UZUSHI Vidonge 'Fake' vinavyofonza maji vipo Tanzania, ni hatari kwa Afya

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Tujihadhari na Vidonge feki vinavyotoka nje ya nchi.

1713448101551.png


 
Tunachokijua
Kumekuwepo na video inayosamba mtandaoni ikibainisha uwepo wa dawa zilizotengenezwa China zenye 'label' ya panadol, na kwamba zimetengenezwa makusudi ili kumaliza watu wa Afrika kwani zikimiminiwa maji kidogo tu hufumuka na kuwa kubwa.

Pamoja na Mambo mengine, video hii inawatahadharisha watu kuwa makini kwani wanaweza kupata matatizo makubwa ya kiafya ikiwa watatumia dawa hii.

Ukweli wa madai haya Upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa madai haya ambayo pia yameletwa Jukwaani na Herbalist Dr MziziMkavu hayana ukweli.

Kinachoonekana kwenye video si vidonge vya Paracetamol (Panadol), bali ni Compressed Tablet Magic Napkin (Compressed Napkin/Towel Tablet), zinazotumika kwenye mambo mbalimbali ikiwemo usafi wa mwili kama ilivyo kwa taulo na vitambaa vya kawaida.

Hutengenezwa kwa kutumia fiber (Nyuzinyuzi) ambazo hupitishwa kwenye mgandamizo mkubwa, kisha huwekwa kwenye vifungashio ambayo mara nyingi hufanana na vile vinavyotumika kufungua dawa za kawaida. Tazama video hii.

Huongezeka ukubwa wake kwa kiwango kikubwa baada ya kufyonza kiwango kidogo cha maji na kinaweza kutumika katika shughuli za kawaida za usafi.

Mambo mengine yanayodokeza uzushi wa taarifa hii ni mtu aliyerekodi kutokuonesha Jina halisi la dawa kwenye kifungashio chake, hajataja dozi ya kidonge husika pamoja na kampuni inayozalisha dawa hiyo.

Machi 19, 2019, Chaneli ya Mtandao wa YouTube inayoitwa Wandani TV ilichapisha video hii ikiambatana na maneno 'Parnado fake zagundulika, embu jionee mwenyewe, ndiyo maana tunakufa kama nzige' ambapo hadi Aprili 16, 2024, ilikuwa imetazamwa mara 104.

Aidha, JamiiChek imebaini kuwa video nyingine ya aina hii iliwahi kuchapishwa Disemba 1, 2016 kwenye Mtandao wa facebook na Ukurasa unaoitwa Tumi Olugunwa International School.

Leso hizi ni rafiki wa Mazingira na Huharibika (Huoza) kirahisi takribani siku 45 baada ya Matumizi yake hivyo kutokuathiri Usafi wa Mazingira kwa Kiasi Kikubwa
Before yakuja forward na kuleta taharuki kwa jamii ebu tulia kwanza ufanye research kidogo.

Hizi tablets si panadol kama unavuaminisha watu.

Ni highly compressed napkins, ambazo ni rahisi kubebeka badala ya kutembea na kitamba, tissue paper.

au wipes.
Screenshot_20240415-081200_1.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom