Elections 2015 Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,657
113,883
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa watu tulijibainisha humu kumuunga mkono kwa dhati, Mwamba wa Kaskazini, Edward Ngoyai Lowassa, na tukaahidi humu akiondolewa kwa mizengwe, hatuta kubali, patachimbika.

Kilichotokea ni kweli Edward Ngoyai Lowassa aliondolewa kwa mizegwe, sasa wakati tunatafakari tumchagize ahame pachimbike au tumtulize akubali matokeo ya kukatwa kwake kwa mizengwe, nimeona nitoe ushauri wa bure kwake.

Najua kuna wengi wanashanga kukatwa kwa Lowassa lakini kama wangeosoma uzi huu kabla, wala wasinge shangaa!.
Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!


Baada ya kuibuka jina la Dr. John Joseph Pombe Magufuli, kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM, kuna watu wanadhani jina hili la John Pombe Joseph Magufuli limejiibukia tuu from nowhere!, No way!, this was a calculated move, tena ni pre meditated siku nyingi nyuma kuwa mgombea wa CCM kwa uchaguzi wa 2015 ni lazima awe ni John Pombe Magufuli Kwa sababu fulani ambazo nimezitaja hapa... Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John

Kwa vile Lowassa ndie kipenzi cha watu, na wengi waliitegemea CCM itimize mapenzi ya wengi, mapenzi ya watu, lakini CCM wakaamua kutanguliza mbele maslahi mapana zaidi ya taifa, kwa kuwaweka pembeni 'the giants', wengi wa wafuasi wa Lowassa wamekuwa taken by surprise na wengine hata ku despaire, lakini laiti wangeusoma uzi huu, Edward Lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe Rais wetu wasingekuwa surprized!.

Maadam sasa uteuzi wa CCM umemalizika, na mgombea wa CCM ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, natoa wito na ushauri wa bure kwa Mhe. Edward Lowassa, kwanza ayakubali matokeo hayo ya uteuzi wa CCM, pili avunje kambi yake au ile team yake, na tatu ayarudishe nyumbani majeshi yake na kujisalimisha rasmi kwenye chama kwa kumsupport mgombea rasmi wa CCM!.

Kama mgombea angekuwa ni Membe, tungependekeza mapambano yaendelee kwa Lowassa kujitoa CCM na kuvuka upande wa pili, nasi tumuingize ikulu!, lakini huyu aliyepitishwa, John Pombe Magufuli, japo ni dikiteta, lakini pia ni jembe la ukweli, hivyo Lowassa hata akiamua ku cross, ataisaidia tuu kambi ya upinzani kuongeza nguvu na kupata wabunge wengi, na yeye kwenye urais ataweza kuvuna kura za kutosha haswa za Kanda ya Kaskazini na maeneo ya majiji na mijini lakini hawezi kupata kura za kutosha kuwa rais wetu, Kwa sababu determinant ya ushindani was urais was Tanzania ni Kura za Kanda ya Ziwa, hivyo Lowassa aki cross upande was pili na kugombea na Magufuli, yeye kama yeye atainyanyua Chadema lakini ataishia kupata kipigo kingine, yaani double tragedy !.

Kwa vile Lowassa ni chaguo la watu, na ni sisi watu tulio mchagiza kuwa 2015, ikulu ni yake, kwa ahadi hata asiposimamishwa na CCM, then asimame nje ya CCM tumpeleke ikulu, lakini kwa vile aliepita ni Magufuli, japo ni dikiteta lakini ni jembe la ukweli, Watanzania watachagua jembe, hivyo hakuna sababu kwa Lowassa kuendeleza mapambano maana huu sasa utakuwa ni mpambano wa mafahali wawili, ziumiazo zitakuwa ni nyika Kwa kuwagawa Watanzania katika kambi mbili!

Lowassa tulikupenda, ila CCM imempenda zaidi Magufuli, teremsha silaha chini, kubali kushindwa, rudisha nyuma majeshi, jisalimishe!.

