Ushauri kwa watu wote walioajiriwa

Tupe mchanganua wa kujenga kwa laki tano!!!

Chakula asubuhi mchana na usiku sio chini ya 10,000 X 30

300,000

Nauli 3000 X 25

75,000

Chumba single 60,000

Vocha 30,000

Maji, umeme, dawa ya meno sabuni na takataka nyingine 50,000

Hapo hujavaa, hujaonga , sadaka kama uko na wadogo au wategemezi.

Kwa laki tano ukijenga wewe ni mtenda miujiza zaidi ya mchungaji kiboko ya wachawi
Screenshot_20220926-051210_WhatsAppBusiness.jpg
 
hupo serious ndio maana
Unakula 10,000 kwa siku
unaweka vocha 30,000
unaishi chumba cha elf 60
maji na umeme unatumia 50,000

Unaposikia mafanikio usihisi ni lele mama.
Behind any successful person there is terrible story.
Acha polojo. Weka mchanganuo.

Chakula cha elfu 10 ni kama ifuatavyo

Chai 2000
Mchana 3,000 + 1000 ya maji ya kunywa
Usiku 3000 + Juice
Weka budget avheni ushuhuda wa walokole
 
Acha polojo. Weka mchanganuo.

Chakula cha elfu 10 ni kama ifuatavyo

Chai 2000
Mchana 3,000 + 1000 ya maji ya kunywa
Usiku 3000 + Juice Weka budget avheni ushuhuda wa walokole
Mzee hio chai ya 2000 una kula bomu??, kwani lazima ule milo 3.

hapo mchana + usiku, hiyo juice tupa kule.
Na mchana ni 2000 tu,
 
Tupe mchanganua wa kujenga kwa laki tano!!!

Chakula asubuhi mchana na usiku sio chini ya 10,000 X 30

300,000

Nauli 3000 X 25

75,000

Chumba single 60,000

Vocha 30,000

Maji, umeme, dawa ya meno sabuni na takataka nyingine 50,000

Hapo hujavaa, hujaonga , sadaka kama uko na wadogo au wategemezi.

Kwa laki tano ukijenga wewe ni mtenda miujiza zaidi ya mchungaji kiboko ya wachawi
Unamaanisha wote waliojenga wana mishahara ya milioni na kuendelea au unatania boss?
 
Hapo hujavaa, hujaonga , sadaka kama uko na wadogo au wategemezi.
Na hapo hujalipia choo ukiwa mjini mihangaikoni
Hujahudumia Khadija (mtarajiwa)
Hujasafiri kwenda kwenye msiba kijijini
Hujamnunulia mzazi sukari na mafuta ya taa
Hujachangia mambo ya kijamii mtaani kwako
 
Ila waTanzania tunajijua kila mtu na siri yake namna anavyoishi
Unakuta mtu analipwa 500K
  1. Anavaa
  2. Anakula
  3. Analipa nauli
  4. Anasomesha
  5. Analipa kodi ya nyumba
  6. Anajenga
  7. Anahonga
  8. Anafungua kibiashara
  9. Anashiriki vikao vya kuzungusha kama tulivyo
  10. Simu haipungui kifurushi
 
Tupe mchanganua wa kujenga kwa laki tano!!!

Chakula asubuhi mchana na usiku sio chini ya 10,000 X 30

300,000

Nauli 3000 X 25

75,000

Chumba single 60,000

Vocha 30,000

Maji, umeme, dawa ya meno sabuni na takataka nyingine 50,000

Hapo hujavaa, hujaonga , sadaka kama uko na wadogo au wategemezi.

Kwa laki tano ukijenga wewe ni mtenda miujiza zaidi ya mchungaji kiboko ya wachawi
1713919033099.png
 
1. Jenga nyumba mapema. Iwe kijijini kwenu au mjini. Kujenga nyumba ukiwa na miaka 50 sio mafanikio. Usizoee nyumba za serikali. Faraja hii ni hatari sana. Hebu familia yako yote iwe na wakati mzuri ktk nyumba yako mwenyewe.

2. Nenda nyumbani. Usiishie kazini mwaka mzima. Wewe si nguzo ya idara yako. Ikiwa utakufa leo, nafasi yako atapewa mwingine bila kuchelewa na shughuli zitaendelea kama kawaida. Ifanye familia yako kuwa kipaumbele.

3. Usifukuzie kupandishwa cheo. Boresha ujuzi wako na uwe bora katika kile unachokifanya. Ikiwa wanataka kukupandisha ni sawa ikiwa hawatafanya hivyo sawa tu, wewe zingatia maendeleo yako binafsi.

4. Epuka porojo za ofisini au kazini. Epuka mambo yanayochafua jina au sifa yako. Usijiunge na genge la kejeli kwa wakuu wako na wenzako. Kaa mbali na mikusanyiko hasi ambayo ajenda yao ni kujadili watu tu.

5. Kamwe usishindane na mabosi zako. Utachoma vidole vyako wala usishindane na wafanyakazi wenzako, utakaanga ubongo wako.

6. Hakikisha una biashara ya kando. Mshahara wako hautakidhi mahitaji yako kwa muda mrefu.

7. Okoa pesa. ruhusu ikatwe moja kwa moja kwenye payslip yako.

8. Kopa mkopo kuwekeza katika biashara au kubadilisha mazingira ya kipato siyo kwa ajili ya kutumia ktk mambo ya anasa. Tumia faida kufanya starehe zako.

