KWELI Uvutaji wa sigara huongeza nafasi ya kupatwa na Changamoto ya Upungufu wa Nguvu za Kiume

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo linalokabili wanaume wengi duniani. Kwa mujibu wa tafiti, tatizo hili linazidi kuwa kubwa miaka ya hivi karibuni tofauti na zamani.

01223CC3-371C-49F1-B07E-837E58A233FA.jpeg

Katika kutafuta visababishi vyake, Mdau mmoja wa JamiiForums aliweka chapisho lake lenye utafiti unaotaja sigara kuwa miongoni mwa mambo yanayofanya tatizo hili litokee.

Ni kweli kuwa sigara inaweza kusababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume?
 
Tunachokijua
Upungufu wa nguvu za kiume kwa kiswahili hutafsiriwa kwa namna nyingi, lakini maana sahihi ya hali hii ambayo kwa lugha ya Kitaalam huitwa Electile Dysfunction ni kukosekana au kupungua kwa uwezo wa mwanamme kwenye kusimamisha uume wake kiasi cha kutosha kuhimili ushiriki wa tendo la ndoa kikamilifu. Hii ni kwa mujibu wa NIH consensus Conference, 1993

Mwitikio wa kihisia unaochochea kusimama kwa uume hutegemea kwa kiasi kikubwa mfumo wa mzunguko wa damu mwilini hivyo magonjwa kama kisukari na Shinikizo kubwa la damu pamoja na hali zingine zinazoathiri mfumo wa damu na moyo hutajwa kama mojawapo ya sababu zinazopelekea kutokea kwa changamoto hii.

Tafiti za kisayansi zimeweka bayana kuwa uvutaji wa Sigara huathiri utendaji kazi wa kemikali za Nitric Oxide (NO) ambazo hupanua mishipa ya damu ya uume na kuongeza msukumo wa damu ili uume uweze kusimama kikamilifu.

Aidha, kemikali za sigara huharibu corpora cavernosa, tishu za uume zinazobeba sehemu kubwa ya mishipa ya fahamu inayoruhusu kutanuka kwa kichwa cha uume ili kuwezesha mzunguko mkubwa wa damu pamoja na kuongeza msisimko wa kihisia ambavyo kwa pamoja huufanya uume usimame kwa nguvu.

Hivyo, JamiiForums imebaini ukweli kuwa uvutaji wa sigara ni mojawapo ya sababu zinazochangia kutokea kwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Hata hivyo, ni muhimu kuweka sawa mambo yafuatayo-
  1. Ukubwa wa tatizo hutegemea na wingi wa dozi (idadi ya sigara) anazotumia mhusika
  2. Wanaovuta wapo kwenye hatari kubwa zaidi kuliko wale wasiovuta
  3. Tatizo linaweza kurekebishika baada ya muda fulani hasa kwa vijana ikiwa mhusika atasitisha uvutaji wa sigara
  4. Wazee wanaovuta sigara huathirika zaidi kuliko vijana
Pamoja na madhara haya ya kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, American Lung Association wanabainisha uwepo wa zaidi ya viambato 600 kwenye sigara ambavyo huzalisha kemikali tofauti zaidi ya 7000 vinapounguzwa, ambapo kemikali 69 kati yake zimethibitishwa kuwa na uwezo wa kusababisha aina mbalimbali za saratani mwilini.
Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo linalokabili wanaume wengi duniani. Kwa mujibu wa tafiti, tatizo hili linazidi kuwa kubwa miaka ya hivi karibuni tofauti na zamani.


Katika kutafuta visababishi vyake, Mdau mmoja wa JamiiForums.com aliweka chapisho lake lenye utafiti unaotaja sigara kuwa miongoni mwa mambo yanayofanya tatizo hili litokee.

Ni kweli kuwa sigara inaweza kusababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume?
Kama ni kweli mbona hao wamarikani ndiyo wavutaji na wauzaji wa hii kitu bila kusahau mabwimbwi? Hata bangi walisema ni mbaya lakini hawaachi kuipepa
 
Acheni kutisha watu mm navuta huu ni mwaka wa 23 na mzigo napiga fresh kabisa,,, unaposema upungufu wa nguvu za kiume sio kusimamisha au kufanya kwa muda mrefu tu, bali pia mbegu zako ziwe na uwezo wa kurutubisha yai. maana kuna mtu anafanya masaaa mawili ila mbegu zake hazimsaidii chochote yanatoka tu maji maji ama mapovu. Mimi napiga fresh kabisa na wala hakuna siku hata moja eti nimeshindwa kwa sababu yoyote
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom