Updates: Mbowe ndani ya Kanda ya Ziwa Victoria

Dec 11, 2010
3,321
6,328
The Leo mwenyekiti wa chama Taifa kamanda Freeman Mbowe yuko kanda ya ziwa Victoria inayo undwa na mkoa wa Mwanza, Kagera na Geita kanda hii pia inafahamika kama kanda ya ziwa Magharibi, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kuimarisha mfumo wa kanda za kichama chini ya CHADEMA.

Ziara hii ni muendelezo wa ziara iliyo anzia kanda ya Pwani (Dsm na Pwani), kanda ya ziwa Serengeti ambayo pia inafahamika kama kanda ya ziwa Mashariki (Mara, Simiyu na Shinyanga), ikafuatiwa na kanda ya kati (Dodoma, Sindiga na Morogoro), kisha ziara kama hii ikafanyika pia kanda ya kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara), na kanda ya Nyanda za juu Kusini (Ruvuma, Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa).

Ziara hii ya kanda ya ziwa Victoria itakuwa na vikao vitatu muhimu ambavyo ni kikao cha kamati tendaji ya kanda, kikao cha baraza la uongozi la kanda na kisha kikao cha wadau wa kanda. Leo mwenyekiti Taifa kabla ya kuanza kikao cha baraza la uongozi la kanda alipata fursa ya kufungua kongamano la vijana kupitia program ya FTP200 inayo husisha vijana wa redbrigade kutoka maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa Victoria ambapo watapata mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali, ulinzi shirikishi na elimu ya stadi za maisha.

Kesho kabla ya kikao cha wadau wa kanda ya ziwa Victoria kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara utakapo fanyika katika uwanja wa Furahisha kuanzia saa tisa mchana, mkutano huo utaongozwa na mwenyekiti wa chama Taifa na Naibu katibu mkuu Zanzabar kamanda Salum Mwalim pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa chama.

Tutaendelea kujuzana...

Akihutubia waandishi wa habari wakati wa ufunguzi Mheshimiwa Mbowe alitoa kauli zifuatazo kuhusu mauwaji ya Albino.

"...Wanao uwa wana chama wa Chadema au kuwabambikizia kesi za ugaidi na kuwatesa wanapandishwa vyeo, huku ndugu zetu Albino wanauwawa waziri mkuu analia lia bungeni hakuna hatua za dhati zimesha chukuliwa mpaka sasa huku mauwaji yakizidi kuendelea kila mara..."

"...Hatuwezi kukubali kuwa Taifa lenye viongozi wanao kubali kuona Albino wana uwawa kinyama halafu bado tukajiona tuko salama, lazima tufanye maamuzi magumu kuokoa kizazi cha Taifa hili, Haiwezekani Albino waishi kwa kuwindwa kama wanyama kwenye nchi inayo jiita huru..."

"...Bado hakuna jitihada za dhati za kukomesha mauwaji, kuna mauwaji ya vikongwe ambayo ni sawa na laana kama kuua Albino kwenye Taifa hili yamekuwa yanafanyika... Hatuwezi kuwa na Taifa lenye raia wanaofikiria kuishi au kupata ridhiki kwa kuua wanzao halafu bado serikali haionyeshi nia ya dhati kukomesha mauwaji hayo..."

Kuhusu BVR.

"...Mpaka sasa tume wameshindwa kuandikisha wapiga kura kwa ufanisi kwenye mkoa wa Njombe mji wa Makambako kwenye kata tisa, watu wana Ari ya kwenda kujiandikisha wanaamka saa tisa usiku kwenda kupanga foleni wanakaa kwenye foleni kwa muda mrefu bila kuandikishwa... "

"..hatuta kubali kuona tume ya Taifa ya uchaguzi inafanya hila za kuto kuwaandikisha watu wenye sifa kwa sababu zozote zile, tume wajue kuwa Chadema haiko tayari na haita kuwa tayari kuona wananchi wenye sifa za kuandikishwa wanaachwa kwa kuwa kuandikishwa ni haki ya kikatiba...."
attachment.php
 

Attachments

  • 1425118111270.jpg
    1425118111270.jpg
    66 KB · Views: 2,491
  • 1425118170369.jpg
    1425118170369.jpg
    92.8 KB · Views: 1,875
  • 1425118198939.jpg
    1425118198939.jpg
    42.1 KB · Views: 1,867
  • 1425118221080.jpg
    1425118221080.jpg
    79 KB · Views: 2,187
  • 1425118239771.jpg
    1425118239771.jpg
    49.1 KB · Views: 3,497
Kila la kheri hakikisheni elimu ya uraia inawapata kila mpiga kura.
 
Najivunia kuwa mwanachama hai wa chadema...nahidi sitokiacha chama hata kama dr. Slaa na mbowe wakikisaliti mi ntabaki chadema...mungu nisaidie.AMEN.
 
Hakika kazi mnayoifanya ni ya kutukuka! Tumeanza na Mungu, tutamaliza na Mungu!
 
Dhamira yetu ni njema sana,kwa watu wema.Hakika ukombozi umekaribia Watanzania endeleeni kuliunga mkono jeshi hili la ukombozi,chini ya Jemedari,Kamanda wa anga,Freema Mbowe.
 
magamba yanatetemeka kila kona... hapo kwenye red brigade wajitahidi kuwaajiri wale waliohitimU JKT ili wasaidie kuwakabili raia wakakamavu wa ccm
 
Safari ni ndefu na ngumu lakini dalili za kufika ni kubwa!

nikweli tumepita kwenye mabomu,kutekwa na kuteshwa na green gurd na policcm ila kwa jeshi hili la kila kata likiongozwa na kamanda mbowe,tunaenda kuvuka mapita hayo na kufikia inchi ya ahadi.
 
chadema ni mpango wa Mungu!


nitakuja viwanja vya furahisha kwa garama zangu sio kusombwa na lori kama kifusi


delete futa kabisa ccm
 
hiyo kanda ndo inayoaamua nani anakuwa rais wa nchi hivyo juhudi kubwa zinahitajika
 
Back
Top Bottom