usiku wa leo utaamua Tanzania inakwenda wapi..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,489
40,018
Jua litakapotua na Giza litakapoingia...mwelekeo wa Tanzania utaamuliwa leo. Natumaini wapo watu ambao watasimama pamoja kupinga. Watu wema wa tanzania wapo wapi? Utafika wakati wale wenye kuamin katika udugu na umoja watoke na kusimama pamoja. Wasikubali kuiachia nchi ivurugwe hivi kwa uzembe wa wawatawala. Sijui usiku hu utapitaje..I dread the thought
 
Tatizo ni kwamba, kadiri center of gravity inavyozidi kwenda chini, ndio uwezekano wa muanguko unavyozidi.

Sasa hivi watu walivyojichokea kutokana na kukosa matumaini, hawajali umewaletea jambo la maana au la kipuuzi, wengi wakipata nafasi ya kuwarushia mawe polisi na kufanya fujo watafanya tu.

Serikali imeweka mazingira ya vurugu tayari kwa kuwaacha wananchi waishi bila matumaini, na hivyo kuwafanya wawe susceptible kwa makuwadi wa umwagaji damu wanaojifunika mwamvuli wa dini.
 
Labda JK anaweza kumuomba Mwamunyange ashikilie Nchi kwa Muda? ili kupunguza hi sintofahamu
 
Nchi ipo katika ombwe la uongozi,.. kiongozi mkuu bado ni kijana mtalii,mwenye kuhusudu starehe na anasa za kidunia.
Paka aliefungwa kengele sasa ataamsha na kuwakumbusha watanganyika nini walichonyimwa chini ya kivuli fake hichi cha amani, huku jamii flani ikionewa,.. kama mkristo nakiri tumevumilia mengi, tumeonewa vya kutosha,tumelazimishwa wakati mwingine kukubali hata yale yanayoonekana si haki
Ikumbukwe Raisi Mkapa alipowaruhusu waislamu watumie majengo ya Umma pale morogoro kufanya chuo chao, haikumaanisha mkristo asiruhusiwe ama akiruhusiwa pale atendewe kama mkimbizi
 
Mi najiuliza hatma yake ni nini? najua leo watatawanywa, tar 1 nov kesi itakapotajwa tena mambo yatakuwa hayahaya kwahiyo kila siku tukimbie ofisi zetu kuwaogopa hawa jamaa wkt kuna watu tunawalipa watulinde? walizembea mwanzo sasa wakaze uzi
 
Kumbe hali ni tete hivyo? Nyinyi watawala tuliyowapa dhamana mmeshindwa? Tuanze kuhamisha familia zetu vijijini ana nchi?
 
Kwa kweli haijakaa sawa maana ni wasiwasi tele miongoni mwa raia.
Hawaelewi usalama wao uko wapi.
Na wanaposikia walinzi wa raia na mali wanauliwa ndio wanachanganyikiwa zaidi.

Eh mungu pisha mbali!
 
mkuu nchi itatulia inatakiwa mtu wa kuwakalisha hao waumini na watoe ya moyoni kwasababu kwa sasa hawana imani na bakwata atafutwe muumini atoke shia ,au wapi watakaa chini watasikiliza .watu wako frustrated na maisha magumu wanapopata nafasi ya kupunguza stress yuko tayari ajitoe mhanga kama tunavyoona sasa .hawa watu ni wamoja lakini kila mtu ana kwake hawakai wote msikitini .wakae nao watu wachache wazee wenye busara ,hekima ,maarifa tatizo litakwisha .Lakini nguvu ikitumika sana itakuwa si busara pia itaweka makovu hawatasahau watapumzika siku nyingine wanalianzisha .
 
Kikwete anafurahishwa sana na hii hali,kama mtawala makini wkt hali ikiwa tete alitakiwa kukaa na kutatua matatizo ndani ya nchi yake lakini anadhurura hovyo hovyo sijapata ona rais punguani kama huyu.
 
Back
Top Bottom