuwa wakitoza pesa kila wateja wao wanaposhiriki bahati nasibu hizo.

HOJA

1. Vodacom ni kampuni inayojihusisha na mawasiliano na huduma za kifedha... hii bahati nasibu ni kuwanyonya watanzania walipaswa kutoa zawadi kama reward kwa wateja wao.
mf. kampuni za soda, benki zimekuwa zikitoa zawadi kwa wateja wao pasipo kuchangishwa au tozo ya ushiriki wa kupata zawadi.

2. vodacom kuchezesha bahati nasibu haiko sawa maana wao ndio wanakusanya pesa na wao ndio wanachezesha hiyo bahati nasibu.... hapa ni rahisi kudanganywa ktk mapato yao na ktk utoaji wa zawadi...

mytake:
TCRA wazuie vodacom kuchezesha bahati nasibu
kama utoaji wa zawadi uwe huru kwa wateja wote pasipo tozo au makato ya pesa za ushiriki.
TCRA hawana jukumu hilo, wenye jukumu ni Tanzania Gaming Board
 
TCRA hawana jukumu hilo, wenye jukumu ni Tanzania Gaming Board

hoja ni kwamba zipo baadhi ya huduma muhusika awezi kuuza au kufanya mwenyewe kuepuka ubabaishaji na ulaghai au wizi...
mf. kuuza hisa lazima kuwepo na wakala na watu wengne wanaosimamia tofauti na kampuni inayouza hisa.
 
Hivi huwa wanawavuta kucheza hizo kamari?

Sijawahi kuamini katika bahati nasibu, huu ni wizi unaofanywa bila nyie wateja kujua.

Ukisha tuma hiyo sms kwenda kwenye hiyo Code ambayo ghalama yake ni 300 tayali unakuwa umeshaichangia kampuni au mtu wao wanaetaka ashinde.

Watanzania huwa tunaibiwa kijinga kijinga tu unakuta mtu anatuma sms kumi kwa siku na vocha yenyewe ya kubangaiza.

Wanaotuma hizo meseji wengi ni maskini kwa kutaka utajiri wa haraka.
 
Back
Top Bottom