Usije ukajidanganya na hii kauli ya "Age is just a number"

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,641
52,456
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Sio vibaya kujipa moyo Kwa MTU ambaye bado mambo yake yamemuendea mrama, yamemuendea kombo. Kauli hiyo hutumiwa kuwa-motivate Watu ambao wapo katika Zone ya hatari au katika hali ya kuchelewa.

Kanuni kuu ya Maisha katika masuala ya muda ni kuwa "Kila Jambo linawakati wake" hiyo ndio Kanuni kuu katika masuala ya muda.

Kila kitu unachokiona hapa Duniani kina Wakati na muda wake. Kila kitu kina umri wake. Maisha yako limited Kwa sababu ya Muda, muda ndio huamua na kutoa majibu.

Age/umri ni sehemu ya muda/Wakati WA kiumbe au MTU tangu alipozaliwa mpaka pale alipo. Usije ukajichanganya kuwa umri hauna lakufanya katika Maisha yako Kwa kujidanganya kuwa umri ni namba tuu na sio zaidi ya hapo.

Ukashindwa kufanya mambo ya muhimu na yalazima kwaajili yako na KESHO yako. Ingawaje hatulijui kesho yetu lakini kutokuijua kesho yetu ndio kunatufanya tujidhatiti na kujiandaa Kwa kujiwekea Akiba na udhibiti mzuri ili kupambana Kwa ajili ya kuishi vizuri siku zijazo.

Kila nafasi unayoipata kwenye maisha yako ni nyeti, muhimu na yalazima kutumiwa Kwa hesabu Kali zenye kuzalisha, Fikra za kujihami, kujidhatiti huku ukiendelea kufurahia Maisha yako ya Leo ni muhimu Sana.

"Age is not just a number but is more than a numbers," hivyo ndivyo naweza kusema.

Unaweza kuwa katika mapito yako ukawa katika mkondo wa matatizo, au ukawa katik njia inayokupatia mapato madogo, hiyo isikufanye ukate tamaa, uone unapoteza muda, sio kweli.

Muda unapotezwa pale unaposhindwa kukitumia na kukizalisha hata kile kidogo ulicho nacho. Mfano unapata 3000 Kwa Siku. Hapo sio Kwamba umekwama, Nop! Bali Maisha yako yapo katika mkondo huo, attitude yako ndio itaamua ujione upo katika Maisha ya namna ipi.

Hiyo elfu tatu uliyoipata kwenye matumizi ndio itaonyeshe jinsi ulivyo. Kwema Maisha hakuna kitu kidogo, Bali kuna Bad attitude na Good Attitude.

Katika Life Cycle, kuanzia ukiwa mtoto, kijana, MTU mzima mpaka Mzee. Zipo sababu za mabadiliko ya kimwili, Kiakili, Kiroho na kihisia unayoyaona katika Mwili wako. Na hayo yote yanapo Chini ya udhibiti WA muda.

Ukiwa kijana unakuwa na nguvu, Akili nyepesi yenye kufikiri kwa baraka, shauku, ndoto na hatakati za hapa na pale. Huo ni umri wa mapambano, umri wa kukusanya n kujijenga. Kamwe usisubiri MTU akufanyie Maisha. Wewe sio mtoto.

Ulipokuwa mtoto wazazi wako ndio walikuwa na wajibu wa kukufanyia Maisha. Umeshakuwa kijana miaka wa 20+ ni Wakati wako sasa. Inashangaza kijana anamiaka 25 anasubiri kutafutiwa kazi, au anampa MTU mwingine majukumu ya kukutafutia alafu wewe umekaa tuu nyumbani.

Sio vibaya kutafutiwa kazi ila hakuna Jambo Baya kama kutegemea kutafutiwa kazi. Nakuhakikishia Hakuna MTU wa kukufanyia hiyo kazi Kwa weledi kama ungefanya wewe mwenyewe.

