Viongozi wetu-proactiveness mbona zero? Au tunasubiri maafa tuunde tume na team za misiba?

the power

Senior Member
Oct 18, 2012
127
220
Fungua attachment 1 na 2 chini. Hilo ni daraja kuu Mwanza, uhuru kwa chini. Ukipita juu ya daraja limeshaanza kumomonyoka picha namba moja. Ukikaribia kulia utaona daraja kubwa hilo lote limejaa mchanga upande wa maji yanapoingilia kweye daraja (picha na 2), huo ni mchanga vimaji hivyo vinapita kwa juu, huo mchanga unaweza kufika malori zaidi ya 100 kwani jiulize mchanga wa kujaza mto mkubwa kuanzia juu kule kwenye daraja lingine mpaka chini kwenye daraja hili si jambo la siku moja ni miaka

Kasheshe ni kwamba mvua kidogo tu maji yanapita juu, ndani ya daraja, mchanga tupu, umeziba na huo mchanga unaendelea upande wa pili chini.Kwenye mvua ya kawaida tunakimbia kabisa kupita hapo, ila majasiri wanapita.

Swali la kujiuliza ni mbali ya viongozi wote wote kupita kwenye daraja hili angalau mara moja kwa wiki, je hawaoni tatizo? je hawaoni jinsi ambavyo daraja lenyewe limeishaanza kutoboka kwa juu? Je tunauhakika gani mvua ikinyesha magari yanaweza kupita juu ya daraja lililobomoka na kuleta mahafa makubwa kama yale tuliyoshuhudia kwa wanafunzi wa mkoa mwingine? Je mkoa, jiji, wilaya , kata, mtaa kweli hatuoni kifo mbele yetu.

Ndio maana tunasema kwa viongozi wetu " Proactiveness Yetu ni Zero;Tunasubiri Mahafa Tuunde tume na team za misiba.

Najua utabisha? sawa, soma vizuri andiko, tunakuwa very active kwenye majanga yakitokea, zitaundwa tume, kamati, michango ya misiba na mafungu yatafunguka kuhudumia wahanga, ni vyema na haki. Swali ni kwa nini hiyo nguvu, hizo pesa zisitumike sasa hivi kuzuia mahafa hayo? Nina uhakika bila kurekebisha mapungufu kwenye hili daraja, soon tutashuhudia janga la mwaka. Huhitaji kuwa engeneer kuona ukuta uliobomoka, kuona mchanga ulioziba njia ya maji.

20240422_155723.jpg
20240422_155735.jpg
 
Mkuu umepiga picha ukiwa juu ya daraja?

Daraja unalozungumza ni hilo lililopo mbele ya dereva boda?
 
Ahaa nimepiga picha nikiwa kwenye daraja kuonyesha mchanga ulivyoziba daraja zima mpaka level ya juu ya daraja, maji sasa yanapita juu ya daraja kila kamvua kakinyesha. Mvua ya kawaida tu huwezi pita,achilia mbali mvua kubwa hiyo mnabadilisha njia kabisa Kibaya hilo daraja limeshaanza kuonyesha kuharibika upande wa kulia. Na hiyo ndiyo hofu yangu
 
Back
Top Bottom