Uwindaji wa Tembo Endulen Umedhoofisha Diplomasia na Kenya

Schengen

JF-Expert Member
Mar 24, 2024
253
425
Habari wadau!

Kuna jambo hili linalalamikiwa sana na Serikali ya Kenya kila kukicha serikali imeweka pamba masikioni. Kuna uwindaji wa Tembo wakutisha unafanyika Endulen (kwa wasiojua Endulen ni pori la wanyama lililoko mpakani kati ya Amboseli National park na Tanzania upande wa huko West Kilimanjaro njia ya Sanya juu), so Kwa Kenya ni National park kwa Tanzania ni pori lililoko chini ya WMA.

Sasa jamaa hawa wanaowinda kihalali huua wale Tembo wakumbwa sana wanaitwa Tusker Elephants kule Kenya so pindi wakivuka upande wa Tanzania hawarudi tena, ni bunduki zinalia full time. Kumbuka wanyama hawana border, serikali imepigiwa kelele lakini hakuna kinachosemwa.

Nilivyomuona Dotto juzi kule msibani ndio nilikumbuka hili jambo kuwa mambo si shwari sana. Sasa Rais Ulaya ameharibu, Marekani kote, na hili koloni la Marekani Africa mashariki naona mambo si shwari amebaki na ndugu zake Waarabu tu sasa!
 
Wazanzibari hupenda sana kuchuuza vitu walivyovikuta na hupenda kuwauzia waarabu kila kitu kuanzia nazi hadi tembo.
 
Kila mmoja adhibiti tembo wake. Kama tunawinda tembo wakiwa Tanzania basi ni tembo wetu na hasara yetu.

Kwa Mtanzania kuanza kuwatetea majirani zetu walafi wa kila kitu ni AIBU, au la mtoa mada utakuwa ni MAMLUKI wa wa -Kenya.

Wakenya wametuburuza kwenye kugawana mali za iliyokuwa East Africa Corporation mwaka 1977 ilipovunjika, Wakenya wanajitangazia kuwa Mlima Kilimanjaro uko kwao. Wakenya wamejenga mahoteli Masai Mara na wamezitumia WWF na taaasisi zingine za kimataifa kutuzuia tusijenge barabara ya lami Serengeti na mahoteli ili wao waendelee kupata wageni wote wanaotembelea Serengeti.

Sisi tutaendelea kuwinda tembo kwa kuwa ni njia moja wapo ya kupunguza idadi yao ambayo ni hatarishi kwa binadamu. Bado Tanzania ni nchi ya 3 kwa wingi wa tembo duniani ikiwa nyuma ya Botswana na Zimbabwe tu
Screenshot_20240430_072059_Google.jpg
 
View attachment 2977169Kwani maximum wanatakiwa idadi Yao Kwenye nchi wawe wangapi? Ili wakizidi wapinguzwe?
 
Nadhani NIMEELEWEKA si ndio Schengen

Hata nchi yetu iwe na matatizo gani, tutayatatua wenyewe. Ila kumbuka jirani yetu wa kaskazini siyo mwema
 
Back
Top Bottom