stickvibration
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 3,227
- 5,133
Bila ya kuchelewesha muda Wana JF wenzangu, nirejee katika mada kwa yaliyonikuta, nikiwa safarini kutokea Dodoma kuelekea Mwanza na Ally's Star Bus.
Ilikuwa ni alfajiri ya saa12 asubuhi tulipoanza safari yetu, nikiwa nimekaa kwenye seat yangu ilikuwa ni namba moja (Extra One).
Baaada ya kupita Manyoni nikaona Simu yangu Ina chaji kama asilimia 38 nikachomoa waya wangu wa chaji na nikachomeka kwenye USB chaji iliopo pembezoni mwa kiti changu, yaani ile naiweka tu waya katika simu, yangu papo hapo simu ikazima ghafla.
Nilikosa raha kabisa nikachanganyikiwa kabisa yaani sijui nifanyaje, na aina ya Simu yangu ilikuwa ni iPhone 8.
Nikavuta subra hadi tulipofika Singida, wakati abiria wenzangu wanashuka kula Mimi nikawahi moja kwa moja soket ya umeme ili nione labda simu itawaka kwa kuchajia umeme wa kawaida, lakini Simu ikawa imezima tu.
Palepale nilimfata dereva na kumuelezea uhalisia ulivokuwa jibu nililopewa ni "Mkuu samahani tulisahau kukwambia kuwa hio seat yako namba 1, ina shoti kwenye charging system yake".
Mhhh, nguvu ziliniishia ukizingatia hapo nlikuwa sina pesa cash mfukoni hela yote ilikuwa ndani ya Mpesa katika Simu yangu.
Napenda kuwashauri Wana JF wenzangu kuweni makini sana na hizi chaji za kwenye mabus, hususan haya mabus ya Ally's Star yaendayo mikoani.
Sent using Jamii Forums mobile app