Viashiria vitakavyoonesha tangazo lako halitafanya vizuri kwenye mitandao yako ya kijamii

Lazaro Samwel

Member
Apr 27, 2019
33
26
Inawezekana ukawa ni mfanyabiashara ambaye unaandika matangazo kila mara na unajikuta haupati matokeo mazuri.

Umelipa kwa watu mbalimbali kukuandikia matangazo lakini bado hakuna matokeo mazuri ambayo umeyaoata kwenye kuuza bidhaa zako.

Kama ni bidhaa hakuna unachouza au hakuna hata watu wanaoulizia unachokiuza basi kuna namna matangazo yako unayaandika kimakosa na unatakiwa kujirekebisha mapema ili uweze kufanya vizuri.

Kwanza kabisa inabidi uweze kuelewa unayataka kumuuzia bidhaa yako sio wewe bali ni mteja wako na njia rahisi ya kuweza kumuuzia ni kuweza kuizungumzia bidhaa yako katika utimizaji wa maono ya mteja ambayo kwa sasa imekuwa changamoto kuyatimiza.

Uandikaji wa matangazo ambao unaweza kukuletea matokeo mazuri ni ule ambao unaonesha unaelewa hali ya mteja wako lakini pia unaelewa ni kwa namna gani bidhaa yako au huduma yako inaenda kumfikisha mteja wako sehemu ambayo anatamani kufika lakini hajaweza kufika kwasababu ya changamoto ambazo ameshindwa kuzitatua mwenyewe.

Kikawaida ni kwamba mafanikio ya mauzo kupitia matangazo yako sokoni huwa yanatakiwa kufuata hatua 3 muhimu ;

1. Kuonesha uelewa wa hali ya sasa ya mteja,kwa lugha nyingine tunaweza kusema kujua tatizo la mteja wako na kuonesha unaelewa tatizo lake ili iweze kuwa rahisi kupata kibali cha kugusa hisia zake kwa wepesi.

2. Mpango mkakati baada ya kuweza kujua tatizo lake kwaajili ya kujenga uaminifu wako kwake kwamba unaweza kuwa msaada wa kumfikisha anapotaka kufika.

Tunasema ni lazima ufuate kanuni ya 4W katika kuandika hili kwa wepesi na mteja kukuona kwamba wewe ni mtaalamu kwa kile ambacho unataka kumsaidia.

3. Kesho yake anayotamani Kuifikia ili aweze kuona kwamba unaelewa kule anapotaka kufika. Wateja wananunua kesho inayoionesha kwao endapo watatumia bidhaa/huduma yako. Hakuna kingine tofauti na hapa,unapojenga picha nzuri ya kule wanapotamani kufika kwa matumizi ya bidhaa yako inakuwa ni rahisi zaidi kuamua kukupatia fedha zao lakini ukichemka hapa bado itakuwa ni ngumu sana kwa wao kuweza kutoa hela.

Lazima ujifunze kuandika hili katika matangazo yako tena kwa kueleweka bila kupindisha.

Hivi ni vitu vya msingi sana kuzingatia unapoandika tangazo lako na ikiwezekana hakikisha kila unapoandikq tangazo kabla ya kuweza kulisambaza unapitia kuangalia kama vitu hivi umevionesha kwa yule ambaye umemlenga.

Kwa kukazia zaidi,vitu ambavyo vinaweza kuonesha kwamba tangazo lako haliwezi kufanya vizuri utakapolipeleka sokoni ni kwamba tangazo lako ndani yake;

1. Umeweka kichwa cha habari ambacho hakioneshi kuna nini kwaajili ya mlengwa wako.

2. Unazungumza sana juu ya bidhaa/huduma yako na kumfanya mteja wako kuona kama bidhaa/huduma yako sio kwaajili yake au haimuhusu yeye tena.

3. Umetanguliza bei mwanzo kabla ya thamani ya bidhaa/yako na mwisho wa siku bei kuwa na thamani kubwa zaidi ya thamani ya bidhaa au huduma yako kwa mteja wako.

4. Kutokugusa hisia za mlengwa wako ipasavyo na kumfanya akuzingatia katika kufanya maamuzi ya haraka ya kununua bidhaa/huduma yako.

5. Kutokuonesha ni kwa namna gani bidhaa/huduma yako itamfikisha muhusika sehemu flani anayohitaji kufika kwenye maisha yake.

6. Kutumia maneno ambayo ni magumu kuweza kueleweka kwa mteja wako.Kwenye kuuza sio sehemu ya kuonesha umaridadi wako wa misamiati migumu au kutumia lugha ngumu kwa wateja wako.

Andika katika lugha nyepesi ma inayoeleweka kwa walengwa wako na utapata matokeo mazuri.

7. Kuwa na call to action ambayo haina ushawishi wowote kwa mteja wako. Ni vyema ukawa na call to action ambayo itamsukuma mtu kutaka huduma au bidhaa yako na sio kuandika tuu.

Types of call to action

1. Direct Call To Action.
2.Transitional Call To Action.

Fuatilia makala zangu utaona namna ninavyoandika.

etc

Kwa kifupi tangazo lako ukiona linakuwa na vitu hivi jua kabisa unajipotezea muda kwa watu wengi kuweza kununua bidhaa zako.

Zaidi utafaidika na watu waliopo kwenye kundi la 3% ambao wanajua wanachokihitaji hata kama usipowaeleza chochote na utakosa kundi la 97% ambalo lingeweza kuwa na faida kubwa sana kwenye biashara yako endapo ungelifanyia kazi vizuri kwa uandishi wako wa matangazo.

Leo niliona nikugusie baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kuanza kukufungua taratibu katika uandishi wako wa matangazo yako.

Hakikisha usiwe na haraka sana ya kuandika tangazo lako na kuanza kulisambaza tuu kwenye mitandao yako ya kijamii,andika tangazo lako lirudie tena kulisoma wewe mwenyewe,angalia linaonesha vitu hivyo vyote 3 ambavyo nimeelezea?

Kama hapana rudia tena upya na jitahidi kuweza kukidhi vigezo hivyo.

Ikiwa na wewe bado unahangaika katika kuandika matangazo ya kuuza bidhaa zako kwa urahisi na umefanya kila namna lakini bado haujawa vizuri basi nikukaribishe katika
madarasa ya AKILI YA USHINDI kujifunza zaidi na kushikwa mkono kuwa vizuri katika undishi huu wa matangazo ambao yanaweza kukusaidia kuuza kwa wepesi lakini kuingiza hela kwa kusaidia wengine kuuza bidhaa zao.

Njoo INBOX na unitumie namba yako ya simu.

Lazaro Samwel
Author | Sales And Marketing Expert | Professional Copywriter
#akiliyaushindi
 
Back
Top Bottom