Ungekuwa na Mamlaka Serikalini, ungefanya nini kuikuza Tanzania kiuchumi bila kumuongezea mzigo mwananchi?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,197
4,120
Kama ungekuwa na uongozi ngazi za juu, ungekuwa au kuja na mpango au mbinu gani ya kuikuza Tanzania kiuchumi bila kumtwisha mzigo wa kodi au makato mengine mwananchi?

Kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusu mzigo wa kodi au tozo kwa wananchi, huku watu hao wakiwa na hoja ya Tanzania ni nchi iliyobarikiwa rasilimali nyingi sana hiyo zikitumiwa vizuri nchi itakuwa kiuchumi maradufu huku wananchi wakipunguziwa mzigo wa tozo na kodi ambazo zinaonekana kuwaelemea.

Katika kuzingatia hoja hizo ungekuwa wewe una nafasi ya kufanya maamuzi ungefanya jambo gani, mbinu gani au mipango gani ili kutumia rasilimali na fursa zilizopo kuzalisha ili kuongeza pato la Taifa na hivyo Tanzania iweze kupaa kuichumi na wananchi tupate maisha yale ambayo wengi tunayatamani kwa angalau thamani ya fedha yetu iweze kupaa juu.
 
DIGITALISE ALL GOVT SYSTEMS!/ VERIFICATIONS SYSTEMS
Tunahitaji framework mpya, katika taifa letu, hasa katika maswala yote ya kikodi, kwa mechanism iliyopo 50% ya mapato ni lazima yapotee, na si kwa uzembe wa yeyote!

- Kuna ubaya gani kukodi wataalamu UK, Waje kututengenezea njia?
Digital economy ndiyo jawabu na adui mkubwa wa wakwepa kodi.

HATA MAOFISA WA TRA, WAO WATAKUWA NA GIANT SCREEN ZA KUMONITOR TU./PIA WENGI HAWATAHITAJIKA BY 50%
  • Nikinunua luku, kodi na vat zitasoma instantly!
  • Nikinunua kwa swap card, vat na kodi zitasoma instantly!
  • Nikipanda daladala kwa swap, vat na kodi vitasoma instantly!
  • Naingiza gari bandarini, naquest system, na print car info / kibati cha infos, automation system inaleta kiasi cha kulipa, na control number nalipa, natoa gari, no longolongo!

Machinga ni pakacha kubwa mno la kuvujisha kodi,maana wanauza vitu kama vile vya madukani!
 
Kwa kifupi bila kufafanua,

1: Kupunguza matumizi ya serikali angalau 30%

2: Wabunge mshaara milion 5 kwa mwezi,Gari Toyota RAV4

3: Hakuta kua Na Wakuu wa Mikoa Wala wakuu wa Wilaya

4: Watakao tajwa kwenye ripoti ya CAG mahojiano watafanya wakiwa UKONGA

5: MAFISADI wapiga deal,vishoka,hakuna kuwachekea
 
DIGITALISE ALL GOVT SYSTEMS!
Tunahitaji framework mpya, katika taifa letu, hasa katika maswala yote ya kikodi, kwa mechanism iliyopo 50% ya mapato ni lazima yapotee, na si kwa uzembe wa yeyote...
Hili naunga mkono. Nilishafikiria hivi siku nyingi sana. With technology, everything is possible. Kuna uwezekano wa kila mwananchi kuweza kufuatilia mapato na matumizi yote ya serikali kwa kutumia hii njia.

Lakini nina uhakika CCM hawatakubali kwa sababu wanajua hawataweza kuiba kwa urahisi tena. hata Samia mwenyewe hawezi kukubali.
 
Kama ungekuwa na uongozi ngazi za juu, ungekuwa au kuja na mpango au mbinu gani ya kuikuza Tanzania kiuchumi bila kumtwisha mzigo wa kodi au makato mengine mwananchi...
Mazingira na mazuri sana kwa chochote kufanyika humu nchini.....

Ningehamasisha na kusisitiza watu waache uvivu wafanye kazi kwa bidii sana, bila kuchoka wala kukata tamaa hasa kazi za, kilimo, ufugaji na biaashara 🐒
 
Kwanza matumizi makubwa ya fedha kwenye Serikali na Taasisi zake, mishahara na posho za wabunge, ningehakikisha nawapiga wabunge na perdiem ya 240,000/= angalau mara mbili ya perdiem za watumishi wa UMMA, mishahara yao ningeifanya nusu ya wanayokula sasa, ningehakikisha rushwa inakuwa adui wa Taifa kweli.

Zaidi sana ningehakikisha kila raia analipa Kodi kadiri anavyostahili, gari za Serikali zisingekuwa za anasa, zingejaa land cruise mkonga tu huko Serikalini.
 
1: Ma Vx V8 ibakie kwa Mh. Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu basiii, wengine wooote watumie Prado tu..!!

2: Futa viti maalum wote katika bunge

3: All tax payment must be digital, no cash payment..!! Hii iwe very serious..!!

4: Miradi mikubwa yote iekewe ulinzi mkubwa kuhakikisha isiwe over estimated ili itumie fedha yenye value sahihi, mfano mradi mdogo tu wa maji unaambiwa Bil 10..!! Lazima uhakiki ufanyike kwa umakini kwenye projects zote kubwa kubana over estimation ya miradi, hasa barabara za lami etc

5: Kilimo kiwe Uti wa mgongo wa Tanzania then connect kilimo na viwanda vyetu

6: Mazao ya kilimo yaongezewe value kwa kupitishwa ktk viwanda vyetu, tuuze nje processed products, sio raw materials

7: Panua barabara za mikoani, uchumi ni barabara siku hizi..!!

8: Serikali iteue viongozi wa Umma hasa wakurugenzi wa halmashauri au watendaji wakuu wa taasisi mbali mbali kwa competence based na sio based on politics..!!
 
Kwa kifupi bila kufafanua,

1:kupunguza matumizi ya serikali angalau 30%

2:wabunge mshaara milion 5 kwa mwezi,Gari Toyota RAV4

3:Hakuta kua Na Wakuu wa Mikoa Wala wakuu wa Wilaya

4:watakao tajwa kwenye ripoti ya CAG mahojiano watafanya wakiwa UKONGA

5: MAFISADI wapiga deal,vishoka,hakuna kuwachekea
Well
 
Kama ungekuwa na uongozi ngazi za juu, ungekuwa au kuja na mpango au mbinu gani ya kuikuza Tanzania kiuchumi bila kumtwisha mzigo wa kodi au makato mengine mwananchi?
...
Well Mikopo ya miradi inatuua kila mwaka lazima tukope kila awamu lazima tuanzishe mradi mpya.

Ingekuwa mimi ndo Rais potelea pote watu waseme wawezavyo hata kama risk nikupoteza kiti kwa kura za wabunge Sitaanzisha mradi wowote katika awamu yangu ili kusiwe na mikopo mipya na tupunguze ile ya zamani lengo ni hela zinazobaki ndani ya nchi ziwe nyingi kuliko zinazotoka "tunalipa hela nyingi sana huko nje"

Mean while nitakachofanya ni
1. Kumaintain miradi iliyopo iweze kufanya kazi vizuri

2. Kushughulikia Katiba mpya ili tupate sheria mpya zitakazoweza kuleta maendeleo katika kila angle na ambazo zitafanya mifumo na mashirika ya serikali yaweze kufanya kazi kwa ufasaha Automatically sio jiwe akiondoka kila kitu kinaondoka

LENGO: Ni kufocus na mambo machache yatakayoleta tija kubwa na sio kufanya utitiri wa mambo ambayo hayana tija in the long run.

Mwisho nimshukuru mama samia kwa huu uzi😂😂
 
Ingekuwa mimi ndo Rais potelea pote watu waseme wawezavyo hata kama risk nikupoteza kiti kwa kura za wabunge Sitaanzisha mradi wowote katika awamu yangu ili kusiwe na mikopo mipya na tupunguze ile ya zamani lengo ni hela zinazobaki ndani ya nchi ziwe nyingi kuliko zinazotoka "tunalipa hela nyingi sana huko
Mkuu hii ni Point kubwa sana.

Mikopo wanayokopa inawanufaisha wao kwanza kuliko wananchi.

Ndio maana kila anayeingia anaanzisha Mradi wake kwanza kabla ya kumaliza iliyopo.
 
Makaa ya mawe na gesi ningezalisha products zinazotumia hizi two items na kuziuza karibia Africa nzima zikiwemo malighafi za kuzalisha chupa za maji na mbolea.

Na pia ningetumia Saso technology ya kuzalisha Petro chemicals (ikiwemo Petrol, Diesel na Mafuta ya taa) kutokana na makaa ya mawe na Gesi asilia.

Tanzania ingekuwa inajipatia zaidi ya Dola billion 100 kwa mwaka na kufanya Watanzania wapate huduma zikiwemo Afya,umeme,Elimu na Makazi( free 3 Bedroom Apartment) kwa Kila Manzania.

Yes inawezekana just in investing in coal and Gas dhahabu, Almas, Lithium tukiongeza na hizi 3 Tunaipita at Saudi kwa utajiri na Ustawi
 
Back
Top Bottom