Asije akakudanganya MTU kuwa unaweza ukafanikiwa hata ukiwa na umri wa miaka 45 Huko. Sio kweli. Hapo unaongelea Watu Exceptional, yaani Watu wenye bahati. Umri wa kutafuta mafanikio unafahamika, ni umri wa mapambano kuanzia miaka 18- 40 hapo ni umri wa kupasuana.

Huo sio umri wa kuwa na busara, Kam unabusara zihifadhi utazitumia ukiwa Mzee. Huo ni umri wa kuwa na Courage(ujasiri), Focus(shabaha sio unayumbayumba, Utulivu), Patience(subira au uvumilivu, Utulivu), Passion (Shauku, hamu, mchecheto wa kujipa Maisha Bora). Justice (Haki).

Elewa kuwa kuna umri Akili yako unayoiona itaanza kupungua na kuleta. Udhaifu WA hapa na pale.
Elewa kuwa kuna umri na wala haupo mbali baadhi ya viungo vya mwili vitapungua ufanisi katika ufanyaji wa KAZI.

Elewa kuwa kuna umri hata Watu hawatakuwa wanakuhitaji unapoenda kuomba kazi watakuwa wanahitaji Vijana wapya wenye mawazo Mapya na nguvu Mpya, wewe utakuwa umeshachakaa kimwili na Kiakili.

Usije ukadanganywa na Akili zako kuwa uwezo ulionao ndio utakuwa hivyohivyo, huo uwezo wako utaitwa uwezo wa kizamani uliopitwa na Wakati, hizo nguvu zako zitaitwa nguvu za kizamani zilizopitwa na Wakati. Hayo mawazo yako unayoyaona ni bora na huenda Watu wanakusifu nayo sio muda yataitwa mawazo ya kizamani.

Mchezo huo utaanzia ndani ya familia yako. Watoto uliowazaa usijesema watakuwa wakubwa mno, nop! Ni vitoto tuu ulivyovizaa ambavyo haya miaka 20 haviijui lakini vitakuambia umepitwa na Wakati. Na Hii ni kama hutokuwa mwerevu WA kuelewa kuwa "Age is not just a number but is more than a Number"

Usishangae ni Kwa nini wazee unaopishana nao wanakaa kimya alafu ukawa unawatambishia na kuwaona wanaakili za kizamani, hizo Akili za kizamani unazoziona pengine ndizo ziliwafanya waheshimike😀😀.

Usiwaone ni wapole hawataki majibishano, ukawaona wanabusara, Dio wanabusara Kwa sababu wametambua kuwa Wakati ni ukuta. Hawaamini kama wao ndio wamekuwa kama Mbwa aliyeingiza mkia kwenye miguu.

Hapo watakachokuambia Subiri nawe utaona, Kuwa uyaone. Sio kwamba wanakutisha ila wanakupa greenlight alert Kabla hujakutana na Redlight alert.

Taikon nimeandika hapa sio kwaajili ya kumtisha yeyote. Isipokuwa ni kwaajili ya Kukutaka ewe kijana kutokusubiri, unasubiri nini, kutokujipa visingizio, Ooh! Mara serikali ya kipuuzi, ooh! Mara Ndugu hawanisaidii, ooh! Mara sina connection.

Fanya kilichombele yako ambacho kinaweza kukusaidia Kwa muda huo. Kifanye Kwa Moyo wote. Usichelewe. Umri ni Wakati. Na Wakati ni ukuta. Epuka kusema ningejua ningefanya. Haya Maisha yapo kwaajili yako mwenyewe.

Taikon nimemaliza, Leo sina maswali. Siongei kama Motivesheni Spika hapa. Naongea Kwa uzoefu Kabisa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
40 something watapita tu huu uzi na hawata comment chochote.
 
Mwaka huu mwisho kukaa kwa shemeji miaka 38 ....Taikuni ameamua kunitukana kwa Mara nyingine
 
Back
Top Bottom