guojr
Member
- Dec 4, 2015
- 56
- 82
Habari za wakati huu wadau wa maendeleo, leo nimekuja tena kuangazia namna TRA inaweza kuchukua hatua ili iweze kuongeza ukusanyaji wa mapato nchini. Kama tunavyojua kodi ndio inayotumika kufanya maendeleo na kugharamia shughuli za kila siku za serikali, lakini TRA inashindwa kukusanya mapato ya kutosha licha ya nchi kuwa na idadi kubwa ya biashara na watu.
Kwakuweka rekodi sawa, mimi sio mtaalam wa uchumi bali ni mtazamo na mchango wangu katika kusaidia mawazo. Nimeandika makala kadhaa moja ikiwahusu TRA iliyonifanya nishinde shindano la SoC2021, hivyo basi huu ni muendelezo wa makala zangu.
TRA INAKABILIWA NA CHANGAMOTO HIZI
1. Wafanyabiashara kutotaka kutumia mashine za EFD na kutoa risiti halali za malipo.
Kwa uelewa wangu, moja ya sababu nilizozisikia ni wafanyabiashara kulalamika kuwa gharama za EFD Machine kuwa kubwa, lakini hapohapo utashangaa kwa wenye nazo hutoa visingizio mbalimbali ili tu wasikupe risiti au wapo radhi wapunguze bei kwenye bidhaa au huduma husika. Hivyo basi sababu ya gharama ya mashine ya EFD inaoesha wazi sio sababu ya msingi bali kuna kitu kingine ambacho wafanyabiashara wanakikwepa.
2. Wananchi kutotilia maanani kudai risiti halali wakati wa manunuzi ya huduma au bidhaa.
Kwa updande wa wananchi kupuuzia kudai risiti halali ya malipo yaliyofanyika sijajua changamoto ni nini au labda hawana sababu ya kuchukua kwakua achukue au asichue hakuna utofauti. ila wananchi wenzangu kutodai risiti kunaikosesha serekali mapato.
TRA NA SEREKALI IAMUE KUFANYA HIVI ILI KUONGEZA MAPATO
1. Serekali iamue kutengeneza mfumo wa tehama utakao unganisha taarifa za wananchi na wafanyabiashara na ufanyekazi kama ifuatavyo.
Mwanachi atakapoenda kununua bidhaa au huduma, mfanyabiashara atatumia mfumo nilioutaja hapo juu kupita App ya TRA kuingiza manunuzi husika na risiti itatumwa kwanjia ya ujumbe mfupi wa maneno. Mfumo utamrudishia mwananchi 1% ya kodi(VAT) aliyotozwa kwenye manunuzi husika. Njia hii itawafanya wananchi wapendelee kudai risiti kwasababu wanajua watarudishiwa 1% ya kodi aliyochangia na hatimae kuifanya serekali kuongeza mapato. Najua kutakua na mswali mengi, nimeshindwa kuelezea kilakitu jinsi mfumo utakavyofanyakazi hivyo nitajibu maswali kadiri nitakavyoweza.
2. Elimu kwa walipa kodi hasa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno au sponsored Ads. Sikumbuki kama niliwahi kutumiwa ujumbe na TRA wa kunisisitiza kudai risiti ninapofanya manunuzi kama taasisi nyingine zinavyofanya kama TCRA au POLISI huwa wanatuma sana SMS.
3.Kuacha kutumia hardware za EFD bali kutumike Web au Mobile App au ikiwezekana USSD kukamilisha manunuzi na mnunuaji kutumiwa ujumbe papohapo wa risiti halali.
Hivyo basi wananchi wenzangu tuendelee kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu, tusisubiri kufadhiliwa na mataifa mengine au serekali kukopa fedha.
Naomba kuwasilisha hoja sasa.