NB: Hii sio mara ya kwanza kwa mimi kutoa ushauri wa bure kwa Lowassa, huko nyuma niliwahi kumshauri, Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.

matokeo yake tunayajua, na huu ni ushauri tuu.

Paskali
 
Vyovyote mtavyosema team lowasa lakini mmepewa kipigo cha mwaka.... Kikwete mliyemdaharau sana kawatandika 2010 na sasa pamoja na kuapa kwenu kuwa nje ya Lowasa lazima pachimbike lakini hakujachimbika na hata vichimbio hatujaviona! Leteni visingizio vyote na kujipendekeza kwa magufuli lakini mmechapwa kisawasawa na sasa ujanja hamna.....
 
Hata kama angeshinda Membe,Lowasa asingehama chama. Kwanza,kulinda maslahi yake,maana CCM ni chama cha wafanyabiashara. Pili,kulinda historia yake ndani ya chama. Tatu,historia yake, anaijua kama ni mbaya ama nzuri. Nne,kuandamwa na vyombo vya dola mara tu atakapokuwa nje ya mfumo wa chama. Hawezi kamwe. Wachafu hawawezi kuhama ccm,makongoro alisema chama kimejaa vibaka alimaanisha.
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa watu tuliomuunga mkono kwa dhati, mwamba wa Kaskazini, Edward Ngoyai Lowassa, na tukaahidi humu akiondolewa kwa mizengwe, hatuta kubali, patachimbika. Kilichotokea ni kweli Edward Lowassa aliondolewa kwa mizegwe. Kuna watu humu hawakuuona uzi huu,
[h=3]Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC![/h]hivyo Lowassa alipokatwa walishangaa, kama wangeosoma uzi huu kabla, wasinge shangaa!.

Baada ya kuibuka jina John Pombe Magufuli, kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM, kuna watu wanadhani amejiibukia tuu from nowhere!, No!. Na kuna wanadhani ameibuka surprisingly!, no!. Kama wangeusoma uzi huu,
[h=3]Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John[/h]angalau wangeelewa ni Magufuli!.

Kwa vile Lowassa ndie kipenzi cha watu, na wengi waliitegemea CCM itimize mapenzi ya watu, lakini CCM wakaamua kutanguliza mbele maslahi mapana zaidi ya taifa, kwa kuwaweke pembeni 'the giants', wengi wa wafuasi wa Lowassa wamekuwa take by surprise na wengine hata kuwa despaired, lakini laiti wangeusoma uzi huu,
[h=3]Edward Lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe Rais wetu [/h]wasingekuwa surprized!.

Maadam sasa uchaguzi wa CCM umemalizika, na mgombea wa CCM ni Dr. John Pombe Magufuli, natoa wito na ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa, ayakubali matokeo, avunje kambi yake au ile team yake, ayarudishe nyumba majeshi yake na kujisalimisha rasmi kwenye chama kwa kumsupport mgombea rasmi wa CCM!.

Kama mgombea angekuwa ni Membe, tungependekeza mapambano yaendelee kwa Lowassa kuvuka upande wa pili, nasi tumuingize ikulu!, lakini huyu aliyepitishwa, John Pombe Magufuli, pia ni jembe la ukweli, hivyo Lowassa hata akiamua ku cross, ataishia kupata kipigo kingine, yaani double tragedy !.

Kwa vile Lowassa ni chaguo la watu, na ni sisi watu tulio mchagiza kuwa 2015, ikulu ni yake, kwa ahadi hata asiposimamishwa na CCM, then asimame nje ya CCM tumpeleke ikulu, lakini kwa vile alipita ni Magufuli, ambaye na yeye ni jembe la ukweli, hakuna tena sababu kwa Lowassa kuendeleza mapambano maana huu sasa utakuwa ni mpambano wa mafahali, ziumiazo zitakuwa ni nyika!.

Lowassa tulikupenda, ila CCM imempenda zaidi Magufuli, teremsha silaha chini, kubali kushindwa, rudisha nyuma majeshi, jisalimishe!.

NB: Hii sio mara ya kwanza kwa mimi kutoa ushauri wa bure kwa Lowassa, huko nyuma niliwahi kumshauri,
[h=3]Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.[/h]matokeo yake tunayajua, na huu ni ushauri tuu.

Pasco
 
JK kawatandika huku akiwachekea...... penda msipende lazima mjipendekeze kwa Magufuli.....mtafanya nini sasa?.....oooh akikatwa patachimbika...... hahaha....hata vichimbio hata hatujaviona.....kichapo cha mbwa mwizi....kwi..kwi...kwi..... kifuatacho ITV ni kupeana faraja mbuzi tu......hela watu washatafuna sana tu....
 
Hapa pia pana mengi mno ya kuyanyambua !

Mkuu Pasco pole kwa kuunga mkono japo ulifahamu litalokupateni na saahib wako bwana Edward N Lowasa !

Ahsanta kwa kukutana baada ya muda mrefu !?

Sasa shughuli imekamilika na yafuatayo/ifuatayo ni uondoshi wa madhaifu ndani kama 'unafiki' taekwa pembeni !

Shukraan !
 
Watu wamepiga pesa buanaaa,,vijana wengi ,wanavyuo matarajio yao yameeishia stand ya bus!,watarudi kundini tuu(ukawa)
 
Maskini Mamvi....wajumbe woooote wanaimba na kucheza mkutanoni....washasahau zile chambichambi......sasa ule msemo wake wa kuhuzunika pamoja na kufurahi pamoja umekuwa kinyume kabisa...... anahuzunika peke yake wajumbe wanafurahi peke yao.....siasa hizi nouma kweli.....
 
Maskini Mamvi....wajumbe woooote wanaimba na kucheza mkutanoni....washasahau zile chambichambi......sasa ule msemo wake wa kuhuzunika pamoja na kufurahi pamoja umekuwa kinyume kabisa...... anahuzunika peke yake wajumbe wanafurahi peke yao.....siasa hizi nouma kweli.....

Mkuu Pasco anacheza na ''kuwa mwanasiasa nje ya mfumo wa CCM nini''. Hapo ndipo utakapojua kweli Dr Slaa, Lipumba and co ni alfa na Omega. Lowassa hana guts za kutoka CCM hata kidogo. Hana lolote la kujivunia na hana ushawishi wa aina yoyote. Waliweza kum-black mail Mkapa ile 2005 akafikiria na hapa ataweza.
 
Wewe ni mnafki mkubwa kuwahi kutokeo Ulimwenguni..

Sasa kama uliyajua matokeo kwamba hawezi kupitishwa kwanini mliendelea kumlia pesa zake..

Nilishawahi kukuitaga mjinga humu na wala sijutii..
 
Lowsa alikua wapenzi ya makundi maslahu , hakuwahi kuwa kipenzi cha wengi. Hakupendwa na watu makini wenye kumfahamu wenye uchu wa kuona uchafu wa rushwa na wizi ndani serikali unaondoka .
Aliwakumbatia matajiri ambao wamegubikwa na rushwa. Angechaguliwa rushwa na wizi ungeongezeka zaidi, na pia upande wa diplomasia si hashha angetuingiza kwenye vita na majirani pia...sio mtu mwenye busara wala siasa haijui.
Nasisittiza wajerumani walimchagua kwa wingi hitler na walikuja kujuta ...kilichowatokea mnakifahamu...kupendwa sio hoja ...nia yake haikuwa mzuri....angetupa tabu.

Ama kwa ushauri bora amfuate tu Malecelela, Msuya na Salim Ahmed ....wamepimzika wanakuwa washauri wa chama chao
 
Back
Top Bottom