Ushauri kuhusu magari

dr shayo

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
555
974
Baada ya kujichanga changa hapa nimeona nivute chuma. Lakini siyo mpya nataka ninunue mkononi kwa mtu. Nilikua naomba ushauri wa gari zifuatazo kwa maana naona zinauzwa bei ndogo nikatia shaka:
1)Mazda, hapa nazungumzia Demio na Tribute
2)Mitsubishi mini
3)BMW mini Cooper
4)Honda fit
Je, kati ya hizi gari ipi ni nzuri kwa town trip na upatikanaji wa spares zake ukoje?
 
Ngoja wataalamu waje, ukifanikiwa kununua siku ukihitaji spare parts hasa body parts nitafute mkuu nitakuuzia kwa bei ya punguzo.
 
Mini ni gari nzuri sana kwa spec zake. Yani iko juu juu, breki nta, iko very stable (ukidondosha Pajero mini unapewa tuzo ya Nobel 😀).
Tatizo ni kabovu bovu.
Demio pia sikuipenda. Haikimbii sana...

Bora utafute mtu mwenye Vitz kali umvue.
 
Mini ni gari nzuri sana kwa spec zake. Yani iko juu juu, breki nta, iko very stable (ukidondosha Pajero mini unapewa tuzo ya Nobel ).
Tatizo ni kabovu bovu.
Demio pia sikuipenda. Haikimbii sana...

Bora utafute mtu mwenye Vitz kali umvue.
Ubovu wake kwa kawaida ni kwenye nini hasa mkuu?
 
Tafuta Toyota kama unahitaji used za hapa TANZANIA Achana na brand tofauti na Toyota hasa zilizotumika na watanzania...
Vitz, starlet, IST,platz,Carina, corolla,premio,probox na raum haya ndiyo magari yatakufaa na utafurahia thamani ya pesa zako
Toyota brand kwenye hizi baby walker labda starlet turbo kidogo ndo itanibariki mkuu.
 
Baada ya kujichanga changa hapa nimeona nivute chuma. Lakini siyo mpya nataka ninunue mkononi kwa mtu. Nilikua naomba ushauri wa gari zifuatazo kwa maana naona zinauzwa bei ndogo nikatia shaka:
1)Mazda, hapa nazungumzia Demio na Tribute
2)Mitsubishi mini
3)BMW mini Cooper
4)Honda fit
Je, kati ya hizi gari ipi ni nzuri kwa town trip na upatikanaji wa spares zake ukoje?
Demio ni gari simple kwa road trip na consuption yake ya mafuta iko vizuri, Kuhusu spea azisumbui zipo za kutosha apo ilala na zipo affordable.
 
Baada ya kujichanga changa hapa nimeona nivute chuma. Lakini siyo mpya nataka ninunue mkononi kwa mtu. Nilikua naomba ushauri wa gari zifuatazo kwa maana naona zinauzwa bei ndogo nikatia shaka:
1)Mazda, hapa nazungumzia Demio na Tribute
2)Mitsubishi mini
3)BMW mini Cooper
4)Honda fit
Je, kati ya hizi gari ipi ni nzuri kwa town trip na upatikanaji wa spares zake ukoje?
hizo zote zitakupasua kichwa nambie offer yako nikwambie gar zitazokufaa
 
Siku Tanzania tukiamua kuachana na mambo ya kukariri na kukatishana tamaa, badala ya kutoa ushauri kutokana na inavyohitajika. Tutapiga hatua kubwa sana.
Ndio maana sijaweka toyota brands mkuu maana hizo ndo ninazoziona zipo nyingi mjini.
 
Ingia kwa mchina kuna magari mazuri tu...

Si una ona mwenyewe sasa hivi tuna mabasi ma yutong, nk

Maroli ndio usiseme FAW nk hakuna tena cha Isuzu, mitsubishi nk

Ukija ktk pikipiki utachoka wewe...

Bado tuna subiria ndege zake anazofanya majaribio ili tuachane kabisa na haya ma airbus sijui dream nni...

Mchina ana vyuma, bei ina eleweka tena vyuma vipyaaaaa...

Nakusisitiza ingia china hapo tafuta chuma kimoja matata... alafu kaa na namba ya agent aliyekuuzia mzigo, spea kuipata ni chap tena mpyaa...
 
Ndio maana sijaweka toyota brands mkuu maana hizo ndo ninazoziona zipo nyingi mjini.
Mkuu tatizo sio brand angalia mfuko wako kwenye spea utaweza kumudu

Wa Tanzania sio kama wanapenda kuishi kama wanafunzi wa shule kuvaa sare hapana
Asilimia kubwa uchumi wetu unalingana
Ila ndio hivyo hatupendi kusema ukweli tu

Unaweza ukanunua Toyota na Bado ika paki ndani
So be careful na angalia mfuko wako

Tena zingatia unataka mkononi kwa MTU

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom