Tetesi: Ushauri kwa Mtu aliyepoteza fedha mtandaoni

Ndikusyaganya

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
204
100
Hello wana jamvi,

Nina suala naomba usaidizi, bwana mdogo anafanya biashara ya TIGO pesa, mwezi mmoja uliopita alipoteza pesa kiasi ki kubwa kwa kukosea kutuma MUAMALA ipasavyo kwa bahati nzuri MTEJA alie tuma muamala huo walikua wanafahamiana. Hivyo alivyo gundua hiyo LOSS na kuahakikisha kua ndio huo hasa akamfuata mteja na mteja akaruka kwamba yeye hauisiki kwa kua si kosa lake, kosa ni la mtumaji au mtumaji ( Wakala) amtafute aliyetumiwa adai pesa zake.

Aliye tumiwa alivyopigiwa simu nae akakiri kupokea lakini hataki kurudisha kiasi kilicho zidi na kusema nenda kwenye vyembo vya sheria, inakaaje hii wakuu?

Na je wapi sehemu sahihi kuazia kufuatilia hii? Na Litarekodiwa kama kosa la aina gani?

ILIKUA HIVI:

Mteja: Naomba mtumie 97,000/= kwa hii namba... huyu ndugu yangu

Wakala: Akapokea pesa elfu 100,000/= na akarudisha chenji kwa
Mteja ambayo ni 3,000/= na kutuma pesa kimakosa Tsh
970,000/= ( LAKI TISA SABINI) badala ya hiyo 97,000/=

Msaada wa ushauri wa kisheria Tafadhali?
 
Back
Top Bottom