Viongozi wa dini, iepukeni dhambi hii

Mushkov

Member
Feb 16, 2024
58
125
Kwa kipindi hiki tunapoelekea kwenye chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka unaofuata kumekuwa na tabia ya viongozi wa serikali kuwaalika viongozi wa Dini kwenye matukio mbalimbali. Lakini pia kumekuwa na kawaida ya viongozi wa serikali kutoa mamilioni ya shilingi kama michango ya ujenzi wa Makanisa na Misikiti.

Kwa maoni yangu hali hii inawafanya viongozi wetu wa Dini kutoona shida wanazokumbana nazo Watanzania zinazosababishwa na uzembe wa viongozi wa serikali. Lakini pia inasababisha viongozi wa Dini kutosimama na wananchi ambao ndo Waumini wao na badala yake kusimama na viongozi wa serikali ambao baadhi yao si wasafi.

Hii imesababisha pia viongozi wetu wa Dini kukaa kimya hata kama wananchi wanalia namna gani kwa madhulumu mbalimbali. Tunataka kuona viongozi wa Dini wanakuwa mstari wa mbele katika kudai haki katika Nchi hii. Wasifungwe midomo na Bahasha na michango ya ujenzi wa Makanisa na Misikiti.

Viongozi wa Dini simameni imara kudai na kutetea haki katika Taifa hili.
 
Kitu ambacho unashindwa kukijua ni kuwa dini ni kilaainishi cha serikali na utawala ili ifanye kazi yake kwa urahisi,huwezi itenga dini na serikali kamwe.
 
Back
Top Bottom