Vifaa vya umeme na electronic vya hospitali vinafanyiwa maintanance na repair wapi?

Rog chimera

JF-Expert Member
Apr 28, 2018
367
602
Habari ndugu zangu kwa wale wanaofanya kazi kwenye vituo vya afya .je vifaa kama xray, ct scan ,ultrasound machine zinapoharibika huwa zinapelekwa wapi kufanyiwa matengenezo?
 
Naskia huwa inabidi aitwe fundi kutoka kwa waliotuuzia.

Mfano mtaalamu kutoka Siemens etc

Stori niliyoisikia sio kuharibika tu. La ni hata uneme ukikatika kuna mashine zitatakiwa kucallibratiwa na fu di wa kampuni, anapanda ndege anakuja.
 
Habari ndugu zangu.kw wale wanaofanya kazi kwenye vituo vya afya .je vifaa kama xray, ct scan ,ultrasound machine zinapoharibika huwa zinapelekwa wapi kufanyiwa matengenezo?
Tafuta biomedical engineers wa kazi hizo, kwa baadhi ya vifaa kama xray za phillips huwa na mafundi wao, anyway kama unamiliki hosp au kifaa husika sio rahisi kujiuliza swali kama lako
 
Habari ndugu zangu kwa wale wanaofanya kazi kwenye vituo vya afya .je vifaa kama xray, ct scan ,ultrasound machine zinapoharibika huwa zinapelekwa wapi kufanyiwa matengenezo?

Inategemea na mambo yafuatayo:

A: Kama ni kifaa kipya chenye guarantee, na muda haujaisha basi ni jukumu la aliyekuuzia/agent au mtengenezaji wa kifaa husika.

B: Kama muda wa guarantee umeisha
Vituo vya afya vyenye uwezo huwa na kitengo cha Maintaince na Biomedical, ambapo matatizo yote hupelekwa kwenye kitengo hiki na kazi yake ni:

1: Kufanya Planned Preventative Maintenance(PPM).

2: Kufanya matengenezo madogo yaliyo ndani ya uwezo wa kitengo.

3: Kitengo kina majukumu la kumuita mtengenezaji kunapotokea ubovu ambao hawawezi kurekebisha.

4: Kuthibitisha kuwa kifaa hiki hakiwezi kuendelea na majukumu yake.

NB: Ukienda kwenye hospitali kubwa unaweza kupata watu wa kukupa mwelekeo, kama ni wao wafanye au kukuelekeza jinsi ya kuwapata wahusika zaidi.

Check na hawa pia:👇

Wauzaji wa vifaa tiba (medical equipment) Tanzania
 
Back
Top Bottom