MVENGEVENGE
Senior Member
- Sep 15, 2011
- 158
- 37
tupeni uzi kamili wanashtakiwa kwa makosa aina gani, ndio tujadili yana dhamana au hayana
na kusababisa mauaji?wameshtakiwa kwa uchochezi,kuvuruga amani,uharibifu wa mali za watu na miundombinu ya barabara.Wote wamenyimwa dhamana,kesi itatajwa tena tarehe 25 Oct.
sourcew
Kweli kabisa 100%. Kutakuwepo na heshima kubwa baadaye!!sasa kama serikali inataka kuanza kuwa serious, wasionewe, wapewe haki zote za watuhumiwa na utu na uhuru wao uheshimiwe ikiwa ni pamoja na dhamana ila kesi iendeshwe kufuata sheria za nchi bila shinikizo za kidini au za kisiasa!
Safi sana! Tena wasipewe dhamana!
Sheria imnyonge Mwnananchi tu ? Jeshi la police jee? nchi haina sheria la kushitaki jeshi la police ? Kuna mauwaji mangapi hapa nchini kwa raia wasiokuwa na hatia kwa jeshi la police ?sasa kama serikali inataka kuanza kuwa serious, wasionewe, wapewe haki zote za watuhumiwa na utu na uhuru wao uheshimiwe ikiwa ni pamoja na dhamana ila kesi iendeshwe kufuata sheria za nchi bila shinikizo za kidini au za kisiasa!
Taarifa ya moja kwa moja kutoka Star Tv, imesema viongozi wa Uamsho wapatao kumi hivi wamefikishwa mahakamani huko Zanzbar..!
Taarifa ya moja kwa moja kutoka Star Tv, imesema viongozi wa Uamsho wapatao kumi hivi wamefikishwa mahakamani huko Zanzbar..!
Aseeeee!!للجنة الدعوة الإسلامية
Kumbuka vitu viwiliSheria imnyonge Mwnananchi tu ? Jeshi la police jee? nchi haina sheria la kushitaki jeshi la police ? Kuna mauwaji mangapi hapa nchini kwa raia wasiokuwa na hatia kwa jeshi la police ?
Kwa upande wangu mimi sikubaliani na mwananchi yoyote atoke taasisi yoyote asitakiwe na serikali kwa sababu zisizo kuwa za msingi,na hasa ukiangalia kesi kama ya uwamsho,ukiangalia begining ya shekh farid ya kutekwa ina mtuhani mkubwa.Kumbuka vitu viwili
1.Mauaji yaliyofanywa na police hayawezi kuhalisha mauaji yaliyofanywa na UAMSHO (kosa la mtu mmoja halihalalishi ya mtu mwingine)
2.Thread iliyo mbele yetu inahusu viongozi wa uamsho kufikishwa mahakamani ndio maana tunaijadili kwa muktada huo sasa hili la police kuua bila kushitakiwa lilishajadiliwa sana hapa na kama hujaridhika iwekee thread yake tutatoa maoni yetu, bila kusahau anayetuhumiwa kuumua Mwangosi amefikishwa mahakamani!
Ni lazima watu wa aina yako watakuwa na matatizo ya akili, hivi unadhani hapa ni nani mtoto mdogo wa kumdanganya kwamba huyo Gaidi kiongozi wa UAMSHO alitekwa? si kweli ni uongo mtupu alijificha ili lengo lake la kuleta machafuko litimie.Kwa upande wangu mimi sikubaliani na mwananchi yoyote atoke taasisi yoyote asitakiwe na serikali kwa sababu zisizo kuwa za msingi,na hasa ukiangalia kesi kama ya uwamsho,ukiangalia begining ya shekh farid ya kutekwa ina mtuhani mkubwa.
Kwanza hakuna ushahidi wa kutosha kuwa alitekwa na police wa usalama, wakili wake ana kazi kubwa kumtetea kwa sababu hizo watuhumia walio mteka walitumia njia ya kijasusi.
Pili amani iliyo vunjwa na wananchi haihusiani na viongozi wa uwamsho,kwa sababu walio fanya sio uwamsho bali ni wananchi wakawaida kama mimi nawewe tunaweza kungia barabarani na kufanya fujo na kuharibu mali za wananchi.
Tatu kuna kesi ya mauwaji ya police eneo la bububu mjini maghribi Unguja,ambao halihusiani na uwamsho,kwa sababu maeneo ambayo walikuwa hayako katika usalama ,ni Darajani,Amani,Kwa mtipura sijui,mbuyuni,ni maeneo ya mjini tu.
Kwa uchunguzi wangu kwa mauwaji ya police, kumbuka kuwa au kama ulisikia aliuliwa mtoto wa miaka 14 eneo hilo la bububu ambapo alipo uliwa police kinyama,mtoto huyo aliuliwa na jeshi la police,serikali imeshindwa kutoa maelezo na kuhalalisha mauwaji hayo, kwa maana hiyo naamini mauwaji ya police yefanywa na wananchi wenyewe hasira wa eneo hilo na sio uwamsho.
Jengine ukubali usikubali uwamsho imekuwa kama vile jaa la taka,kwa vile jumuiya hii ndio ambayo inahamasisha wanzanzibar kudai zanzibar huru ambapo ni kinyume cha sera ya ccm, pamoja na serikali tawala,na ndio maana wanawapga vita uwamsho kwa kila njia ili kuwasukumizia makosa ya ajabu ajabu kupata nafasi ya kuwasambaratisha.
Amini usiamini hii ni agenda maalum, lakini wananchi mara hii watashinda, ccm ipo hoi inasambaratika taratibu.