Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 575
- 2,559
Tende ni matunda yenye kiasi kikubwa cha nyuzilishe, protini, nishati, madini chuma, Calcium, zinc, copper, magnesium pamoja na aina mbalimbali za sukari.
Huwa pia na viondoa sumu vya Beta Carotene, Lutein na Zeaxanthin pamoja na vitamini A, K na folate.
Tende huwa faida nyingi kwa afya yako, baadhi yake ni hizi;
Huwa pia na viondoa sumu vya Beta Carotene, Lutein na Zeaxanthin pamoja na vitamini A, K na folate.
Tende huwa faida nyingi kwa afya yako, baadhi yake ni hizi;
- Huwa na kampaundi za Flavonoids ambazo husaidia kupambana na aina mbalimbali za uvimbe pamoja na kuzuia saratani, kisukari na magonjwa ya akili.
- Huwa na Kampaundi za Carotenoids ambazo huhusikana utoaji wa rangi halisi za matunda. Kampaundi hizi huboresha afya ya moyo na macho.
- Hurahisisha uchungu wa kujifungua, hasa zikitumiwa na wanawake walio kwenye hatua za mwisho za ujauzito
- Huimarisha mifupa sababu ya uwepo wa madini ya phosphorus, calcium na Magnesium
- Hurahisisha choo