9. Hebu fanya maisha yako ya ndoa na familia kuwa ya faragha(siri). Waache wanafamilia wakae mbali na masuala yako ya kazi. Hii ni muhimu sana.

10. Uwe mwaminifu kwako mwenyewe na uamini katika kazi yako. Kukaa karibu sana na bosi wako kutakufitinisha na wenzako na bosi wako hatimaye anaweza kukustukia na kukutenga.

11. Jitahidi kustaafu mapema. Njia bora ya kupanga kuondoka kwako ilikuwa wakati ulipokea barua ya ajira. Wakati mwingine mzuri ni leo. Ktk umri wa miaka 40 hadi 50 uwe umestaafu.

12. Jiunge na Taasisi ya Ustawi wa kazi na uwe mwanachama hai kila wakati. Itakusaidia sana wakati tukio lolote litatokea.

13.Siku za likizo zitumie kwa kuendeleza nyumba au miradi ya siku zijazo, kwa kawaida unachofanya wakati wa siku za likizo ya mwaka huakisi jinsi utakavyoishi baada ya kustaafu. Hii ina maana kuwa kama utatumia muda huo kukaa kizembe kama vile kushinda unatazama tamthilia ktk TV yaani rimoti haitoki mikononi basi usitegemee chochote cha tofauti baada ya kustaafu.

14. Anzisha mradi ukiwa bado unahudumu au unafanya kazi. Hebu mradi wako ufanyike ukiwa kazini na ikiwa haufanyi vizuri, anza mwingine hadi ufanye vizuri kabisa. Wakati mradi wako unaendelea vizuri basi staafu ili kusimamia biashara zako. Watu wengi au wastaafu wanashindwa maisha kwa sababu wanastaafu kuanzisha mradi badala ya kustaafu kuendesha mradi.

15. Pesa ya pensheni si kwa ajili ya kuanzisha mradi au kununua shamba au kujenga nyumba bali ni fedha kwa ajili ya kukutunza au kujitunza katika afya njema. Pesa ya pensheni si ya kulipia karo ya shule au kuoa mke mdogo bali ni kujiangalia wewe mwenyewe na maisha yako ya uzeeni.

16. Kila wakati ukumbuke kuwa, unapostaafu hutakiwi kuwa mfano wa kuishi maisha duni baada ya kustaafu bali uwe mfano wa kuigwa na wenzako kufikiria kustaafu pia.

17. Usistaafu kwa sababu tu umezeeka au sasa wewe ni mzigo kwa kampuni na unasubiri siku yako ya kufa. Staafu ukiwa bado kijana au ukiwa bado una nguvu za kufurahia kuamka kwa kikombe cha kahawa, kufurahia jua, kupokea pesa kutoka kwa biashara yako, tembelea sehemu nzuri ambayo umeikumbuka na kutumia wakati mzuri na familia. Wale wanaostaafu wakiwa wamechelewa, hutumia takriban 95% ya muda wao kazini kuliko kuwa na familia zao na ndiyo maana wanaona ni vigumu kukaa na familia zao wanapostaafu lakini wanaishia kutafuta kazi nyingine hadi wanakufa. Wasipopata kazi nyingine, wanakufa mapema.

18. Staafu ukiwa nyumbani kwako kuliko katika makazi ya serikali ili unapostaafu uweze kufaa katika jamii iliyokulea. Si rahisi kuzoea kuishi katika eneo baada ya kukaa kwa miaka mingi kwenye nyumba ya kampuni au katika nyumba ya serikali.

19. Usiruhusu kamwe faida za ajira yako zikufanye usahau kuhusu kustaafu kwako. Manufaa ya ajira yanakusudiwa tu kukufanya uwe na utulivu, ujichokee wakati muda unasonga. Kumbuka ukistaafu hakuna mtu atakayekuita bosi ikiwa huna biashara inayoweza kukutegemeza.

20. Usichukie kustaafu maana lazima ipo siku utastaafu tu ama kwa hiari au kwa kutopenda.
Sisi wengine hatujisumbui kwa ajili ya kesho,leo tukishiba na kucheka na familia kwa furaha,inatosha
Kesho ni ya Mungu,maana mshahara wangu ni 400,000/=
 
👏👏
 
Na ukifika 50 usijenge kwa sababu sio mafanikio? unataka wakaishi wapi? nilifikiri nyumba ni ya kuishi sio kuonyesha umefanikiwa
 
Na hapo hujalipia choo ukiwa mjini mihangaikoni
Hujahudumia Khadija (mtarajiwa)
Hujasafiri kwenda kwenye msiba kijijini
Hujamnunulia mzazi sukari na mafuta ya taa
Hujachangia mambo ya kijamii mtaani kwako
Aisey hii nchi ina vichwa vibovu sana.
wakati wenzako wako bize kutengeneza maisha yao ya baadae wewe uko bize kumudumia khadija ambae hujamuoa na kwenda kwenye misiba.
Ndio nyinyi ambao mnajinyonga kwa kusomesha halafu jamaa anakuja kuowa kiulaini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom